Jumanne, 28 Machi 2017

BABY FACE



SURA YA MTOTO

Moja ya furaha katika familia nyingi za waafrika ni watoto, imefikia kipindi kuwa ndoa inaweza kudumu sio kwasababu kuna mapenzi bali kwakua kuna watoto ambao ndio kiunganishi cha wana ndoa hao hivyo wanaweza kuendelea kuishi maadam Mungu amewajalia pumzi sio kwa maana ya mke na mme,

Kiafrika sio swala la kushangaza kuona ndoa imevunjika kwasababu ya kukosa mtoto japo kuwa na watoto hakuna maana ndoa haita vunjika! Sababu ziko nyingi sana ambazo wanadamu wanazo lakini sina uhakika sana kama Mungu anazitambua na kuhalalisha kuachana,

Kwahiyo mtoto katika familia ni kivutio, heshima, staha, majivuno na naamini pia ni sifa kwa mwanamke kuwa anazaa.

SURA YA MTOTO ni furaha ya wazazi hasa inapotokea mtoto anafanana na baba, na kwa upande mama kama yeye ni mwaminifu katika ndoa itapunguza maswali upande wa kiumeni, kwakua kufanana na baba maswali yanakuwa sio mengi lakini akifanana na mama maswali uweza kujitokeza.
Mama yeyote mwenye akili uwa awezi kujizuia pindi anapomuona mwanae anacheka/anafurahi bila shaka na yeye atakuwa na sura ya tabasamu lililoanzia moyoni na kwenda hadi kwenye muonekano wanje!

Katika dunia ya sasa wanawake wengi wamekuwa wakitamani sana vitu vya watoto utakuta wanaitana BABY FACE moja ya maana zao sura iliyo na muonekano mzuri usio na makunyanzi wala ma waa! Ngozi ili nawiri na kupendeza………………….mabinti wengi wamekua wakiambiana hivi wamekuwa wakijisikia vizuri hata kutamani kuendelea na kutumia mafuta hama lotion iliyomfanya mpaka asifiwe kuwa anakabebi face, bila shaka unapomtamkia binti kuwa anakabebi face anaweza kutamani kuwa rafiki yako kwakua umemsifia naye amejisikia vizuri na ni kawaida ya binadamu yeyote kupenda sifa mathalani una mwambia umefanya vizuri, umependeza, umetokelezea hama umefunika.

Hali hii imepelekea hata mabinti wengi kudanganyana kuambiana kuwa wana muonekano mzuri katika sura yake na huku wanamkejeli  unakuta yule binti kujisikia vizuri lakini baadae anapotambua kuwa walikuwa wana msanifu anaweza kujisikia vibaya sana!

KARIBU SANA!

Sura ya mtoto imebeba tafsiri nyingi sana kwa mama pindi anapomuona na kumwangalia anakumbuka mengi wakati mwingine anaweza kucheka peke yake hama kuhuzunika kutegemea mwegemeo wa kumbukumbu yake,

Katika hili napenda tujifunze kitu kimoja katika SURA YA MTOTO kwa maana kuna mfanano mkubwa wa kile anachokifanya kwa nje na kile kinachoendelea ndani, uwa hajui maana ya UNAFIKI, uwa anapotabasamu hama kucheka uwa ana maanisha hivyo………ndomana mtoto akiwa anaumwa utamuona katika sura yake namna ilivyopoa ucheshi wote umekwisha ( kwa mwenye hulka ya ucheshi) analia hovyohovyo tofauti na ilivyo kawaida yake.

Muonekano wa mtoto katika sura yake ndio kusudi la Mungu katika maisha yetu mbele zake na mbele za wanadamu, japo kwa sasa unaweza kukuta mtu anacheka sana lakini amaanishi kabisa kucheka, anakuwa zaidi ya wenye tasnia ya wachekeshaji.

Marko 10:15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.

Mwenendo wa mtoto unaubariki sana moyo wa Mungu, anapo samehe  ana maanisha na anapopenda pia ana maanisha sura yake iliyobebwa na hisia zake uwa zinaonekana katika sura yake, hivyo upati shida kutambua hiki nilichokifanya nimemfurahisha hama nimemuhuzisha pindi utakapomuangalia katika uso wake utatambua ukweli usio kuwa na maswali lakini sio kwa watu wazima anaweza akacheka hadi jino la mwisho lakini hakuna la kweli hata mmoja siri iko ndani yake.

SURA YA MTOTO NDANI YA SURA YAKO NDIO FURAHA YA MUNGU!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson………………………………………………………….0764 018535

“Sura inayosadifu kilicho ndani ya moyo wa mtu”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni