Jumanne, 24 Januari 2017

NAKAZA MWENDO.



NAKAZA MWENDO.


Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu;  ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1 Wakorintho 10:13)

Ukubwa wa jambo unakuwa pale unapolitazama katika hali ya kulikuza!

Pindi unapoingia ulingoni na utakapo muona mpinzani wako namna alivyo na maandalizi yake uliyo yasikia akiyafanya katika kujiandaa kupambana na wewe unaweza ukajikuta unazimia hata kabla pambano kuanza.

Kulitazama jambo hakuna shida maadam linaonekana lakini kubwa ni namna unavyolitazama ndio linaweza kutoa picha ndani ya moyo wako katika hofu hama ujasiri katika kuliendea ili kulikabili,
Katika mashinadano mengi kuna changamoto nyingi sana hadi kufikia kwenye hatima au kuibuka kuwa mshindi na kama wangeweka MKAZO katika kutazama dhoruba zitakazo wakabili basi bila shaka kushinda ingekuwa ngumu sana,

Moja ya dalili ya mtu kuliweka na kulikuza jambo linalo mkabili ni kulia, unaweza kukuta mtu analia mpaka anazimia zimia na kumwagiwa maji napengine hata kuwekewa watu wakumwangalia wakati wote.

Ni muhimu kujua kuwa chochote utakachokipa nafasi kitachukua nafasi na kutoa matokeo yake katika maisha yako katika upande ulio wa faida au hasara, na katika ulimwengu tulionao wako watu ambao ni lazima watiwe nguvu ndio wa hamishe mawazo kutoka katika hali ya inayowakabili na kupata mwanga au njia katika maisha yanayo wakabili na wako watu walivyo pekee pasipo msaada mwingine wa nje wanapoona jambo wanaona njia ya kupita,

Ni muhimu kutambua unapoliangalia tatizo katika ya wasiwasi hapo unaweza kujikuta hali ya hofu inatanda katika moyo wako na giza litayafunika macho na miguu itakuwa mizito na kukuta unasimama njia panda usijue uende au ubaki hapo.

Atakama unajua sana na uzoefu pindi utakapo weka mkazo mkubwa katika jambo linalokukabili na kuona katika mapana yake na sio madogo hapo hofu na kuona tayari umekuwa mdogo na kamwe kutoka hapo itakuwa ngumu kwakua ndivyo unavyojiona naam ndivyo utakavyo kuwa.

Mbaya zaidi hata kama mtu mke na mme kamwe hamuwezi kurithishana namna ya kutazama jambo japo unaweza kumwambia na kumuamasisha lakini kamwe hauwezi kumpa ufahamu wako uwe kwake bado atakuwa na utayari wake wa kuamua kuchukua hama kuitikia tu.

Unapolitazama tatizo kwa maana ya tatizo ni ngumu kutoka hapo lakini ukilitazama tatizo katika ufumbuzi basi hapo utaona njia ya kupita,

Lazima ujipende na kujithamini kwa kuona kila jambo linalo kukabili ujue kuna namna la kuliangalia ili lisiwe mzigo kwako bali funzo na kuimarisha imani yako,

UKIONA VYEMA UTAPITA VYEMA LAKINI UKIONA VIBAYA UWEZI PITA SALAMA!
INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni