JANA SIO LEO JAPO ZOTE NI SIKU!
Utofauti wa kitu usichotegemea kuwa tofauti ndio usumbufu wa
akili ya mtu!
Tukiangalia mfano wa mama aliye na mtoto mdogo pindi
anapotambua chakula kile mtoto apendacho hama kinywaji kile mtoto atakacho
hivyo kutoka na mapenzi makubwa kwa mtoto wake uhakikisha kile apendacho mwanae
anampatia sawa na uwezo wake lakini pindi atakapo tambua mbona ajakifurahia
vizuri hama ajachangamkia kama ilivyo kawaida yake hapo maswali kwa mama uweza
kuibuka kwanini mwanangu ali vizuri kama jana je! Ana nini? Kipi kinamsumbua
ndani yake? Hapo tofauti ya jana na leo unaweza kuiona,
Kinachomfanya mtu awe na maswali pindi atakapo kutana na mtu
ni hile hali aliyoizoea kuona kuwa haipo tena hata kama kwa udogo maadamu
kunatofauti basi ujua kuwa hii hali ni ya dalili mbaya/nzuri hivyo uweza kutoa
chumba cha mawazo kuhusu hilo jambo na kutafuta kwanini huyu rafiki amekuwa
tofauti inawezekana ni kwa sababu yangu hama yake mwenyewe hama upendo
umekwisha hama unaelekea ukingoni,
Japo nakubaliana kabisa pindi unapoona utofauti wa hali
yoyote kwa mtu au kitu bado uko una maamuzi ya kuweza kutafuta ufumbuzi hama
kupotezea ukisema lolote na liwe tu! Kwani yeye ameshika pumzi yangu.
Pia na amini sio kila utofauti unaojitokeza unakuwa na
utatuzi mmoja uko utofauti mwingine utaitaji upe nafasi kwanza na uko utofauti
ambao unahitaji ukabili mapema kabla ujawa mkubwa ukashindwa kuupatia ufumbuzi
pia uko utofauti ambao unahitaji kuupotezea maana wakati mwingine ukichukua
nafasi ndani ya maisha yako utakuchelewesha kuyafanya mambo ya msingi hama
kufanya mambo kwa ufanisi,
Naamini tatizo sio utofauti uliojitokeza bali kwanini
utofauti umetokea? Jibu la hapo ndilo linaweza kuzaa moyo kuwa chini hama
kuweza kuikabili hali hiyo iliyojitokeza.
Unaweza kuwa mtu kuwa hauna pesa kwa sasa lisiwe tatizo kwako
kwakua labda kuna mahali umewekeza na unategemea kupata mrejesho mzuri tu kwa
muda mfupi lakini inapotokea ukajikuta huna hela kutokana na matumizi mabaya
hama umeibiwa na hauna akiba hapo jambo hilo linaweza kuleta shida,
Katika maisha ya mwanadamu kuna kipindi hama siku unazozipenda
kiasi kwamba unatamani ziendelee tu maana zinaleta faraja sana katika maisha
yako! Wakati mwingine unafikiria hivi jana nilifanya nini ikawa hivi ngoja na
leo niongeze umakini labda itajirudia ile jana ukweli hali hii inakuwa njema
sana pale hali ya jana inapojirudia lakini inakuwa mbaya sana ile hali ya jana
inaposhindwa kijirudia kwa maana hapo ndipo maswali na kuchanganyikiwa kunaweza
kuzaliwa,
Lakini inapotokea utofauti wa kitu ambacho ulikuwa unahisi
kitabadilika hama kujua kabisa kitabadilika hapo inakuwa ni rahisi tu kwakua
akili yako ilikuwa imesha jua mathalani nyama/samaki wabichi wasipo tunzwa
kwenye friji katika mazingira ya joto bila shaka baada ya siku chache
utakapoanza kusikia harufu hauta shtuka sana kwakua unajua uwezekano wa mboga
hiyo kuharibika ni mkubwa kutokana na hali halisi.
Ndomana mtu mmoja anaweza kuwa katika pande mbili mkionana
anacheka na mkiwa mbali anaanza kukuponda, mchana rafiki na usiku ni adui yako,
Ndomana unaweza kuwakuta watu jana walikuwa marafiki sana
kiasi kwamba ilikuwa uweza kutabiri kuwa ipo siku watatengana au kuwa mbali
lakini siku inafika unashangaa hivi leo mmekuwa hivi.
Usikubali kutembea kwa namna hilehile uliyoizoea hatakama ni
nzuri lazima uandae akili yako kukabiliana na hali itakayokubali ili mradi
USALAMA WAKO uzidi wala usipungue siku baada ya siku,
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni