KUJUA KWA FAIDA
Katika dunia ya sasa ni nadra sana
umuulize mtu jambo alafu akakujibu AJUI labda jambo hilo ameona alina faida
kwake lakini mbali na hapo lazima na yeye aonyeshe kuwa anajua na sio kujua tu!
Bali kujua vizuri sana kana kwamba alitabiri hicho kitu/ jambo kabla alijatokea
hata kama anajua nukta moja ya picha nzima bado atataka kuonyesha anajua vizuri
akionyesha kuwa yuko “updated” issue mbalimbali kwake ndio kisima………ukimtazama
sana mtu huyu utakuta anapenda sana sifa alafu mbaya zaidi ajui kiunaga ubaga.
Katika sayari ya sasa watu wengi
upenda kujua vitu vingi na hasa vipya hama vinavyoonekana kuwa watu wengi
wanahitaji kuvijua ili na yeye aonekane kuwa ni wa kisasa na mwisho naye
apatesifa kuwa katika watu naye yupo na kwa bahati mbaya ukimwangalia mtu huyu
ukimweka katika maisha yake unaweza usione tofauti yake na mtu asiyejua kabisa,
Nipende kusema kwamba ni kweli KUJUA
ndio ukumbozi wa kwanza katika maisha ya mwanadamu kwakua katika kujua uweza
kupelekea kuamua/ utendaji uweze kuwa wa maana na wenye tija katika maisha ya
mtu,
Napenda kusema KUJUA kunakuwa na
maana:
i.mazingira ya utendaji kazi kwa yale unajua
ii.hali ya kuchukua hatua
iii.wakati sahihi
haya ni mambo machache ambayo
yanaweza kuleta tija ya wewe kujua na kuwa faida kwako na wengine wanao
kuzunguka hivyo kicheko chako kinakuwa kicheko cha wote.
Msukumo wa kutaka kujua kitu nacho
kitu muhimu sana katika kukupa matumizi sahihi wa kile utakachokijua
a)unaweza kutamani kujua kitu kwa
ajili ya kuongeza/kuimarisha maisha yako na hatimaye kukupa hatua moja katika
kufikia hatua bora ya maisha yako.
b)maumivu/hasira/uchungu hali hizi
zikikupelekea kujua kitu hakika kujua huku hakuta kuwa na maana sana kwako na
hata kwa wengine kwaku katika hali hii hapo kiburi na kisasi ni sehemu yake
c)kutaka na wewe utambulike
kanisani/mtaani/jamii ni kweli watu watajua unajua lakini hawatafaidika na hayo
unayo yajua kwakua utafanya kwa masharti yasio na utu ndani bali yanayo
kutambulisha wewe pasipo faida yoyote.
Isaya 66:2 Maana mkono wangu ndio uliofanya
hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu
ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Tambua Mungu ili ahusike na maisha
yako atufuti mtu mwenye kujua tu! Japo kujua ni vizuri lakini sifa kubwa ambayo
Mungu utamani kuiona kwa mtu:
i.mtu aliye mnyonge
ii.mwenye roho iliyopondeka
iii.atetemekaye asikiapo neno lake
jua ujuavyo pasipo kuwa na msingi
huu kujua kwako hakuta kuwa na maana kwa Mungu sana kwakua unaweza fanyika
daraja kwa wengine lakini wewe usiwe na faida kwa hayo.
Umuhimu wako katika kujua kwako
hutumie kwa wakati sahihi, penye kusikiliza basi sikiliza, penye kuongea basi
ongea na penye kujifunza basi ni vizuri.
Dhahabu haina haja ya
kujitengeneza ili ionekane ina thamani uwa ikionekana basi watu huitaka kuwa
nayo, kwakua wanajua wanapokuwa nayo nini kinatokea katika maisha,
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa
na:
Cothey Nelson………………………………………………….0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni