MISULI YA
NDANI
Moja
ya ushupavu wa mtu katika muonekano wa nje ni kuonekana kwa misuli ikitandaa
katika sehemu ya mwili wake mathalani mikononi na hata miguuni.
Ina
aminika kuwa pindi mtu atakapoanza kuonekana kuwa na misuli bila shaka watu watajua
mtu huyu ameanza kufanya mazoezi na wengine watasema anataka kuimarisha mwili
wake hama kutengeneza muonekano mzuri katika mwili,
Japo inawezekana mtu kuamua maamuzi hayo ni baada
ya kuona watu wakiwa na muonekano tofauti tofauti wa kupendeza kutokana na mazoezi
wanayo yafanya,
Japo
ilikuwa na mwili ulioimara sio lazima utoke misuli kuna aina ya mwili misuli
haionekani kwa nje kama wengine lakini mwili wake uko vizuri na tishio hata kwa
wale wenye miili iliyotuna kifuani hama sehemu nyingine katika mwili wake.
Katika
kutoa maana ya neon MISULI ningependa tujikite katika dhana ya UIMARA,
Kutoka
hapo ndipo tunapata kuona watu wamewekeza hama wamesimamia wapi na kutoa picha
inayojidhirirsha katika mienendo yao, katika hili wako watu uimara wa imani zao
unakuja pale anaposikia shuhuda basi
hapo ujenga imani kuwa kama imewezekana basi hata mimi itanitokea na pengine
hata kujipa matumaini kama kwa mtu ametendewa wakati mwingine unaona kama wewe
ulistahili zaidi basi una weka mkao wa wewe kutendewa
Wako
wengine uimara wao wameweka katika kufahamiana na watu wengi, wakijua kuwa
kwakua wanafahamiana na watu basi wako salama hivyo shida yake itakuwa ni
rahisi kutatuliwa kwa kuwa ana amini katika nguvu ya wengi hakuna kitu
kitakacho mshikilia sana,
Wako
wengine pia wamejiona kuwa wako salama na imara kwasababu wanafahamiana hama kujulikana na mchungaji hama watu waliokaribu hama
mke mchungaji hivyo anaweza kujiachia na kufanya anachoona na kujiona yeye
ana nafasi na kamwe hakuna ataye mtingisha kwakua ameshikwa na mihiri ya
kanisa,
Pia
wako wachache ambao misuli yao ya ndani imetengenezwa na neno la Mungu hama
Mungu mwenyewe watu hawa wana muona Mungu kuwa ndio uimara wao, ushindi wao na
ushupavu wao wana amini wanaweza fika popote kwakua waliye nao anaijua njia.
Misuli
ya ndani uwa haiweki msingi wake katika yale yanayomkabili sasa bali hata
yatakayo mkabili bado anaona atakuwa salama tu!
Daniel 3:16
Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu
katika neno hili.
17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru
ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.
18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali
kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Ni
watu huwa awaogopi kupoteza kitu chochote ili mradi wasimkose Mungu kama
watumishi hawa shadraka, meshaki na Abednego walikuwa tayari ni bora kuangamia
wakiwa mikononi mwa Mungu kuliko kuishi maisha yaliyo mbali na Mungu,
Watu
wana mna hii Mungu uwatafuta ili aweze kujivunia na kuona fahari juu yao kwakua
Mungu ujivunia katika kitu kilicho bora na sio kitu kilichopo tu,
Ili
ufike mbali lazima uhakikishe misuli yako ya ndani inajengwa na kuimarishwa na
NENO LA MUNGU kwa kulikubali hili neno utafanya Mungu mwenyewe ashughulike na
wewe katika kukuhakikisha unakuwa bora na wa maana zaidi.
KUBALI KUWA FAIDA KWA MUNGU UPATE
MATUNDA YAKE HAMA KUBALI KUWA FAIDA KWA WANADAMU UPATE HASARA ZAO!
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni