Jumanne, 27 Desemba 2016

MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU!

MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU!


Kama bahari inavyo hifadhi vitu vingi na hata kufanya viumbe viishi na kuimarisha mzunguko wao pamoja, kwakua ndani ya ulimwengu viko vitu mathalani viumbe vinavyoishi nchi kavu kama vile binadamu, wanyama( samba,tembo,swala,nyoka n.k) na viumbe vinavyoishi ndani ya maji(samaki,mamba, papa, nyangumi n.k) kwakifupi ukiangalia ulimwengu unaweza kuona imesheeni vitu vingi sana, lakini uzuri wakevitu vyote vina nafasi yake ya kuishi ukiachilia mbali na mwingiliano usiokuwa rasmi.

Ni kibinadamu tu, kutambua kuna watu na wako watu wanahusika na maisha yako katika hali zote kwa maana binadamu anataka awe na watu katika kuendelea shughuli zake, lakini shida inakuja pale utakapoona jambo linalo kugusa wewe wengine aliwagusi wanaona ni lako na wala sio la wote.

Niseme tu kuna wakati unaweza kuona watu wanakuwa na wewe, kuna wakati utakuta watu kama hawako tena nawe, hali hii inakuwa shida sana kwa mtu ambaye ameweka akili zake katika matarajio ya watu, japo kwa ukweli unaweza kuweka akili kwenye matarajio ya Mungu tu lakini bado utaona faraja ya wanadamu inahitajika katika maisha yako kwakua unaishi katika ulimwengu uliobeba watu.
“ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU” hii ni sauti inayo nenwa na moyo wa mtu husika baada ya hali ya fulani katika maisha ya mtu husika inaweza kuwa hali njema au mbaya! Japo kwa kiasi kikubwa inaonekana sana katika hali mbaya.

Niseme tu hali hii hakuna anapenda impate ila inapotokea uwa hakuna namna nyingine ya kuikwepa zaidi ya kuikabili na kusubiri namna itakavyo kuwa kwakua ni wewe na ndilo limekukuta  uwezi kuomba mzigo ulionao umpe mwingineza zaidi ya Mungu ajuaye kesho maana ndio aliye iruhusu iwe.

Nikutie moyo hali hii inawakuta watu wa namna zote walio weka imani yao kwa Mungu kwa asilimia zote na kwa wale wanaotumia hadhina zao katika akili (elimu na maarifa) lakini inafika wakati wana jikuta wako wenyewe, kwa hali halisi katika maisha husika muda mwingi unakuwa katika maongezi yako binafsi ambayo utaki mwingine ahusike.

Katika kipindi hiki unapojiona “ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU” ni kipindi cha kudhihirisha wewe ni nani? Kutoa ile hadhina ambayo Mungu amekupa kuona mkono wake katika namna yake kwakua yeye ndiye ajuaye mwisho kabla ya yote.

Kipindi hiki usipokuwa makini unaweza kuchukua maamuzi yanaweza kuharibu hatima yako au kuifanya iwe bora, wako watu wanapojiona wako pekee yao katika ulimwengu kutokana na hali aliyokuwa nayo uweza kuwaza hata kujiua, kwenda sehemu mbali ambako anahisi nafsi yake itapata pumziko na mwingine kujiingiza katika mtindo mwingine wa maisha ambayo uta hatarisha zaidi maisha yake badala ya kuleta mwanga wa matumaini.

Lakini ni muhimu kutambua hichi kipindi kina muhusu kila mtu kwa muda wake maadam anaishi katika ulimwengu ambao wewe unaishi na hivyo usione kuwa wewe ndio hali hiyo imekukumba kama umeonewa kumbe kila mtu anapopita hapo ila kuvuka hapo inategemea imani yake ameiweka wapi na utayari wa kuingia mazingira mapya.

Usipoteze muda wako katika kutafuta mbaya ni nani? Mpaka ni mekuwa hapa maana kwa kufanya hivyo utakuwa umeliongeza tatizo na sio utatuzi wa tatizo kwa maana utafanya ufahamu wako kulikuza tatizo zaidi na kuzidi kukita mizizi katika moyo wako na mwisho wake unaweza kuibua kisasi kisichokuwa na faida yoyote katika maisha yako.

Hapo lazima utulie na Mungu mwenye dira nzima ya maisha yako maana yeye alikujua tangu ulimwengu ujakuweko!

Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Katika kuzidi kwa Mungu ndio unaleta wepesi wa kutoka hapo ulipo, mbali na hapo utazidi kukaa katika muonekano usio na tija katika maisha yako.

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni