Jumatano, 1 Machi 2017

ISHARA KUBWA YA KUJIPENDA! PENDA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO.



THAMANI YA KITU KILICHOPOTEA!


Hili limekuwa tatizo la wanadamu wengi hasa waafrika kuona thamani ya kitu mara baada ya kutokuwepo tena……unaweza kuwa na chepeo/koleo likawepo tu nyumbani pasipo na uangalizi wowote kwa sababu uhitaji wake bado hivyo ukapoteza umakini juu ya hicho kifaa pindi kikatoweka kwa kuibiwa hama hali yoyote mathalani mvua na hapo pakatokea uhitaji wake ndipo uanza kulitafuta kwa bidii na kuuliza kila kona jamani mmenionea wapi kifaa changu maana nina kazi nacho na bila hicho hali itakuwa ngumu sana “naombeni mnisaidie”

Unaweza kuwa ukipendi kiungo kimoja wapo katika mwili wako mathalani kidole katika mguu wako kwa kuwa watu wanakisema kimekaa vibaya lakini siku mguu wako utakapoondolewa kwa sababu mbalimbali hapo ndipo utaona ubora na hauta ona kasoro yoyote ya kile kidole ambacho wengi waliona akikosawa,

Tumeona watu walioishi na kujisifia uzuri wao na baadae ulipopotea akaanza kuwa mpole na tambo/majivuno yote yakaisha pia wako walikuwa na pesa nyingi sana lakini baada ya kipindi pesa zikaisha akawa anakumbuka enzi zile alizokuwa na pesa sio hayo tu pia wako watu walikuwa wakimiliki madini ya gharama kubwa lakini muda hiyo biashara ikaondoka mikononi mwao na wakajikuta wakiwa katika hali mbaya sana na wengine baada ya kushindwa kuimiri maisha mapya tofauti na walivyo zoea wakajikuta wamekuwa chizi,

Katika maisha ya kawaida ya wanadamu kunakipindi unaishi na vitu/kitu kana kwamba unaishi nacho/navyo milele, ukajisahau na ukaona kuwa wewe tayari umeshafika hama umeshapata.
Naweza sema thamani ya kitu kilichopotea hakuna uwezo wa kukikisia ukapata hile thamani yake halisi kinachotakiwa kuwa nacho!

KARIBU!
Ujue kama mwanadamu kuna vitu ukivipoteza unaweza kupata mabadala wake na maisha yakaendelea mathalani vitu vilivyo nje ya wewe ukivipoteza na moyo uka chini kwa muda fulani lakini baadae ukapata mbadala basi furaha inaweza ikaendelea hama neema ya Mungu ikauwisha nafsi yako ikawa imara tena!

Lakini sio vitu vya ndani yako alivyoweka Mungu mwenyewe kwa kusudi lake ukashindwa kuvitendea ipasavyo na hatimaye vikashindwa kuleta faida kwa Mungu, hapo ugomvi wake unakuwa wewe na Mungu na hakuna kisingizio yeye ataelewa, labda jirani yako amepelekea  ukashindwa kukitendea kazi kile kilicho ndani yako, Mungu maadamu amekupa anajua kitafanya kazi japo kuwa wewe ndio muhusika mkuu wa kukiruhusu

-isije kama ya Adam na Eva kuwaza kusingiziana, badala ya kufuata maelekezo waliyopewa,
Mathayo 25:14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
                    15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
                    16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
                    17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
                    18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
                    19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
                    20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.
                 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
                 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.
                 23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
                 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
                 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
                 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
                 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
                 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
                 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
                 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
                  31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

Ni kweli ukikosa mengine Mungu atakupa faraja lakini sio kusudi likiondolewa ndani yako hapo faraja ya Mungu inakosekana unakuwa mpweke hata kama unakila kitu ambacho ulifikiri kitaleta amani ndani ya maisha yako,

Niseme wazi kila jambo mtu analifanya anataka faida lakini ujue kuwa pasipo faida anaona hakuna maana ya kuendelea kulifanya,

Ni muhimu kuheshimu kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako baada ya kuona unastahili kuwa nacho aijarishi ni kidogo hama kikubwa bado aliona unaweza kukifanyia kazi,

Na ukumbuke kuwa amehakikisha uwepo duniani na anakuhudumia kukufanya uendelee kuishi kwa sababu ya hilo, sawa na mtu aliye ajairiwa na kupewa nyumba, gari na mshahara kuna kusudi ambalo anatakiwa alitekeleze ili hiyo kampuni iweze kufaidika naye,

Mungu anashida na unaonekaje! Bali anashida na lile kusudi aliloweka ndani yako kuhakikisha kuwa linamletea faida aliyoitaka ndani yako.

ISHARA KUBWA YA KUJIPENDA! PENDA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni