NGUVU YA UKIRI
Tunapozungumzia ukiri hii ni zaidi ya kusema, pindi utakapo
kuwa na furaha hama huzuni!
Unaweza ukaongea maneno mengi kwa misisimko najazba pamoja na
maamuzi ya dhati yasiyo usisha moyo katika ufahamu ulio mkamilifu hapo hakuna
NGUVU YA UKIRI
Ni muhimu kujua ukiri wako unaongoza maisha yako katika mema
hama mabaya, muda mwingi mtu anapo kuwa katika hali ngumu katika maisha yake
uwa moyo wa mtu huyu unazungumza mambo mengi wakati mwingine anaweza kujuta
hama kujilaumu sana.
Yako mambo yanapotokea hasa katika upande hasi watu wengi
uweza kujiapiza na kusema maneno mazito mathalani mtu uweza kusema katika
maisha yangu sitakaa na kuzungumza nae kwa namna alivyo nitenda hakika sitakaa
nisahau! Uwa maneno ya namna hii mara nyingi uambatana na hasira na wakati
mwingine hasira zikisha poa uweza kubadilika hama kuendeleza na msimamo wako,
Sio kila ukiri una nguvu, bali ukiri unao maanisha ukibebwa
na mizizi ya moyo na ufahamu kamili.
Nazungumzia ule ukiri unaoweza kukutenga wewe na furaha hama
amani yako na hata kusababisha afya ya mtu kudhoofika, akili kudumaa na hata
kusababisha mahusiano kufa na kupelekea mtu kuishi maisha ya upweke.
Moja ya njia ya kutambua ukiri wako ni badiliko la dhati
katika mfumo wa maisha yako; unaweza kukuta pindi mtu atakapo kutana na mtu
hama baadhi ya watu utakuta ana badilika kabisa, ata kama anataka kununua
bidhaa yuko tayari aache pesa zote dukani kuliko kuonana na mtu huyo hama kundi
hilo, dalili kubwa ya ukiri ni hali ya kutofanya yale uliyo yazoea kuyafanya.
Ni muhimu kutambu atupaswi kuchukua maamuzi au ukiri kutokana
na tendo ulilofanyiwa ujapendezewa bali katika yote iruhusu AMANI YA KRISTO,
ichukue nafasi katika maamuzi yako.
Uwa na amini kila maamuzi ya mtu yanayo ambatana na ukiri ulio
na makusudi ya kuleta unafuu wa nafsi ya mtu na amani ya kufikirika lakini muda
unapozidi kwenda ndio utatambua ukweli kuhusu maamuzi uliyo yachukua, na
ikumbukwe kuwa baadhi ya maamuzi yanaenda na muda ukisha amua neema
yakurekebisha inaweza isiwepo tena.
Ni muhimu kutambua kuwa kila ukiri unao ambatana na maamuzi una matokeo yake unapoamua jambo
uwe tayari gharama utakazo zibeba hivyo kila ukiri unaoufanya utoe muda mzuri
wa kujiandaa kwa gharama za matokeo yake.
Kila ukiri ujue una matokeo kwako na kwa mwingine hama jamii
husika na matokeo mazuri hama mabaya utegemea na vyanzo vya maamuzi vilivyo
pelekea ukiri, imekuwa ni rahisi sana mtu kudumu katika maamuzi ya ukiri yaliyo
jengwa na maumivu,hasira na husuda kuliko maamuzi yanayo ambatana kujenga kesho
yake mathalani maamuzi nakujiapiza kusema nitasoma neno la Mungu na kuliishi
kwa uaminifu na kwa gharama yoyote.
Katika yote hakikisha ukiri wako unakuwa na FAIDA KWA MUNGU
katika gharama yoyote haijarishi nafsi yako itakuwa na maumivu kiasi gani?
MUNGU ATAKUPA RAHA.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………..0764 018535