HAKUNA MAANA YA NURU KAMA HAKUNA GIZA
Ni kweli taa unaweza kuiwasha wakati wowote, ila inakuwa na maana sana pale inapoiwasha wakati wake ( wakati inahitajika) yaani usiku, kwani usiku uhitaji wake unakuwa ni wa lazima sana ukitofautisha na mahitaji ya nuru wakati mwanga hupo (mchana)!
Utakuwa wa kawaida, pale ambapo utahitaji nuru mchana ila utakuwa wakushangaza kidogo usiku ukihitaji giza.
Na uwa atuhitaji sana maji ya kunywa kama hatuna kiu! Japo kwa afya unahitajika unywe maji ya kutosha kwa siku ingawa inategemea na uhitaji wa mwili wako.
Katika dunia ya sasa umaana wa kitu utegemea sana na uhitaji wa hicho kitu, kwa maana rahisi niseme tu hata kama kitu kikiwa na uzuri gani kama hakuna uhitaji wa hicho kitu basi hakuna maana wa hicho kitu….kwakua sababu ya kuwepo haipo.
Maana ya mwalimu inakuja pale panapo kuwa na wanafunzi na hasa akiwa anafundisha!
Maana ya daktari inakamilika sio baada ya kusomea tu bali hasa pale anapokuwa na wagonjwa akiwahudumia vizuri!
Maana ya mama inakamilika pale anapokuwa na watoto na hasa akiwa anawalea!
Na maana ya mume uwa inakamilika pale anapokuwepo mke!
Na maana ya baba inakamilika anapokuwepo mama na hasa yule baba anaye tambua majukumu yake
Haijarishi unapenda mwanga kiasi gani lazima utambue kuwa kuna usiku utakuja ili ukamilishe siku na majira yaendelee kutokea.
Ni muhimu kutambua kuwa fahari ya nuru ipo pale palipo na giza, na giza linapokuwepo ndipo hapo unaweza kuona kuwa hali ingekuwaje bila nuru kuwepo.
Hivyo katika maisha hauhitaji uwe muoga sana katika kudhihirisha nuru yako katika giza linapokukabili maana linapokuja ndipo nuru uonyesha ubora na uweza wake.
Katika yote hakikisha unahakikisha kuwa nuru iliyo ndani yako inakuwa na nguvu siku zote ili giza lisiwe na nguvu sana kwako likazalisha mateso ndani ya maisha.
Unahitaji kutambua tu kuwa nuru iliyo ndani yako inaweza kukuangazia sahemu zote na ukawa salama, kwakua kazi ya nuru ni kukuangazia usalama na matumaini yasiyo koma.
Bila kuwa na nuru ndani yako ukweli utawalaumu sana watu kuwa hawakuoni katika giza lako kumbe wewe binafsi unahitaji hiyo nuru kwanza na mengine yatafuata kutokana na nuru inayo ng’aa toka ndani yako maana yenyewe inajitosheleza.
Napindi unapokuwa na nuru uhitaji kuliogopa giza bali giza litaiogopa hiyo nuru iliyo ndani yako na hata ikitokea giza limekuvaa ile nuru itaonyesha nguvu zake na ndipo hapo utaona ushindi wa Mungu kwakua yeye ni nuru.
Ahuhitaji mambo mengi ili ung’ae ila unahitaji NURU ili ung’ae!
ANAITWA MUNGU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni