ACHA NIANZE, ITANIFUATA!
Imekuwa kikwazo kwa watu wengi katika kushindwa kuanza kitu
hama safari, hata jambo fulani lenye maana/tija katika maisha yake, inawezekana
wengine watasema maandalizi bado au hayaja jitosheleza na wengine watatumia
maneno yanayosemekana kuwa yenye hekima…kuwa wakati bado!
Imekuwa ni jambo la hekima na kuonekana kama mtu mwenye
busara pindi unapotaka kuanza safari ukaanza kupanga mambo ya muhimu ya
kuzingatia katika safari yako ili uweze kufanikiwa katika yale unayo yakusudia
au yale unayoyaendea, na katika ulimwengu wa sasa imekuwa fezea sana pindi
utakapo anza safari alafu uka kwama katikati, moja ya sababu kubwa watu
watakayokuambia kuwa ukujiandaa vizuri, kwa lugha nyepesi watasema umekulupuka!
Ni kubaliane kuwa katika safari nyingi ambazo watu uweza
kusafiri kwa maana ya maisha na hatua zake hama safari za kawaida tu! Uwa
maandalizi yake yanatakiwa kuwa kwa 100% (asilimia mia), naam hata ukijiamini
vipi uwezi kuikabili kesho kiufasaha haijarishi una hela, elimu, marafiki hama
ndugu wa kukusaidia kwa kila hitaji lako litakalo jitokeza……..kwakua ni yeye
mwenye kuijua kesho ndio mwenye majibu ya kesho.
Sikatai jambo ili ulifanye kiufasaha lazima liwe ndani ya
wakati lakini imekuwa ni changamoto katika kuujua wakati wa kila jambo na
wakati mwingi mpaka matokeo yatokee ndio tujue kuwa hivi kumbe nilipaswa kufanya
haya na sikupaswa kufanya yale…….wakati unakua muda umeshapita! Sijui utamlaumu
nani? Hiyo ni siri yako iliyo ndani ya moyo wako!
Ukiwa mfatiliaji mzuri wa wengi waliofanikiwa awakusubiri
kila kitu kiwe vizuri ndipo waanze shughuli zao, wengi walianza na mwanzo ambao
pale walipo sasa apakuwa na uwezekano wa kumtabiria kuwa leo atakua hapa hama
atakuwa na miliki hizo, kwani wako watu walioanza na kuuza maji sasa hivi wana
miliki makapuni makubwa na biashara zao zimevuka hata nje ya mipaka ya nchi pia
wako walikuwa makonda wa daladala leo wamekuwa waandishi wa habari maalufu
katika dunia ya sasa (BBC Swahili) jina naliweka kapuni ila ni kweli na mtu
huyo yupo.
Ni vizuri kukuta mazingira ya metengenezwa kwa ajili yako
lakini sio mara zote unaweza kukuta mazingira ya namna hiyo hasa katika dunia
ya sasa, ili upenye na kufika mbali unahitaji kuonyesha utofauti wako, watu
waone kuna umuhimu wa kutokana kwa huyu na kwenda kwa yule!
Lakini imekuwa ni tofauti sana katika dunia ya leo watu
wamekuwa wakisubiri fursa ziwafuate na pindi zisipo wafuata wanaona kuwa wakati
bado hivyo uendelea kusubiri mpaka mtu anazeeka na kufanya lisilo mpasa na
hatimaye kuwa vile asivyotakiwa kuwa.
Tambua macho yako yanapoona kitu kwa namna ya tofauti na kuzalisha
deni katika moyo wako hilo silo jambo la kupuuzia wala lakusubiri utiwe moyo
ili uanze, bali anza kuliandalia mazingira ya kitu kipya kizaliwe ndani yako
haijarishi kwamba hakina mfanano na wengi hama kitachukua muda mrefu katika
kutambulika na kukubalika. Ni muhimu kutambua kila kitu kina ngazi yake la
muhimu wewe ni kufanya mpaka pale kusudi lako litakapo isha na wengine
wataendelea hapo usipende kufanya kila kitu hata kama unapenda kufanya hivyo!
1 Mambo ya Nyakati 28:6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa
nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye.
2 Mambo ya Nyakati 6:9 lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo;
ila mwanao atakayetoka katika viuno vyako,
yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu.
Mfalme
daudi alikuwa anatamani sana kumjengea bwana hekalu kwakua ndio ilikuwa shauku
yake kwa vile anavyompenda Mungu lakini hilo ilikuwa nje ya kusudi la Mungu
alilokusudia na pindi Mungu alipokataa mfalme Daudi alikubaliana nayo!
Niseme
vitu vingi tunavyotumia vimepita katika hatua mbalimbali mpaka kuwa katika
muonekano uliopo sasa mathalani computer, mavazi, ndege na hata taa muonekano
wa sasa sio ule wa awali na kila hatua inaweza kuwa ili muhusisha mtu mwingine
lakini mwisho ika faida katika jamii husika.
Kila
kitu kidogo au kikubwa fanya katika ufanisi wote wala usitami tu kufika tu anza
na padogo utafika pa kubwa kwakua kusudi litakusukuma ufike mbali sana!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson……………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni