NAMNA NYINGINE
Katika dunia ya sasa utendaji wa mambo mengi umerahishwa
sana, unaweza kufanya kitu kwa njia mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo maendeleo ya sayansi na teknolojia, hali ya hewa, aina ya kitu/ jambo
husika.
Katika kufanya jambo moja, kunaweza kuwa kwa njia nyingi sana
lakini shabaha inawezakuwa ni moja kwa wote….. kama vile wote wanaweza kuwa na
nia/mwelekeo mmoja lakini kila mtu anaweza kutumia njia yake na mwisho wote
wakajikuta wamekutana sehemu moja, japo wakati mwingine utofauti wanjia ya
kutumia utegemea sana wapi umetokea hivyo mahali ulipotokea unaweza kukupa
mwelekeo ambao ni tofauti na mwingine,
Tukiangalia katika uwasilishaji wa habari unaweza kutumia
njia nyingi kutokana na uwezo wako na uelewako kama sio umahiri wako unaweza
kuwasilisha habari kupitia njia za mitandao fb, twitter n.k au kutumia media
mathalani radio, tv japokuwa njia ni tofauti lakini inawezakana kuwa ni habari
moja inayowasilishwa kwa njia nyingi.
Vilevile wako wataalamu wanaweza kuwasilisha ujumbe kwa namna
mbalimbali mathalani kwa njia ya picha, kinyago hama kwa njia ya maandishi
lakini unaweza kukuta wote wanawasilisha jambo moja inawezekana kuwa hali ya
siasa nchini, ubora wa kitu, tuuthamini utamaduni wetu ,umuhimu wa amani hama
tuyatunze mazingira na mengine mengi.
Japo watu kuamua kutumia namna nyingine katika kufanya jambo
kunaweza kuwa kwa nia njema hama la! Kwakua wapo watu kwakuwa hawapatani na mwenzao
hivyo uweza kutumia namna nyingine kuonyesha kuwa akubaliani,
Nakubaliana kuwa wakati mwingine katika kufanya jambo moja
kunaweza weza kuibuka kwa namna mbalimbali katika kulitekeleza jambo moja na pengine
hiyo njia ikaleta matokeo mazuri na kwa haraka mathalani ujumbe unaweza kutumia
simu kuwasilishwa sehemu husika kuliko kutumia barua kutuma kwa mtu inaweza
chukua muda kulingana na umbali, hama kutoka katika matumizi ya jembe kwenda
kutumia trekta.
NAMNA NYINGINE!
Tumeona watu wakikubali hama kukataa kutokana na kupata namna
nyingine katika kufanya jambo, wazo jingine, nia nyingine, maamuzi mengine
katika kufanya jambo unaweza kukuta mtu alishauriwa ilikupunguza unene lazima
upunguze kula na baada ya kupata wazo hama ushauri mwingine inawezekana kufanya
mazoezi tu,anaweza kuacha njia moja na kuingia katika njia nyingine hama
kutumia njia zote inategemea halmashauri ya ubongo wake.
Wako wako watu wameshindwa kwenda mbali/ kupata kile
wanachokitaka kwa sababu ya kukosa
kutambua njia nyingine katika utatuzi wa jambo………mathalani kilimo unaweza
kukuta mkulima analima apati mazao ya kutosha sawa na vile anavyotegemea kwa
kukosa njia nyingine uweza kujikuta akaghairi kulima kabisa badala ya kutafuta
namna nyingine ya kilimo chenye tija, hama kupata uelewa kuhusu namna ya
kuitunza ardhi ili iweze kuwa na rutuba na hatimaye aweze kupata mazao
anayoyataka.
Ni kweli unaweza kuwa unaomba sana na unasoma Neno la Mungu,
unapoona hakuna mpenyo katika yale unayoyafanya lazima utafute namna nyingine
ili maombi na Neno liwe na faida katika maisha yako na sio dawa kuacha kwakua
umefanya kwa muda mrefu na hakuna matokeo unayo yategemea maana kila jambo kuna
namna namna yake yakulifanya tena kulingana na wakati na uhitaji uliopo sawa na
Roho mtakatifu atakavyokuagiza,
Upaswi kukariri kuwa ukimsikia mtu anacheka basi anafuraha
wako watu wanavyolia ukiwasikia kwa mbali unaweza fikiri wanacheka,
Upaswi kuweka imani mbali na Neno la Mungu kwakua unaweza
kukuta mtu ana amini kuwa akiuza maembe Tabora basi yatatoka kwakua rafiki yake
alipeleka maembe roli zima yote yakaisha anaamini na yeye akipeleka yake
yataisha pasipo kujua ule ulikuwa msimu gani?
Upaswi kukubali kushindwa kwa kuliona jambo limeshindikana
bali tambua kila jambo lina njia zake katika utatuzi wake sio lazima utatue kwa
njia moja hama kwa namna ulivyofikiria, kuna njia nyingi ni wewe kukubali
kuitumia tu.
Ni vizuri ufahamu uwe umetengenezwa kutatua kila jambo litakalo
kuja mbele yako na sio kukariri jambo moja namna ya kulitatua yakija mengine
yanakuweka chini, kumbuka utatuzi wa jambo ndio unapelekea amani, ushujaa na
zaidi sana kuzidi kumpenda Mungu.
KUJIKWAA SIO MWISHO WA
SAFARI BALI NI NAMNA NYINGINE YA KUJIFUNZA!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………….0764 018535