TAFSIRI YA JICHO
Niseme kuna tofauti ya kuwa na macho na kuwa macho yenye
tafsiri sahihi!
Japo kila jicho linapoangalia kitu uwa linakuwa na tafsiri
ila sio kila jicho linaloweza beba tafsiri sahihi.
Moja ya fahari ya mwanadamu ni MACHO! Kwakua kupitia macho
uwezesha vionjo vya mwili kufanya kazi kwa wepesi na kwa hali stahiki, kwa
maana baadhi ya watu kwakukosa kuona uweza kupelekea baadhi ya hali kushindwa
kufanya kazi inavyotakiwa mathalani kucheka, kutabasamu,kuhuzunika na hata hali
kufikiri kwa wepesi uweza kupungua.
Naamini katika JICHO kuna makundi makuu mawili kundi linalo
ona alafu likwenda mbele na kundi linarudi nyuma, yote haya ni makundi yanafanya kazi kutegemea na mtu
husika…….kwakua kila jambo linapotokea ushindi au kushindwa utegemea NAMNA UNAVYOONA!
Tafsiri sahihi ya jicho
ukupa:
i.kuwa na bidii kwa kile unachokifanya,kwakua wewe pekee
unakiona
ii.kuwa na imani thabiti isiyo yumbishwa
iii.kuwa na amani katika hali zote
-utofauti wako na watu wengine unao onekana ni sawa kwa kuwa
mnaona tofauti hivyo maamuzi hayawezi kufanana.
Tukubaliane tu kuwa maamuzi mengi yanafanywa baada ya JICHO
KUKUPA TAFSIRI kwani kupitia kuona unaweza kuona kuwa hili jambo lina nihitaji
mimi peke yangu au watu zaidi ili liweze kutendeka na wengine wengi jambo
linapokuwa gumu sana kuzidi kimo cha akili yake hapo uona haja ya kuwa na Mungu
kuhusika kwa watu wote wameshindwa.
Niseme unapokosa tafsiri sahihi ya macho hapo inakuwa ni
rahisi kuona upendeleo baadhi ya watu na kuona wewe unanyimwa haki kwa tafsiri
rahisi wanakuzibia riziki yako au hawataki maendeleo yako na mwisho kuona
wanakukomoa, nawe hapo utajipanga kupambambana ili uwakomoe na sio kutoka hapo,
Tatizo kubwa kwa watu wengi pindi tunapoona mtu anainuka
katika hatua fulani katika maisha yake kwa kuona tafsiri sahihi ya jambo fulani
au hali fulani katika maisha yake, tuna anza kumpa siku kama atadumu katika
maisha yake baada ya ya wewe kutafuta siri nawe uchomoke katika hali uliyoko.
Niseme kwa dhati ukubwa wa tatizo na udogo utegemea TAFSIRI
YA JICHO, wote mnaweza kupata shida moja lakini matokeo yakawa tofauti kutokana
na tafsiri binafsi uliolipa hilo jambo ukiona litakutesa maisha mwako nalo
litachukua nafasi katika maisha yako na kuhakikisha jambo hilo linakuwa sawa na
vile ulivyo liamini.
Na niseme tu, katika kitu kigumu sana katika maisha ya mtu ni
kubadilisha tafsiri inayotolewa na macho yake, maana bila hapo unaweza ukafanya
yote kama macho hayaja badili tafsiri yake mabadiliko kuyaona hapo ina kuwa ngumu
ni kama kuona chozi la samaki akiwa majini.
Na inawezekana tatizo likachukua siku moja , wiki moja,
mwezi, mwaka hama miaka ishirini, ambalo limeshawai kukutokea katika maisha
yako yote utegemea na tafsiri ambayo jicho lako litatoa kutokana na hali
inayokuzunguka mathalani.kufukuzwa kazi, kuachwa hama kutengwa na mambo mengine
mengi
Niseme unapokuwa na jicho lililobeba tafsiri unaweza kuona
vitu tofauti na wengine wanavyoona maana unaweza kuona maisha mengine pindi
unapoona jalala la uchafu wewe ukaona maisha ya utele na ustawi wa mambo mengi.
Na msimamo unao zalishwa baada ya kuona/ kupata tafsiri
sahihi ya jicho kamwe hauwezi kuyumbishwa kwani unaweza kuona mwisho kabla ya
mwanzo kuanza unajua kupitia hapa na utafika wapi! Hivyo utajali kule unako
kwenda kuliko vile wanavyosema,
Kukosa tafsiri sahihi ya macho unaweza kuishi maisha ambayo
kiukweli hakupaswa kuishi hivyo unaweza kujikuta unaishi maisha ya kujikunyata
hata kama hakuna baridi, hata mtu akikushauri bado unaweza usimwamini kwakua
wewe ndivyo unavyoona na sio vile unavyotakiwa kuona.
Uwezi kupata tafsiri sahihi ya kuona kama tu kama ujampa
nafasi ya kutosha yeye aliyekupa macho uwe
nayo naam yeye ndio anajua matumizi sahihi hayo macho,
Niseme unapoona watu mbali waliomwamini Mungu wakitumia
vizuri tafsiri ya macho yao na hata kufanikiwa katika maisha yao hayo yote ni
matokeo ya wana wa Mungu kutotumia nafasi zao, kwa hiyo wamechukua nafasi zote
katika upande huo nasi tumebaki kwenda kanisani tu,
Na Mungu amewaachie watu wengine mbali na watoto wake katika
matumizi sahihi ya tafsiri ya macho yao ili kuonyesha kuwa tunatakiwa tuishi
vipi ilikuweza kuitawala dunia katika misingi yake, kwani hakuna mzazi ambaye
anaweza kuruhu mwanae anayempenda kuteseka wakati uwezo wa kufanya aishi maisha
ya utele na furaha anao uwezo.
Kama kunavitu unahitaji upambane navyo sana ni hali ya
kuapata tafsiri sahihi ya jicho katika mambo
yanayokuzunguka,yanayokutokea,yanayokunyimaraha,yanayofanya usiwe na amani,
kwani tafsiri sahihi ya macho upelekea kuamua mazuri yaliyo jaa hekima na yenye
ubora yanayo kutengenezea kesho yenye matumaini bora yasiyo kwamishwa na mtu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………..0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni