Jumanne, 31 Januari 2017

SIKU YANGU!



SIKU YANGU


Kama kuna kitu ambacho thamani yake haiwezi kupimwa ili uipate hama kisichoangalia uwezo wa mtu kuwa huyu anavyo vingi na huyu ana kidogo hama kwa maana pawepo na kitu kishawishi uweze kuipata ukweli HAKUNA, hicho kitu kinaitwa SIKU

 Inapotokea watu kumi  wakapewa zawadi zinazo fanana, kama imeamliwa kutolewa gari kwa kila mmoja basi  watapewa gari zinazofanana, lakini kila mmoja baada ya kupewa gari basi atashukuru kwa nafsi yake ( kwakua yeye atakuwa ndio mmiliki) na sio kwa ujumla kwakua kila mtu kapewa  na ana namna yake ya kushukuru,

Ni tabia nzuri ya kushukuru pindi unapoona nawe umepata zawadi miongoni mwa wengi kwakua ni jambo jema kukumbukwa au kutambulika na wala usiwe na kinyongo kuwa wewe kutaka kupewa zaidi ya wengine, ni bora kupata hata kidogo kuliko kukosa kabisa.

 Ni muhimu kutambua lolote linaloendelea katika siku linakuwa ni kwa ajili yako, mvua, jua na kwa ujumla hali ya hewa yote vinakuwa ni kwa ajili ya kuwezesha maisha yako yawe vizuri. (ila inategemea tafsiri ya akili yako), maana unaweza kukuta mtu analalamika ikiwa mvua anaona mafuriko na jua likiwaka anaona kiangazi.

Ni vizuri kutambua Mungu baada ya kuumba dunia katika kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri kwa ajili ya mwanadamu aweze kukaa na kumfurahia Mungu kwaku mwandalia mahala pazuri, hivyo Mungu aliingia gharama katika kuitengeneza kuanzia siku ya kwanza mpaka anafikia kumtengeneza mwanadamu katika siku zote hizo Mungu alikuwa ana hakikisha mazingira yawe mazuri ambayo mwanadamu( kipenzi chake) aweze kuifurahia kwakua kila kitu cha kuhakikisha kila kitu cha kumwezesha kuishi kinapatikana. 

Maadam umepata kuona siku nyingine naam katika wachache waliopewa neema na wengi walikosa kuiona lazima ujue umepita katika hatua nyingi sana na hatimaye kupata kibali cha kuona hiyo siku mathalani mtoto tangu mimba inapotungwa hadi mtoto anapozaliwa sio kitu chepesi ukipata neema ya kuangalia mchakato wake wa hatua ya awali mpaka hatua ya mtoto anazaliwa, kwakua wako watoto wana kufa katika kila hatua ya kufanyika kuwa mtoto ni yule tu mwenye uwezo wa kuimiri katika hali zote na hatimaye kutokea duniani.

Hivyo uone thamani kubwa sana ya wewe katika kuona siku nyingine haijarishi umeona ukiwa katika hali njema au mbaya bado uone katika yote uone neema ya Mungu iliyokupa heshima ya kukupa siku na kama zawadi iliyo kuu ya kufanya uweze kuifurahia zawadi zingine mathalani chakula, marafiki na ndugu pamoja na wale unaowapenda maana vitu vyote hivi vinakuwa na maana sana pindi unapopata neema ya kuona siku,

Ni muhimu kutambua kuwa furaha ya mtoa zawadi ni kuona unaifurahia na kuitumia sawa na vile au na lile kusudi analolitaka ulifanye atajisikia vibaya sana pindi anapokupa zawadi anapoona inakutesa, inapunguza upendo wake kwako, yaani inaondoa ibada mbele zake kwakua tumeona baadhi ya watu wanavyoitumia tofauti ya na lile kusudi alilokusudia, wako watu wanatamani siku isiishe kabla hajatimiza hazma yake inawezekana kuua, kuiba, kumfanya mtu ajute! Hama kulewa sana na mengine mengi yasiyo ufurahisha moyo wa Mungu.

Lazima utambue japo wote mmepewa siku tambua kila mtu atafaidika sawa na namna atavyoitumia mathalani inawezekana wote mnasoma kitabu kimoja lakini kila mtu anaweza kuondoka na kitu chake na akakitumia katika maisha yake kikawa msaada kwake na mwingine aliyesoma kitabu hichohicho akamaliza na akawa kama ajasoma kitu na mbaya zaidi kesho yake ikawa mbaya kuliko leo.

Ni muhimu kuwa na mtazamo sahihi katika siku yako maana siku ina maana kwakua wewe upo maana wewe ndio inaipa kuwa leo ni siku fulani, sawa na mtoto wako unapo mpa jina, lazima aishi vile uwezo wako ulivyo ndivyo ilivyo siku lazima uifanye kuwa siku yako na kuweza kuitawala na niseme kuitawala siku hahitaji fedha tu, bali akili inayojielewa na kuitumia,

Hivyo huna sababu kusema siku yangu ni mbaya kwakua ni wewe pekee unaweza kuifanya iwe unavyotaka mathalani kama njaa, shida, misiba, kusalitiwa, kuachwa na mambo mengine hiyo ni kawaida ya wanadamu na amini ingeweza kutokea mambo makubwa zaidi hapo hivyo lazima ujifunze na kuona uone upendo wa ajabu wa Mungu katika kila siku,

Ni muhimu kutambua siku inakuja kwa kusudi jema ila inategemea namna unavyoitafsiri mambo yanayotokea katika siku hiyo  kwakua ndani ya kuitafakari kuna ruhusu moyo wako kukamatwa na unaweza kuufanya moyo wako kuwa chini bila sababu yoyote.

SIKU NI NZURI IPENDE ITAKUPENDA NAAM UTAIFURAHIA!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni