Jumanne, 25 Oktoba 2016

ILIKUWA NGUMU ILA ILIKUWA INAWEZEKANA!



ILIKUWA NGUMU ILA ILIKUWA INAWEZEKANA!


Ndani ya dunia kuna vitu ukiviangalia kwa macho ya kawaida tu, unaweza kuibua maswali mengi sana kichwani mathalani hivi ili jambo lilianzaje? Hivi huyu mtu alifikiria nini mpaka kutengeneza kitu kama hiki? Hivi huyu mtu alipata wapi ujasiri wa kuamini kuwa anaweza kutengeneza kitu kama hiki? Huyu mtu aliweza vipi kukamilisha jambo hili wakati uchumi wake hauwezi kumwezesha? Mpaka kufika hapa aliweza vipi kumudu changamoto zilizo mkabili na hatimaye kufikia hapa?

Ni kweli kuna wakati unaweza kuwaza sana ukashindwa kupata jibu lililo sahihi pindi unapotazama majengo ya kifahari yalivyojengwa katika muundo wa kisasa na wakupendeza! Hama vyombo vya moto mathalani gari hama pikipiki katika miundo mbalimbali sana ukashindwa kupata jibu lililo toa majibu katika maswali yako.

Pia unaweza kuona mtu kainuka na kuwa mahali fulani pa juu sana ukashikwa na butwaa na wasiwasi hivi kweli huyu amefikaje hapa? Nami naweza fika hapa nami  ni kawa pale au nikawa zaidi ya pale, yote yanabaki kuwa ni maswali katika akili yako katika kutafuta uwezekano wa kufika pale ambako macho yako yanatazamia.

Wako watu wakiangalia mambo wanajisikia wanyonge sana kwa sababu kama huyu amefanya haya ata mimi naweza lakini sijui kama nitaweza kufikia hapa lazima utambue kuwa yeye anatangulia wewe utakuja kukamilisha kufanya kitu kilichobora zaidi kwakua kitakuwa kimefanyika kwa namna yako na sio kwa namna yake.

Katika hali ya kawaida hapa duniani wako watu ambao wanajitahidi kuwa miili wanayoipenda hasa wale walio na maumbo makubwa wanao taka kuwa na maumbo madogo uwa utumia njia mbalimbali kuhakikisha kuwa na maumbo madogohivyo ulazimika njia mbalimbali ambazo ziko njia nyingine zinaumiza sana lakini ndizo njia sahihi wanazo amini katika kuwa na muonekano ulio mzuri machoni pao au muonekano kwa watu wengine.

Niseme wazi katika maandalizi ya kufikia mahali fulani kuna maandalizi ya akili katika kutengenezwa ili kuweza kuyakabili mazingira mageni kuna kipindi cha mpito katika kuandaa akili yako kupokea mazingira mageni na katika mazingira haya unaweza kupita kwa kujua hama kutojua jua ila mara nyingi sio mara zote katika maisha haya yanafanyika pasipo kujua ila baada ya kupitia kipindi utaingizwa katika mazingira ambayo utaona akili yako ikitumika kwa ufanisi wake.

Lazima akili yako itambue tu kama jambo limefanyika basi kuna gharama mtu ameingia mpaka kufikia hapo na kamwe usiipe akili yako wakati mgumu kuwa kwakua ni gumu basi haiwezekani kufikia lengo langu! Tambua kila ugumu una sababu yake na upo kwa ajili ya kukufanya kuwa mtu maalum kwa ajili ya kazi maalum.

Unapoliona jambo lolote usijijengee hofu au kuto wezekana bali tambua linawekana kwakua uwezekano wa kufanyika upo basi itakuwa hivyo kwa namna yoyote hiyo, japo sio lazima lililofanyika basi nawe ulifanye hivyo kwakua kila mtu ana upekee wake utafute upekee wako nawe utakuwa katika hatua iliyo bora yenye tija kwako na kwa jamii husika.

Hivyo unapowaona watu wengine au vitu vingine usijijengee hali ya kutofanya vizuri kwakua mwenzako amekifanya katika kiwango kizuri bali tambua utofauti utatokea kwakua kila mtu atafanya kwa namna yake na bila shaka itakuwa nzuri.

Ugumu wa jambo usijenge hofu au hali ya kutoweza bali tambua ugumu upo kwa ajili ya kukufanya uwe imara sana na kitu kuwa kizuri zaidi, hivyo ni vizuri kutambua kuwa huo ugumu upo ili kuwezesha akili yako kuzidi kumtegemea Mungu.

ANAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 18 Oktoba 2016

DAKIKA MOJA KWA MUNGU NI NYINGI.



DAKIKA MOJA KWA MUNGU NI NYINGI


Katika siku kuna masaa 24 au dakika 1440 hama tunaweza sema kuna sekunde 86400, na katika dunia tunayoishi kuna mambo yanafanyika kila lisaa, kila dakika na mengine kila sekunde na tukumbuke katika kipindi kuna mambo tofautitofauti yanatokea ziko hali za asili kama kuvuta pumzi na kutoa na wengine katika hali za kawaida, kwani wako watu wanaoanza kucheka na wengine wanamalizia kucheka, wako wanaoanza huzuni na wako wanamalizia/ huzuni inakoma na wengine wanamaliza kulia na wengine wanaanza kulia.
 
Ndomana unaweza usishangae kukuta huyu anafukuzwa kazi na mwingine anapata kazi, na wengine uchumba unavunjika na kwa wengine unaanza na mambo mengi yanatokea na kuwa katika hali ya mbadilishano, kwa kusema hivyo tujue kile kinachompata au kukikosa sio kila mtu uweza kuwa katika hali hiyohiyo (vitu au hali hazifanani),

Biblia inasema;
Mwanzo 8:22  Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Kwahiyo hatuna shaka na hili maadam DUNIA inaendelea kuwepo basi namna yake itaendelea kuwepo kwa jinsi yake sawa na asili yake.

Ni kawaida tunatambua utendaji wa mtu uamliwa na uwezo wa uchumi alionalo pamoja na matamanio ya moyo wake naam kuchelewa/ kuwai  kufanikisha jambo lake mara nyingi utegemea uwezo wa kulifanikisha (fedha, mikakati na dhamira ya dhati)

Ni vizuri kutambua kuwa utendaji wa jambo linalokukabili mathalani unaweza kuishi katika hali ya kutoifurahia kwa muda mwingi na ukahisi kuwa hayo ni maisha yako hivyo ahunabudi kuyaishi lakini utokaji wa mahali hapo kwa mkono wa Mungu “sekunde” inaweza kubadilisha historia yako.
Kwahiyo siku moja katika muda mchache unaweza kuzalisha hali njema katika maisha yako ikaifanye siku yako kufungwa hiki hiacha akili katika hali ya kutaharuki kwa namna ilivyofanyika ikitoa njia katika macho ambayo akiwa kawaida.

Kuna wakati mwingine inakuwa ngumu sana katika kutoka katika hali moja na kwenda katika hali nyingine iliyo njema sana kutokana akili zetu kuwa tofauti na uwezo wa akili ya Mungu tunafikiri utendaji unaoaminika katika akili zetu ndio unaohakisi mtazamo wa akili ya Mungu.

Ahutaji kuhesabu msoto wako kwani moyo wako utashuka bali tambua dakika ya Mungu yawezafuta historia ambayo inaweza kuwa neno  moja tu lililochukua sekunde mbili, likarejesha nguvu na matumaini mapya katika maisha yako linaweza kuwa  SAWA! UNAWEZA KUENDELEA! IMEKUWA!

Changamoto ya watu wengi walionao ni kutaka akili za Mungu zifanane na wanadamu pasipo kujua akili za mwanadamu  katika hali ya mwili hazina mwanga wa uhakika.

Waamuzi 16:28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.

Tunaona Samson anafanyika kuwa mkombozi wa Israel japo kuwa waliishi utumwami muda mwingi lakini ukombozi wa kiMungu haukuchukua miaka mingi bali ndani ya siku moja katika masaa machache furaha ikarejea katika himaya ya watu wa Mungu.

Nakubaliana kuwa utendaji wa Mungu uko katika namna mbalimbali yapo mambo yanachukua muda kutokana akili ya mtu kushindwa kuhimili huo utukufu lakini inaweza kuchukua muda mfupi ajabu na ikabadilisha kabisa maisha yako.

Mungu hayupo kukuchosha wala kukudhalilisha bali ni katika hali ya kukufanya uwe na maandalizi bora ya kufaa kwa ajili ya ufalme wake katika nafasi atakayo kupa utumike.

Usitazame jambo katika ukubwa wake ikakuonyesha kuchukua muda mwingi katika kuishia/utatuzi wake bali tambua inahitaji kauli ya Mungu tu itakayochua chini ya dakika na mambo yatafanyika tu!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 11 Oktoba 2016

ACHA NIIKABILI KESHO YANGU!



ACHA NIIKABILI KESHO YANGU!


Imekuwa kama fumbo katika kuiongelea “KESHO” wakati mwingine kwa hofu au hali ya kutokuwa na uhakika wa kuwa vile mtu anavyowaza hama vile anavyotazama ndivyo itakavyokuwa, na ndomana unaweza usishangae sana mtu anaposema “KESHO TUKIJAALIWA” hama mtu akisema wakati mwingine” MUNGU AKITUPA NEEMA” bila shaka wako watu wengine kutokana na uhakika unaombatana na macho yao wanasema KESHO ITAKUWA SAWA au KESHO NITAKAMILISHA  kwasababu jambo hili ni dogo sana!

Wakati mwingine nikubaliane kuwa KESHO kama fumbo kwani unaweza kujigamba sana na wakati mwingine ukaona kama unamiliki kila kitu hivyo ukatumia LEO namna unavyo ona na KESHO ikawa vile unavyopaswa kuwa na sio unavyopenda.

Niseme tu kumekuwa na maana nyingi kuhusu KESHO na ni nzuri sana kwa maana wakati mwingine zinakuwa zimebeba ushawishi wa akili na hata kusadifiwa na mazingira yanayozunguka na namna unavyoona mambo yanavyotendeka.

KESHO KAMA HATUA INAYOFUATA KATIKA MAISHA YAKO!
Katika maisha kuna mwingiliano na muachano wa vitu vingi kuna vitu vinatoka na vingine vinaingia, uzuri ni kwamba kila mtu uomba usiku na mchana kuona KESHO yake inakuwa nzuri hata mtu kama yeye mwenyewe ahusiki kuifanya kuwa kesho iliyo bora.

Wako wajawazito wanaitamani kesho yao kupakata watoto wao wakiwa na furaha na amani na wakiona heshima yao imerudi hama imekuwa kubwa katika jamii na wakati mwingine kuona kama kaongeza heshima ukweni, lakini cha ajabu wako wenye mipango ya kuikimbia kesho yao kwa maana yakutaka kutoa mimba kwa sababu nyingi tu ambazo ufahamu wa mtu huyo utamdanganya mathalani huu sio wakati sahihi wa mimi kuzaa, baba wa mtoto amtaki mtoto wake, hama sikupanga kumzaa na mtu kama huyu!

Wako watu wamekuwa na uwoga katika kupandishwa cheo kwa hofu kuwa hivi hizi changamoto zake naweza kuzikabili hama naweza kufikia mafanikio yale niliyoaminiwa kwayo, wakati mwingine uweza kuwa na maswali ni kweli naweza kupata ushirikiano mzuri wa kuniwezesha kutimiza malengo…….. ujue kwamba aliyekupa nafasi hiyo amekuamini na kujua unaweza kufanya vizuri na kama kunauwezekano wa kuweza basi utaweza! 

Pia kuna watu waliomaliza hatua fulani ya masomo yao inawezekana kuwa mtu alisoma nje sasa anawaza nitakaporudi nyumbani ni kweli nitaweza kufanikiwa katika lengo langu anaweza kuwa alifuatilia watu wanamna yake jinsi walivyo sasa wako walio fanikiwa katika njia zisizo halali na wengine hawajafanikiwa,

 Na wengine walio maliza nchini wanaona maisha ya waliotangulia jinsi yalivyo kwa asilimia kubwa sio ya kuvutia kwa maana sikuhizi sio jambo la kushangaza mtu mwenye stashahada kuwa mmachinga wa kutembeza nguo barabarani!

Pamoja hayo ikumbukukwe kuwa kama hakuna mabadiliko basi hakuna maendeleo” No change No improvement”

Jifunze kuyafurahia mabadiliko yenye tija kwako ili yawe rahisi katika kuyakamilisha hata kama yana ugumu gani kwa kuwa moyo wako utakuwa tayari kupambana na chochote ili mradi tu utimize lengo lako

Ikumbuke kuwa vile ulivyoishi leo sio utakavyoishi kesho kwakua changamoto zake ziko tofauti mathalani unapokuwa pekee yako ni tofauti utakapoamua kuwa na mtu mwingine lazima ujiandae katika kubadilisha mtindo wako ili uweze kuifurahia kesho yako na isiwe mzigo kwako.

Ni kweli watu wanaogopa kuiikabili kesho wakati mwingine mtu kulizika vile alivyo hama kuipenda leo yake na asione umuhimu wa kesho yake, pasipo kujua inawezekana leo una nguvu ndo mana unaifurahia lakini kesho unaweza usiwe na nguvu hizo na kushindwa kuimiri kishindo cha kesho ukabaki katika lawama na hata majuto………ni kweli leo sio kesho!

IPENDE KESHO YAKO ITAKUWA NZURI!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 4 Oktoba 2016

UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE.



UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE


Kwa maana ya haraka haraka unaweza kushindwa kuona uhusiano wa karibu kati ya haya maneno mawili UGUMU na UBORA! Kwa maaana ya kawaida kitu kigumu kinahusishwa kitu kibaya hama kitu ambacho kinachohitaji nguvu nyingi ili ukipate na pindi unapokikosa basi huitwa KUJICHOSHA hivyo hapo swali uweza kujitokeza katika mwisho wa namna hii, UBORA utatoka wapi?

Kuna namna lazima uwe ili uweze kuvipata vitu ambavyo havipatikani kwa urahisi………….uwezi kufananisha maisha ya mtu anayetafuta dhahabu kama mtu anayetafuta ng’ombe.

Ifahamike kuwa watu upenda kitu sio kwakua ni kigumu tu, kwa maana ya kukaa muda mrefu bali kwakua ni bora! Kwa maana kinakuwa na tija ile iliyokusudiwa,

Na ikumbukwe kuwa ugumu wa kitu utegemea nini kimfanya kuwa na ugumu na ubora wa kitu utegemea kile kinachotoka/kinachozalisha!

Katika  picha ya kawaida tu, uwa tunaamini kitu kigumu ndicho kinachodumu basi hapo tuna amini kuwa chenye ugumu ndipo hapo kuna ubora! Japo wakati mwingine sio kweli kwani sio kilicho kigumu kina ubora kwa kuwa vingine vinakuwa vimekomaa hivyo vinakuwa havina faida zaidi ya maumivu.

Samahani naomba niuongelee upande huu japo sio dhima ya ujumbe bali yote ni kukupa mwanga zaidi katika kile ninachotaka uimarishe akili yako ikawe katika njia inayostahili, watu wengi wana amini kuwa msichana mgumu ndio bora kwa kuwa sio rahisi kutoa jibu sawa hama nimekubali kuwa mtu wako katika kuanzisha safari ya kuwa pamoja! Swali langu alipo katika ugumu au uwepesi bali msingi wake/akili yake imeshikiliwa na nini katika kutoa jibu la kusema ndio au hapana……kwa maana rahisi katika hali hii uwezi kusema UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE! Japo wakati mwingune inaweza kuwa sawa lakini sio mara zote.

UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE!

Ni jambo la kawaida unapoendelea kusaga nafaka ndipo unawezidisha ulaini(kupondeka) wa hicho kitu unachokisaga!

Bila shaka unapotaka kutengeneza maandazi mazuri basi ahunabudi kukanda vizuri ngano  hatimae ile ngano yako iweze kuwa laini na hapo kutengeza ubora wa maandazi yako na kuzidi kutamaniwa na watu wengi!

Hakuna shaka ukitaka samaki wakubwa na wenye uzito mkubwa ahunabudi kuingia vilindini zaidi katika maji kule waliko ndipo uweze kupata  mbali na hapo utaishia katika kupata wale waliosawa na kina kile ulichoingia.

Unapoangalia katika ufalme wa giza unaweza usiuelewe lakini wenyewe unajitambua na kuhakikisha unakuwa pale panapohitajika na sio chini ya lile kusudio kwa kuwa chini  ni ishara ya kushindwa katika utawala wake, ndomana wako radhi kutoa uhai wa mtu yeyote katika utawala uliondani yao ili mradi kudumisha ufalme wao.

Na ukiingia ndani zaidi utatambua nafasi ya mtu utegemea uwezo wake katika sadaka inaweza kuwa miili ya watu, vichwa hama watoto wachanga, ukubwa wa sadaka ndio ukubwa wa mtu husika.
Na ndipo unaweza kuunganisha kuwa mateso ya mtu ndio nafasi ya mtu katika utawala wa ufalme huo kwakua sadaka kubwa inatakiwa kujitoa na kuteseka zaidi ili uweze kukamilisha ile shehena unayotakiwa kuileta katika ufalme huo.

Kwa maana rahisi katika ufalme huo sadaka yako ndiyo inayoamua nafasi katika ufalme iwe kubwa au ndogo sio kitu kingine kwakua uko ndiko kunaitwa kujidhabiu.

Unaweza kumuona mtu kuwa na muonekano na fahari yake ya kuvutia na ya kutisha lakini kamwe usijue UGUMU anaoupata katika kuhakikisha anakuwa hapo, mateso ya usiku wengine wanaambiwa kulala katika banda la kuku! Uwa ahuhitaji maswali zaidi ya kutekeleza.

KATIKA UPANDE ULIO BEBA USALAMA WA MAISHA!

Katika kuhakikisha ufalme kuwa na nguvu na kuzidi kuwepo kwa kishindo kisicho zuiliwa ukweli unahitaji watu, na sio kwa maana ya watu bali unahitaji watu waliotayari kuutumikia ufalme huo kwa moyo uliobeba dhamira njema ulio na maongozo ya Roho mtakatifu.

Bila shaka ukiona ufalme umelala basi tambua watu wake wamefanya ulale au watu wenyewe wa melala na ukiona umeanza kushamiri basi tambua watu wake wameamua kuutumikia.

Namna unavyojigharimu katika kuhakikisha ufalme unasimama na kuimarika basi nawe unazidisha nafasi yako mbele za Mungu na kanuni alizoziweka Mungu kuanza kuchukua nafasi katika maisha yako, katika kukufanikisha.

Mwanzo 22:15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
                    16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
                    17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Sio lazima utoe sadaka kubwa la kwanza yatoe maisha yako kwanza kuhakikisha ufalme wa Mungu unajengwa na mengine yatakuwa sawa,

Ukumbuke kuwa namna unavyojitoa ndivyo unavyotengeneza nafasi yako kwa Mungu, hivyo usijitoe kidogo ukategemea kuyapata makubwa kwa Mungu,

Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535