Jumanne, 27 Desemba 2016

MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU!

MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU!


Kama bahari inavyo hifadhi vitu vingi na hata kufanya viumbe viishi na kuimarisha mzunguko wao pamoja, kwakua ndani ya ulimwengu viko vitu mathalani viumbe vinavyoishi nchi kavu kama vile binadamu, wanyama( samba,tembo,swala,nyoka n.k) na viumbe vinavyoishi ndani ya maji(samaki,mamba, papa, nyangumi n.k) kwakifupi ukiangalia ulimwengu unaweza kuona imesheeni vitu vingi sana, lakini uzuri wakevitu vyote vina nafasi yake ya kuishi ukiachilia mbali na mwingiliano usiokuwa rasmi.

Ni kibinadamu tu, kutambua kuna watu na wako watu wanahusika na maisha yako katika hali zote kwa maana binadamu anataka awe na watu katika kuendelea shughuli zake, lakini shida inakuja pale utakapoona jambo linalo kugusa wewe wengine aliwagusi wanaona ni lako na wala sio la wote.

Niseme tu kuna wakati unaweza kuona watu wanakuwa na wewe, kuna wakati utakuta watu kama hawako tena nawe, hali hii inakuwa shida sana kwa mtu ambaye ameweka akili zake katika matarajio ya watu, japo kwa ukweli unaweza kuweka akili kwenye matarajio ya Mungu tu lakini bado utaona faraja ya wanadamu inahitajika katika maisha yako kwakua unaishi katika ulimwengu uliobeba watu.
“ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU” hii ni sauti inayo nenwa na moyo wa mtu husika baada ya hali ya fulani katika maisha ya mtu husika inaweza kuwa hali njema au mbaya! Japo kwa kiasi kikubwa inaonekana sana katika hali mbaya.

Niseme tu hali hii hakuna anapenda impate ila inapotokea uwa hakuna namna nyingine ya kuikwepa zaidi ya kuikabili na kusubiri namna itakavyo kuwa kwakua ni wewe na ndilo limekukuta  uwezi kuomba mzigo ulionao umpe mwingineza zaidi ya Mungu ajuaye kesho maana ndio aliye iruhusu iwe.

Nikutie moyo hali hii inawakuta watu wa namna zote walio weka imani yao kwa Mungu kwa asilimia zote na kwa wale wanaotumia hadhina zao katika akili (elimu na maarifa) lakini inafika wakati wana jikuta wako wenyewe, kwa hali halisi katika maisha husika muda mwingi unakuwa katika maongezi yako binafsi ambayo utaki mwingine ahusike.

Katika kipindi hiki unapojiona “ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU” ni kipindi cha kudhihirisha wewe ni nani? Kutoa ile hadhina ambayo Mungu amekupa kuona mkono wake katika namna yake kwakua yeye ndiye ajuaye mwisho kabla ya yote.

Kipindi hiki usipokuwa makini unaweza kuchukua maamuzi yanaweza kuharibu hatima yako au kuifanya iwe bora, wako watu wanapojiona wako pekee yao katika ulimwengu kutokana na hali aliyokuwa nayo uweza kuwaza hata kujiua, kwenda sehemu mbali ambako anahisi nafsi yake itapata pumziko na mwingine kujiingiza katika mtindo mwingine wa maisha ambayo uta hatarisha zaidi maisha yake badala ya kuleta mwanga wa matumaini.

Lakini ni muhimu kutambua hichi kipindi kina muhusu kila mtu kwa muda wake maadam anaishi katika ulimwengu ambao wewe unaishi na hivyo usione kuwa wewe ndio hali hiyo imekukumba kama umeonewa kumbe kila mtu anapopita hapo ila kuvuka hapo inategemea imani yake ameiweka wapi na utayari wa kuingia mazingira mapya.

Usipoteze muda wako katika kutafuta mbaya ni nani? Mpaka ni mekuwa hapa maana kwa kufanya hivyo utakuwa umeliongeza tatizo na sio utatuzi wa tatizo kwa maana utafanya ufahamu wako kulikuza tatizo zaidi na kuzidi kukita mizizi katika moyo wako na mwisho wake unaweza kuibua kisasi kisichokuwa na faida yoyote katika maisha yako.

Hapo lazima utulie na Mungu mwenye dira nzima ya maisha yako maana yeye alikujua tangu ulimwengu ujakuweko!

Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Katika kuzidi kwa Mungu ndio unaleta wepesi wa kutoka hapo ulipo, mbali na hapo utazidi kukaa katika muonekano usio na tija katika maisha yako.

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 20 Desemba 2016

USIKU WA KIPOFU!

USIKU WA KIPOFU


Katika dunia kuna aina mbalimbali za ulemavu mathalani ulemavu wa ngozi, miguu, mikono, macho, masikio na mengine mengi lakini kubwa zaidi la kutambua kuwa imekuwa ni kasumba mbaya pindi mtu anapokuwa mlemavu mbali na ulemavu wa akili basi ulemavu huo unahusianishwa na akili yake kana kwamba kama mtu ni mlemavu wa mikono basi hata akili yake itakuwa nzito kuelewa vitu.
Sipendi kukubaliana kuwa uko uelemavu mbaya zaidi kuliko mwingine ila ninachojua mimi uelemavu wowote ukipata huduma za karibu na uhakika basi wote watajisikia vizuri kwa maana wote wanapata mahitaji yao na maisha yanaendelea.

Ningependa niongelee ulemavu wa kutoona vizuri au kutoona kabisa ( UPOFU) watu wanamna hii kubwa sana wanaoteseka ni hali ya kutoona vitu vinavyoonekana japo wanaweza kugusa na hata kuonja kwa vile vinavyoonjeka, kwa wale wanaonza hali ya upofu kutokana na sababu mbalimbali ajali ikaathri macho yake hama kuvamiwa na kuharibiwa macho na nyingine nyingi uwa upata shida sana kutokana na MAZOEA aliyokuwa nayo lakini baada ya muda uweza kuendana na hali iliyopo kutokana na urahisi wa akili ya mtu husika mbali na hao wako wengine waliokuwa vipofu tangu kuzaliwa kwao kwa maana rahisi mtu huyu ajawai kuona chochote kinacho oneka tangu atoke katika tumbo la mama yake, muda mwingi utumia ngozi katika kutambua hali inayomzunguka kutambua huu ni mchana na huu ni usiku.

Nikubaliane kuwa kila ulemavu unashida zake na pindi hizo shida zisipo patiwa ufumbuzi mtu huyo uona bora afe kuliko kuishi katika mateso yasiyo na kikomo! Yanayo pelekea azidi kudharaulika na kutengwa na kuonekana kuwa yeye sio kitu.

Sifa kubwa kwa kipofu ni hali ya giza inayo mtawala katika fahamu zake na kuishia kutumia milango mingine ya fahamu katika kuendesha maisha yake, kucheka kwake kunatokana baada ya kusikia na sio kuona na hali hii wakati mwingine uweza kuhisi anachekwa yeye kama asipojua watu wanacheka nini?

Kipofu ni mtu anaye hitaji mtu wa karibu sana katika kumwezesha yeye kufanya siku yake iwe njema na maisha yake yaende……….pamoja na hayo pia kipofu uweza kushindwa kumudu mahitaji yake ya msingi kutokana kushindwa kumudu shughuli zake za kiuchumi kutokana na hali aliyonayo, japo wako vipofu wanajimudu katika maisha yao na hata kuendesha maisha ya familia zao.

Kipofu ni rafiki wa giza japo kuwa anaweza jua sasa hapa ni mchana hama usiku lakini katika yote bado anaona giza katika fahamu zake…………………..! anaweza apende au asipende hama hali ya kuvumilia lakini bado ataishi maisha ya giza.
USIKU WA KIPOFU!

Wako watu wanaishi maisha yanayo fanana na maisha ya kipofu! Watu hawa hawaoni jambo maana katika maisha yao kwakua kila kitu kinatafsiri isiyofaa/ isiyojenga katika maisha yake.

Akili zao zimeona ndio maisha yao kwakua hali zao zinadhihirisha kuwa ndivyo walivyo hawana uwezo wakuona nje ya giza linalo wazunguka hata wakisikia wengine wanaona mwanga na kuufurahia kutokana na hali inayomzunguka haoni maana yoyote.

Watu wana mna hii huishi maisha ya giza pasipo kupenda bali inaweza kujitokeza hali ya kuridhika kuwa haya ndio maisha wacha niishi!

Lazima utambue kuwa kipofu katika hali ya dhati angepewa nafasi angeweza kusema kuonyesha kile akipendacho afanyiwe basi bila shaka angesema anataka kuona! Lakini wako watu akili zao hazina mtazamo wa kuona mwanga katika maisha yao bali uona giza( maisha ya kupapasapapasa) ndivyo wanavyoona wanapaswa kuishi hivyo.

Marko 10:51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.

Laiti ungefungua ufahamu wa kipofu uone nini kinacho msukuma na namna ya kiu yake ilivyo kwa kutaka kuona usingeweza kuamini hile shauku aliyo nayo! Lakini wako watu ambao katika akili zisizo kuwa na shauku ya kuona mwanga na kuufurahia na kuona inawezekana kuona mwanga kwakua unayosifa ya kuona.

Wako watu wengi wamekuwa na maisha ya namna ya kuyapenda wao wenyewe pasipo kujua hiyo ndio sawa yangu hama sio yangu kwa kukosa uelewa ulio sahihi ujikuta mtu kuona hali aliyonayo ndio sawa yake.

Usijizuie macho kuona hatua nyingine na kuona ni haki yako kuona yote kwakua Mungu amekupa nafasi ya kuona na sio kwa ajili ya wengine bali wewe ni mmoja wao kati ya watu hao.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:


Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 13 Desemba 2016

ACHA NIANZE, ITANIFUATA!

ACHA NIANZE, ITANIFUATA!


Imekuwa kikwazo kwa watu wengi katika kushindwa kuanza kitu hama safari, hata jambo fulani lenye maana/tija katika maisha yake, inawezekana wengine watasema maandalizi bado au hayaja jitosheleza na wengine watatumia maneno yanayosemekana kuwa yenye hekima…kuwa wakati bado!

Imekuwa ni jambo la hekima na kuonekana kama mtu mwenye busara pindi unapotaka kuanza safari ukaanza kupanga mambo ya muhimu ya kuzingatia katika safari yako ili uweze kufanikiwa katika yale unayo yakusudia au yale unayoyaendea, na katika ulimwengu wa sasa imekuwa fezea sana pindi utakapo anza safari alafu uka kwama katikati, moja ya sababu kubwa watu watakayokuambia kuwa ukujiandaa vizuri, kwa lugha nyepesi watasema umekulupuka!

Ni kubaliane kuwa katika safari nyingi ambazo watu uweza kusafiri kwa maana ya maisha na hatua zake hama safari za kawaida tu! Uwa maandalizi yake yanatakiwa kuwa kwa 100% (asilimia mia), naam hata ukijiamini vipi uwezi kuikabili kesho kiufasaha haijarishi una hela, elimu, marafiki hama ndugu wa kukusaidia kwa kila hitaji lako litakalo jitokeza……..kwakua ni yeye mwenye kuijua kesho ndio mwenye majibu ya kesho.

Sikatai jambo ili ulifanye kiufasaha lazima liwe ndani ya wakati lakini imekuwa ni changamoto katika kuujua wakati wa kila jambo na wakati mwingi mpaka matokeo yatokee ndio tujue kuwa hivi kumbe nilipaswa kufanya haya na sikupaswa kufanya yale…….wakati unakua muda umeshapita! Sijui utamlaumu nani? Hiyo ni siri yako iliyo ndani ya moyo wako!

Ukiwa mfatiliaji mzuri wa wengi waliofanikiwa awakusubiri kila kitu kiwe vizuri ndipo waanze shughuli zao, wengi walianza na mwanzo ambao pale walipo sasa apakuwa na uwezekano wa kumtabiria kuwa leo atakua hapa hama atakuwa na miliki hizo, kwani wako watu walioanza na kuuza maji sasa hivi wana miliki makapuni makubwa na biashara zao zimevuka hata nje ya mipaka ya nchi pia wako walikuwa makonda wa daladala leo wamekuwa waandishi wa habari maalufu katika dunia ya sasa (BBC Swahili) jina naliweka kapuni ila ni kweli na mtu huyo yupo.

Ni vizuri kukuta mazingira ya metengenezwa kwa ajili yako lakini sio mara zote unaweza kukuta mazingira ya namna hiyo hasa katika dunia ya sasa, ili upenye na kufika mbali unahitaji kuonyesha utofauti wako, watu waone kuna umuhimu wa kutokana kwa huyu na kwenda kwa yule!

Lakini imekuwa ni tofauti sana katika dunia ya leo watu wamekuwa wakisubiri fursa ziwafuate na pindi zisipo wafuata wanaona kuwa wakati bado hivyo uendelea kusubiri mpaka mtu anazeeka na kufanya lisilo mpasa na hatimaye kuwa vile asivyotakiwa kuwa.

Tambua macho yako yanapoona kitu kwa namna ya tofauti na kuzalisha deni katika moyo wako hilo silo jambo la kupuuzia wala lakusubiri utiwe moyo ili uanze, bali anza kuliandalia mazingira ya kitu kipya kizaliwe ndani yako haijarishi kwamba hakina mfanano na wengi hama kitachukua muda mrefu katika kutambulika na kukubalika. Ni muhimu kutambua kila kitu kina ngazi yake la muhimu wewe ni kufanya mpaka pale kusudi lako litakapo isha na wengine wataendelea hapo usipende kufanya kila kitu hata kama unapenda kufanya hivyo!

1 Mambo ya Nyakati 28:6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye.

2 Mambo ya Nyakati 6:9 lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako, yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu.

Mfalme daudi alikuwa anatamani sana kumjengea bwana hekalu kwakua ndio ilikuwa shauku yake kwa vile anavyompenda Mungu lakini hilo ilikuwa nje ya kusudi la Mungu alilokusudia na pindi Mungu alipokataa mfalme Daudi alikubaliana nayo!

Niseme vitu vingi tunavyotumia vimepita katika hatua mbalimbali mpaka kuwa katika muonekano uliopo sasa mathalani computer, mavazi, ndege na hata taa muonekano wa sasa sio ule wa awali na kila hatua inaweza kuwa ili muhusisha mtu mwingine lakini mwisho ika faida katika jamii husika.
Kila kitu kidogo au kikubwa fanya katika ufanisi wote wala usitami tu kufika tu anza na padogo utafika pa kubwa kwakua kusudi litakusukuma ufike mbali sana!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:


Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 6 Desemba 2016

HAKUNA MAANA YA NURU KAMA HAKUNA GIZA!



HAKUNA MAANA YA NURU KAMA HAKUNA GIZA


Ni kweli taa unaweza kuiwasha wakati wowote, ila inakuwa na maana sana pale inapoiwasha  wakati wake ( wakati inahitajika) yaani  usiku, kwani usiku uhitaji wake unakuwa ni wa lazima sana ukitofautisha na mahitaji ya nuru wakati mwanga hupo (mchana)! 

Utakuwa wa kawaida, pale ambapo utahitaji nuru mchana ila utakuwa wakushangaza kidogo usiku ukihitaji giza.

Na uwa atuhitaji sana maji ya kunywa kama hatuna kiu! Japo kwa afya unahitajika unywe maji ya kutosha kwa siku ingawa inategemea na uhitaji wa mwili wako.

Katika dunia ya sasa umaana wa kitu utegemea sana na uhitaji wa hicho kitu, kwa maana rahisi niseme tu hata kama kitu kikiwa na uzuri gani kama hakuna uhitaji wa hicho kitu basi hakuna maana wa hicho kitu….kwakua sababu ya kuwepo haipo.

Maana ya mwalimu inakuja pale panapo kuwa na wanafunzi na hasa akiwa anafundisha!
Maana ya daktari inakamilika sio baada ya kusomea tu bali hasa pale anapokuwa na wagonjwa akiwahudumia vizuri!

Maana ya mama inakamilika pale anapokuwa na watoto na hasa akiwa anawalea!
Na maana ya mume uwa inakamilika pale anapokuwepo mke!

Na maana ya baba inakamilika anapokuwepo mama na hasa yule baba anaye tambua majukumu yake
Haijarishi unapenda mwanga kiasi gani lazima utambue kuwa kuna usiku utakuja ili ukamilishe siku na majira yaendelee kutokea.

Ni muhimu kutambua kuwa fahari ya nuru ipo pale palipo na giza, na giza linapokuwepo ndipo hapo unaweza kuona kuwa hali ingekuwaje  bila nuru kuwepo.

Hivyo katika maisha hauhitaji uwe muoga sana katika kudhihirisha nuru yako katika giza linapokukabili maana linapokuja ndipo nuru uonyesha ubora na uweza wake. 

Katika yote hakikisha unahakikisha kuwa nuru iliyo ndani yako inakuwa na nguvu siku zote ili giza lisiwe na nguvu sana kwako likazalisha mateso ndani ya maisha.

Unahitaji kutambua tu kuwa nuru iliyo ndani yako inaweza kukuangazia sahemu zote na ukawa salama, kwakua kazi ya nuru ni kukuangazia usalama na matumaini yasiyo koma.

Bila kuwa na nuru ndani yako ukweli utawalaumu sana watu kuwa hawakuoni katika giza lako kumbe wewe binafsi unahitaji hiyo nuru kwanza na mengine yatafuata kutokana na nuru inayo ng’aa toka ndani yako maana yenyewe inajitosheleza.

Napindi unapokuwa na nuru uhitaji kuliogopa giza bali giza litaiogopa hiyo nuru iliyo ndani yako na hata ikitokea giza limekuvaa ile nuru itaonyesha nguvu zake na ndipo hapo utaona ushindi wa Mungu kwakua yeye ni nuru.

Ahuhitaji mambo mengi ili ung’ae ila unahitaji NURU ili ung’ae!

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………0764 018535