AMANI YANGU!
Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Tunakubaliana kuwa unapozungumzia AMANI ni mbali na kicheko, kufurahi hama tabasamu…… japo hivi vyote vinaweza kubebwa na amani, na sio lazima vikiwepo hivi ni dalili ya kutosha kuwa hapo pana amani,
Katika swala linalobeba ubinafsi kwa kiasi kikubwa ni hali hii inaitwa AMANI kwani unaweza kuwa watu zaidi 10000000 katika sehemu moja na wote mkaonekana wanafuraha, wanacheka na kucheza kwa pamoja lakini katika hali hiyo kila mtu anakuwa siri ya moyo wake ( mambo yanayoendelea ndani ya moyo wake) bila shaka wako watu wengine watakuwapo hapo lakini awana utulivu wa akili hata moyo yaani makazi ya AMANI,
Tafsiri rahisi ya kidunia hili neon amani ni hali ya moyo kukubaliana na hali iliyopo haijarishi wengine wanaonaje(kuridhika kunako pelekea kufurahia).
huwezi kutambua AMANI ya mtu kwa kuangalia muonekano wake namna alivyo vaa hama anavyoongea tu kwakua wapo wenye hulka ya kuchekesha sana (yani ukimuona tu unajisikia kufurahi) lakini siri ya moyo wake anaijua mwenyewe.
Tunakubaliana kuwa Amani isipokuwepo basi hapo radha ya vitu inatoweka hata kama ni chakula chenye ubora gani? Hama gari lenye thamani kubwa kiasi gani ? hama nyumba yenye fahari kubwa kiasi gani kamwe hauta ona maana ya kuwa navyo kwakua kiunganishi chema kati ya moyo wako na vitu ulivyonavyo hakipo.
Napia unaweza kuwa na kitu hama mtu ambaye watu wote wakashindwa kupata tafsiri sahihi ya wewe kuwa naye inawezekana wakikuchukua wewe na yeye hama hivyo vitu ulivyonavyo hawaona kuwa ulitakiwa kuwa hapo/kuwa na mtu huyo lakini kwakua hivyo vitu viunganishwa na amani ya moyo wako wewe ndio unawashangaa hao watu kwakua wanawaza hivi kana kwamba wanaishi wao na wala sio mimi nabinafsi ndio ulichukua maamuzi kwa utashi wa akili yako na Uradhi wa mapenzi ya moyo wako.
Tafsiri rahisi ya dunia kuhusu Amani ni hali ya uhakika wa kitu chema,hivyo uishi katika matumaini na kujipa moyo kuwa ipo siku kile anachokitamani hama shauku nacho kitatimia kwa majira fulani lakini hali hii ni tofauti kwa mtu anayemwamini Mungu uwa anajua kwa sababu yuko na Mungu basi amani yake hipo Mungu ndio amani inayotawala ndani yake, hivyo matumaini yake hayako katika vitu bali yako ndani ya Mungu, ndiko amani yake iliko fichwa na iko salama.
Katika swala hili la AMANI uwa hakuna maombi yatakayoleta amani ndani ya maisha zaidi ya kuwa mbeba Amani aingie ndani yako aichie amani yako ipitayo akili zako na kukupa utatuzi katika maisha yanayo kukabili.
Uwa hakuna mwendelezo wa kudumu kama kuna kitu unafanya pasipo amani kwakua hauta kifurahia sana na lolote linaweza kutokea haijarishi umelipanga au la! Kwani kuwa na mtu hama kitu au kufanya shughuli yoyote pasipo kuwa na amani nayo hapo ni sawasawa na kutembea na mtu pasipo kunia mamoja hama kupata……. hivyo kila mtu utembea na akili yake mwenyewe hivyo hapo kuachana ni jambo linalowezekana tu! Hama kuacha shughuli unayoifanya.
Katika dunia utasikia sana watu wakisema “ mimi nailinda amani yangu” lakini ukweli amani hailindwi kwa namna unavyoweza fikiria bali mwenye asili ya amani anayeichupua katika mazingira yote haijarishi nini kimekukumba amani yake inazidi hilo jambo lakini kwakutumia akili ya kibinadamu yako mambo ambayo utashndwa kuyaimiri na hatimae ukakuta uko chini.
Ni muhimu kutambua Amani ni mali ya Mungu yaani inapatika katika himaya ya Mungu hivyo unahitaji wewe kuwa wa Mungu kweli hili amani yake iwe ndani yako na wala sio kuomba mchana na usiku, amani yake ikupe uwezo wa kumudu kila kishindo hatimae uweze kuwa bora katika kila kona.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni