USIKU WA KIPOFU
Katika dunia kuna aina mbalimbali za ulemavu mathalani
ulemavu wa ngozi, miguu, mikono, macho, masikio na mengine mengi lakini kubwa
zaidi la kutambua kuwa imekuwa ni kasumba mbaya pindi mtu anapokuwa mlemavu
mbali na ulemavu wa akili basi ulemavu huo unahusianishwa na akili yake kana
kwamba kama mtu ni mlemavu wa mikono basi hata akili yake itakuwa nzito kuelewa
vitu.
Sipendi kukubaliana kuwa uko uelemavu mbaya zaidi kuliko
mwingine ila ninachojua mimi uelemavu wowote ukipata huduma za karibu na
uhakika basi wote watajisikia vizuri kwa maana wote wanapata mahitaji yao na
maisha yanaendelea.
Ningependa niongelee ulemavu wa kutoona vizuri au kutoona
kabisa ( UPOFU) watu wanamna hii kubwa sana wanaoteseka ni hali ya kutoona vitu
vinavyoonekana japo wanaweza kugusa na hata kuonja kwa vile vinavyoonjeka, kwa
wale wanaonza hali ya upofu kutokana na sababu mbalimbali ajali ikaathri macho
yake hama kuvamiwa na kuharibiwa macho na nyingine nyingi uwa upata shida sana
kutokana na MAZOEA aliyokuwa nayo lakini baada ya muda uweza kuendana na hali
iliyopo kutokana na urahisi wa akili ya mtu husika mbali na hao wako wengine waliokuwa
vipofu tangu kuzaliwa kwao kwa maana rahisi mtu huyu ajawai kuona chochote
kinacho oneka tangu atoke katika tumbo la mama yake, muda mwingi utumia ngozi
katika kutambua hali inayomzunguka kutambua huu ni mchana na huu ni usiku.
Nikubaliane kuwa kila ulemavu unashida zake na pindi hizo
shida zisipo patiwa ufumbuzi mtu huyo uona bora afe kuliko kuishi katika mateso
yasiyo na kikomo! Yanayo pelekea azidi kudharaulika na kutengwa na kuonekana
kuwa yeye sio kitu.
Sifa kubwa kwa kipofu ni hali ya giza inayo mtawala katika
fahamu zake na kuishia kutumia milango mingine ya fahamu katika kuendesha
maisha yake, kucheka kwake kunatokana baada ya kusikia na sio kuona na hali hii
wakati mwingine uweza kuhisi anachekwa yeye kama asipojua watu wanacheka nini?
Kipofu ni mtu anaye hitaji mtu wa karibu sana katika
kumwezesha yeye kufanya siku yake iwe njema na maisha yake yaende……….pamoja na
hayo pia kipofu uweza kushindwa kumudu mahitaji yake ya msingi kutokana
kushindwa kumudu shughuli zake za kiuchumi kutokana na hali aliyonayo, japo
wako vipofu wanajimudu katika maisha yao na hata kuendesha maisha ya familia
zao.
Kipofu ni rafiki wa giza japo kuwa anaweza jua sasa hapa ni
mchana hama usiku lakini katika yote bado anaona giza katika fahamu
zake…………………..! anaweza apende au asipende hama hali ya kuvumilia lakini bado
ataishi maisha ya giza.
USIKU WA KIPOFU!
Wako watu wanaishi maisha yanayo fanana na maisha ya kipofu!
Watu hawa hawaoni jambo maana katika maisha yao kwakua kila kitu kinatafsiri
isiyofaa/ isiyojenga katika maisha yake.
Akili zao zimeona ndio maisha yao kwakua hali zao
zinadhihirisha kuwa ndivyo walivyo hawana uwezo wakuona nje ya giza linalo
wazunguka hata wakisikia wengine wanaona mwanga na kuufurahia kutokana na hali
inayomzunguka haoni maana yoyote.
Watu wana mna hii huishi maisha ya giza pasipo kupenda bali
inaweza kujitokeza hali ya kuridhika kuwa haya ndio maisha wacha niishi!
Lazima utambue kuwa kipofu katika hali ya dhati angepewa
nafasi angeweza kusema kuonyesha kile akipendacho afanyiwe basi bila shaka
angesema anataka kuona! Lakini wako watu akili zao hazina mtazamo wa kuona
mwanga katika maisha yao bali uona giza( maisha ya kupapasapapasa) ndivyo wanavyoona
wanapaswa kuishi hivyo.
Marko 10:51 Yesu
akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu
wangu, nataka nipate kuona.
Laiti ungefungua ufahamu wa kipofu uone nini kinacho msukuma
na namna ya kiu yake ilivyo kwa kutaka kuona usingeweza kuamini hile shauku
aliyo nayo! Lakini wako watu ambao katika akili zisizo kuwa na shauku ya kuona
mwanga na kuufurahia na kuona inawezekana kuona mwanga kwakua unayosifa ya
kuona.
Wako watu wengi wamekuwa na maisha ya namna ya kuyapenda wao
wenyewe pasipo kujua hiyo ndio sawa yangu hama sio yangu kwa kukosa uelewa ulio
sahihi ujikuta mtu kuona hali aliyonayo ndio sawa yake.
Usijizuie macho kuona hatua nyingine na kuona ni haki yako
kuona yote kwakua Mungu amekupa nafasi ya kuona na sio kwa ajili ya wengine
bali wewe ni mmoja wao kati ya watu hao.
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni