UBORA WA MTU
Kuna dhana mbili zinazo kinzana kama sio kushabiriana UBORA
/UMUHIMU
Ukweli ni makosa sana kufananisha umuhimu na ubora japo
wakati mwingine kutokana ubora wa mtu uweza kupelekea umuhimu wake, kwa maana
kama hakuna uhitaji wake/ umuhimu wake basi watu uweza kuona hapo hakuna UBORA
wakati ubora siku zote uko ndani yake lakini umuhimu upo penye uhitaji tu.
Japo kuwa ubora wa mtu anakuwa nao mtu ndani yake lakini
umuhimu wa mtu unaoneka pale atakapoonyesha utendaji wake, na wakati mwingine
umuhimu wa kitu uonekana pale kinapokosekana, kwa hivyo yale mambo yake
yanapokosa mbadala basi hapo ndipo uona nafasi yake.
Nipende kusema kuna wakati UMIHIMU wa kitu unaweza isha
lakini sio ubora uliondani, kwakua ubora ni kitu alichokiweka Mungu ndani ya
mtu kwa faida yake,
Ubora wa mtu ahuonekana katika muonekano wa mtu japo umuhimu
wa mtu unaweza kutokana na muonekano mathalani mashindano ya urembo, model uwa
wanapenda watu wenye umbo fulani lakini huo sio UBORA wa mtu.
Ubora wa mtu tunauona kwa Mungu pale alipo amua kumuachilia
mwanae kipenzi kwa ajili ya mwanadamu!
UBORA WA MTU!
Kama mzazi pindi anapomwangalia mtoto wake uwa siku zote
anamuona kuwa katika UBORA WAKE ( kwa mzazi mwenye akili) na sio kwa umuhimu
wake, maana anajivunia yeye anajisifia yeye na fahari yake imebebwa na yeye,
Ndo mana Mungu alionyesha THAMANI/UBORA wa manadamu kwa
kumtoa kipenzi chake, kwa maana rahisi tu kuwa Mungu alitoa kipenzi chake kwa
ajili ya wapenzi wake, mwanadamu ulivyo kuwa bora ili mlazimu atoe kilicho
bora,
Japo katika dunia ya sasa ubora wa mtu umekuwa ukichukuliwa
katika hali isiyo sawa ndomana watu kuutoa uhai wa mwenzake kwa ajili ya maslai
binafsi hawaoni shida, kumtoa kasoro mtu kana kwamba anaweza kumrekebisha,
unaweza kukuta mtu anasema”mwangalie anamacho makubwa kama mguu wa tembo
asingekuwa anayatoa maana yanatisha” mtu anaongea kwa ujasiri tena pengine
wakitiana ujinga na mwenzao huku wanacheka kwa kebei.
Unaweza kukuta mtu anasema”huyu jamaa ombaomba yaani akikuona
lazima akubomu ingefaa naye awe mgogo na aende Dodoma” watu wanasema tu kwa
kuwa wamepewa kinywa cha kusema kwa hiyo wana kitumia vile wanavyoona na wala
sio kama wanavyopaswa,
Pia unaweza kuta watu wanasema “ king’ang’anizi kaja yani
akishiria jambo lake hata la uongo yani huyu mbishi yani ruba anasubiri kwa ung’ang’anizi wake
bora angekuwa super glue ingejulikana moja, mangi angeuza iishe”
Yako mengi lakini watu wako huru kana kwamba wanamjua
mwanadamu kinagaubaga hama walikaa na Mungu wakati anamtengeza mtu au huyo
jirani yake,
Marko 12:31 Na
ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako
kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Biblia imekosa lugha nzuri yakueleza ikasema kama unavyojiona
na kujipenda, kujithamini basi fanya hivyo kwa mtu yeyote pasipo kujali unamjua
hama umjui,
1 Yohana 4:20 Mtu
akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni
mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu
ambaye hakumwona.
Lazima ujue hatima umeshika na wewe ila Mungu ndio muamuzi, sio
kila hali aliyonayo mtu binafsi anaifurahia laiti ungeuona usiku wake namna
macho yake yanavyolowesha mashuka yake usinge thubutu kuwaza tofauti na namna
unavyopaswa kuwaza,
UBORA WAKO NA WAKE NI SIRI
YA MUNGU!
ANAITWA MUNGU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………..0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni