Jumanne, 2 Mei 2017

UHURU WA NAFSI



UHURU WA NAFSI


Moja ya vitu ambavyo binadamu anavyo vipenda katika utendaji wake ni kuwa huru!
Kuna kipindi kinafika pindi mtu anapokosa uhuru wake uwa chakula, pesa na mali vinakosa maana kwake…anaweza kujiona kama asiye na hadhi yoyote kwa maana haoni maana ya kuwa navyo maana anakosa uhuru wa nafsi ambao ndio msingi mkubwa wa maisha yake.

Natambua kuna uhuru wa aina nyingi mathalani uhuru wa akili yako! Uhuru wa mwili wako! Tukiachia mbali uhuru wanchi, na huku tukiwa na tafsiri fupi kuhusu neno UHURU kwa maana hali kufanya mambo pasipo na kuingiliwa/ hama shinikizo lolote la nje bali lililobebwa na utashi wa mtu/nchi husika. 

Twende mbele na kurudi kama kuna vitu bora ukiachana na uhai basi uhuru wa nafsi ni kitu bora maana hapo ndipo unaweza kuanza kuyafurahia maisha binafsi, na kudumu kwa mambo mengi unayo yafanya utegemea sana nafsi ilivyo kuwa huru.

Japokuwa sio kitu rahisi kufanya jambo lilibebwa na uhuru wa nafsi wakati wote kwakua nafsi inaweza kukutuma kufanya jambo ambalo ni kinyume utaratibu uliozoeleka na jamii husika, sasa wewe kwa kuogopa hilo ukawa unaumia tu kwa ndani.

Usitegemee pindi utakapo amua kufanya jambo linalo tokana na uhuru wa nafsi  yako watu wote watalipenda hama kuliunga mkono tambua kila mtu ana nafsi yake na yuko huru kufanya yale anayo yaona kuwa ni sawa machoni pake hivyo nawe tia bidii katika yako ili mradi tu yamebeba nia njema.
Mtu anaye heshimu uhuru na nafsi yake uwa haogopi itakuwaje? Gharama zake ni kubwa kiasi gani? Bali uamini atafanikisha tu na upenda kufanya jambo lake kwa ubora wake na sio bora limefanyika tu.

Hakuna shaka maumivu yanakuwa katika maeneo mengi mathalani ndoa kwasababu mtu ameingia sio kwa uhuru wa nafsi yako bali kwa ushawishi wanje yaani marafiki hama vitu vinavyoonekana na mwisho migogoro na mateso yakawa ndio maisha.

Kuna maumivu makali pindi utakapo fanya jambo nje ya uhuru wa nafsi yako na kisha matokeo ya kawa mabaya zaidi na kukuacha na msongo wa mawazo usio na mwisho.

Ni muhimu kutambua kila mtu alikuja akiwa na utashi wa nafsi yake hivyo huna haja kuangalia nani atafurahi hama kuchukia tambua kuwa wewe ndio mwenye dhamana ya maisha yako kuyajenga hama kuyabomoa siku zote watu usubiria matunda yakionekana mazuri mbona watakuheshimu na pindi yasipo onekana hata uliwafurahisha kiasi gani bado watakusema tu na kukukebei.

Iboreshe nafsi yako kuwa yenye maamuzi ya maana kwa wewe KUMJUA MUNGU ili ikupeleke katika maamuzi yakayo jenga hatima yako na sio kuiharibu.

Maisha yanaanza kuwa na maana pindi nafsi yako inapoanza kutembea katika uhuru wake!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni