Jumanne, 17 Januari 2017

NENO ZURI.



NENO ZURI

Kama kitu hiki kingekuwa bidhaa basi soko lake lingekuwa kwa haraka sana, tena kwa kasi ya ajabu! Naam kama angekuwa mtu basi kila mtu angetamani awe rafiki yake na kama angekuwa mtoto basi kila mama angetamani awe wake hama awe rafiki wa mwanae……..linaitwa NENO ZURI (USIOGOPE).

Masikioni mwa watu wengi wangependa kusikia kitu/jambo hama neno zuri ili aweze kufurahi na kuzidi kufarijika na inawezekana kuwa sababu ya yeye kwenda mbele, japo maneno mazuri utegemea mtu husika namna alivyo au hali aliyonayo napia  naamini unaweza kuongea neno moja lakini likapokelewa tofauti, kwani wako watu ukiwaambia POLE wanaweza kuona una wakashifu na kuna wengine wanaweza kujisikia vizuri na kuona fahari ndani yao kwa sababu yako.

Nakuna watu wengine ukiwaambia HONGERA wanaweza kusema ona huyu naye anajipendekeza lakini wengine ukiwaambia HONGERA watajisikia vizuri watakupenda sana na kuona wewe ni mmoja kati ya watu wanaothamini kile wanachokifanya.

Hivyo neno zuri utegemea mtu/ watu husika namna watakavyolipokea!

Yako maneno mengi mazuri ambayo kwa ukweli binadamu yeyote angependa kusikia akiambiwa kila siku mathalani UNAWEZA, SONGA MBELE, UNAJUA!, USIOGOPE, JITIE NGUVU UTAFIKA, KAZA BUTI, USICHOKE BADO KITAMBO KIDOGO! Na mengine mengi.

Lakini mimi leo ningependa kuliongelea neno hili USIOGOPE!

Naamini katika maneno ambayo yanapendwa na watu wengi ni hili neno kwa kuwa tunajua kama binadamu kuna kipindi unafika uwoga unaweza kukuingia katika jambo lolote linalo kukabili na hapo unaweza kuwa na kiu ya kutaka kusikia neno USIOGOPE likitamkwa na mtu unayemwamini au kumtegemea, unayempenda na hatimae moyo wako ukainuka tena.

Nimeona hali za watu zikibadilika ghafla mara baada ya kuambiwa neon hili “USIOGOPE NIKO NA WEWE” walipokuwa wanalia ghafla machozi yakakoma, mioyo ilipokuwa imeinama ghafla ikainuka, walipokuwa wamechoka mara wakapata nguvu, alipokuwa ametendwa ghafla amani ikaingia ndani yake na kuona inawezekana kuishi na mambo yakasonga.

Uwa na penda kusema kuwa maadamu unaishi huna haja ya kuona kuna mambo yanawezekana na mengine unayo yaona hayawezekani maadamu uko na Mungu anayeweza basi atakukuwezesha nawe utaweza.

Unaweza kukuta mtu ameanza safari ya jambo lake na akakuta njiani kuna hali ya kutoeleweka na mawazo yake yakaanza kuwaza kuona bora  arudi nyuma ili ajipange vizuri lakini hapo akikutana na neno USIOGOPE likabadilisha akili yake nakuona kuwa ninaweza endelea mbele, na ni vizuri kutambua hakuna safari isiyo na vikwazo na vikwazo ndio ishara ya uimara wako.

Na niseme wazi tu kuwa hata mtu uwe unajiamini kwa kiasi gani bado utalihitaji hili neno USIOGOPE kusikia kutoka kwa mtu mwingine na pindi unapolikosa uwa unakuwa na hali ya mashaka hata kama moyo wako unajua kuwa utashinda, maadamu Mungu amekuweka na watu basi tambua wapo watakutia moyo (watafanyika Baraka) na wengine wataona bora uangamie tu lakini hatima yako haiku mikononi mwao.

Ndani ya kitabu ninachokipenda yaani BIBLIA neno hili USIOGOPE limeandikwa mara nyingi na wataalamu wanasema ukiliangalia neno hili katika biblia limeandikwa zaidi ya mara 360 kwa kusema kwamba kila siku neno hili usiogope liwe kinywani mwako katika jambo lolote hama hali yeyote uone kutoogopa ndio sehemu yako.

Ili neno liwe na nguvu kwako lazima uyajue mambo ya msingi:

i. maana ya neno USIOGOPE

II. na mamlaka anayekuambia USIOGOPE

Ni vizuriutambue kuwa Mungu amekuweka duniani sio kuishi maisha ya kuogopa na ukweli maisha ya kuogopa hayawezi kumpendeza Mungu na kamwe uwezi kuishi maisha unayopaswa kuishi kama uoga utatatawala maisha yako.

Usijali inapotokea hakuna mtu atakwambia USIOGOPE unaweza kujiambia mwenyewe na Mungu akalithibisha na amini utakuwa salama!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni