Jumanne, 21 Februari 2017

KUJIKWAA SIO MWISHO WA SAFARI BALI NI NAMNA NYINGINE YA KUJIFUNZA!



NAMNA NYINGINE

Katika dunia ya sasa utendaji wa mambo mengi umerahishwa sana, unaweza kufanya kitu kwa njia mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maendeleo ya sayansi na teknolojia, hali ya hewa, aina ya kitu/ jambo husika.

Katika kufanya jambo moja, kunaweza kuwa kwa njia nyingi sana lakini shabaha inawezakuwa ni moja kwa wote….. kama vile wote wanaweza kuwa na nia/mwelekeo mmoja lakini kila mtu anaweza kutumia njia yake na mwisho wote wakajikuta wamekutana sehemu moja, japo wakati mwingine utofauti wanjia ya kutumia utegemea sana wapi umetokea hivyo mahali ulipotokea unaweza kukupa mwelekeo ambao ni tofauti na mwingine,

Tukiangalia katika uwasilishaji wa habari unaweza kutumia njia nyingi kutokana na uwezo wako na uelewako kama sio umahiri wako unaweza kuwasilisha habari kupitia njia za mitandao fb, twitter n.k au kutumia media mathalani radio, tv japokuwa njia ni tofauti lakini inawezakana kuwa ni habari moja inayowasilishwa kwa njia nyingi.

Vilevile wako wataalamu wanaweza kuwasilisha ujumbe kwa namna mbalimbali mathalani kwa njia ya picha, kinyago hama kwa njia ya maandishi lakini unaweza kukuta wote wanawasilisha jambo moja inawezekana kuwa hali ya siasa nchini, ubora wa kitu, tuuthamini utamaduni wetu ,umuhimu wa amani hama tuyatunze mazingira na mengine mengi.

Japo watu kuamua kutumia namna nyingine katika kufanya jambo kunaweza kuwa kwa nia njema hama la! Kwakua wapo watu kwakuwa hawapatani na mwenzao hivyo uweza kutumia namna nyingine kuonyesha kuwa akubaliani, 

Nakubaliana kuwa wakati mwingine katika kufanya jambo moja kunaweza weza kuibuka kwa namna mbalimbali katika kulitekeleza jambo moja na pengine hiyo njia ikaleta matokeo mazuri na kwa haraka mathalani ujumbe unaweza kutumia simu kuwasilishwa sehemu husika kuliko kutumia barua kutuma kwa mtu inaweza chukua muda kulingana na umbali, hama kutoka katika matumizi ya jembe kwenda kutumia trekta.

NAMNA NYINGINE!

Tumeona watu wakikubali hama kukataa kutokana na kupata namna nyingine katika kufanya jambo, wazo jingine, nia nyingine, maamuzi mengine katika kufanya jambo unaweza kukuta mtu alishauriwa ilikupunguza unene lazima upunguze kula na baada ya kupata wazo hama ushauri mwingine inawezekana kufanya mazoezi tu,anaweza kuacha njia moja na kuingia katika njia nyingine hama kutumia njia zote inategemea halmashauri ya ubongo wake.

Wako wako watu wameshindwa kwenda mbali/ kupata kile wanachokitaka  kwa sababu ya kukosa kutambua njia nyingine katika utatuzi wa jambo………mathalani kilimo unaweza kukuta mkulima analima apati mazao ya kutosha sawa na vile anavyotegemea kwa kukosa njia nyingine uweza kujikuta akaghairi kulima kabisa badala ya kutafuta namna nyingine ya kilimo chenye tija, hama kupata uelewa kuhusu namna ya kuitunza ardhi ili iweze kuwa na rutuba na hatimaye aweze kupata mazao anayoyataka.

Ni kweli unaweza kuwa unaomba sana na unasoma Neno la Mungu, unapoona hakuna mpenyo katika yale unayoyafanya lazima utafute namna nyingine ili maombi na Neno liwe na faida katika maisha yako na sio dawa kuacha kwakua umefanya kwa muda mrefu na hakuna matokeo unayo yategemea maana kila jambo kuna namna namna yake yakulifanya tena kulingana na wakati na uhitaji uliopo sawa na Roho mtakatifu atakavyokuagiza,

Upaswi kukariri kuwa ukimsikia mtu anacheka basi anafuraha wako watu wanavyolia ukiwasikia kwa mbali unaweza fikiri wanacheka,

Upaswi kuweka imani mbali na Neno la Mungu kwakua unaweza kukuta mtu ana amini kuwa akiuza maembe Tabora basi yatatoka kwakua rafiki yake alipeleka maembe roli zima yote yakaisha anaamini na yeye akipeleka yake yataisha pasipo kujua ule ulikuwa msimu gani?

Upaswi kukubali kushindwa kwa kuliona jambo limeshindikana bali tambua kila jambo lina njia zake katika utatuzi wake sio lazima utatue kwa njia moja hama kwa namna ulivyofikiria, kuna njia nyingi ni wewe kukubali kuitumia tu.

Ni vizuri ufahamu uwe umetengenezwa kutatua kila jambo litakalo kuja mbele yako na sio kukariri jambo moja namna ya kulitatua yakija mengine yanakuweka chini, kumbuka utatuzi wa jambo ndio unapelekea amani, ushujaa na zaidi sana kuzidi kumpenda Mungu.

KUJIKWAA SIO MWISHO WA SAFARI BALI NI NAMNA NYINGINE YA KUJIFUNZA!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni