Jumanne, 16 Mei 2017

UKIMTUMIKIA ATAKUTUNZA

UKIMTUMIKIA ATAKUTUNZA


Yohana 15:2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

Katika kitu ambacho Mungu ataona fahari juu yako ni KUMTUMIKA, maana gharama nyingi Mungu anaingia juu yako, yote ni kuhakikisha unakuwa huru katika kumtumikia yeye na zaidi sana unakua na kuongezeka katika utumishi wako juu yako.

Moja ya jambo la msingi sana unapoamu kuyatoa maisha yako ili kutumika kwa ajili ya Mungu tu yeye mwenyewe uku safisha hama kwa lugha rahisi ukufanya kuwa bora ili uzidi kutumika katika namna anavyotaka na ukupa neema yake kuhakikisha unatumika kwa furaha.

Katika jambo la kuzingatia pindi unapoamua kwa dhati katika utumishi wako mbele za Mungu tegemea kutunzwa na yeye tena kwa namna yake kwakua unapoamua kwa dhati kumtumikia nay eye ana amua kukustawisha katika njia zake.

Mathayo 6:26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

                    27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
                    28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

                     29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

                    30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

                    31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

                    32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

                   33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Moja neema ambayo Mungu anahiachilia pindi unapo amua kumtumikia Mungu ni hali ya kutoishia njiani wala kuchoka hama kukata tamaa, bali siku zote Mungu ukupa nguvu mpya ili uzidi kuleta faida katika ufalme wake,

Japo nakubaliana kutumika mbele za Mungu sio kitu rahisi ndomana wapo wanafanya kazi ya Mungu katika mafanikio na wengine wakibwaga manyanga( kukimbia huduma) kutokana na sababu mbalimbali lakini bado atabaki kuwa Mungu na kuzidi kutumikiwa katika viwango vyake.

Kutumika ni jambo jema hasa unapotumika katika hali ya kupenda na utayari maana utalifanya katika ufanisi na uhodari mkubwa hilo kusudi ulilopewa! 

Niseme tu, tatizo sio kutumika tu bali namna unavyo tumika mbele za Mungu ina maana kubwa lazima ujiulize mapenzi yako kwake yanaongezeka hama yana pungua…maana ni muhimu unapotumika kwa Mungu uone deni likiongezeka siku zote kwa ajili yake tu,

Ili uweze kumtumikia Mungu katika namna anavyotaka uwezi kujitenga na KUMJUA MUNGU! Kwakua hapo ndipo  panazaliwa utofauti aliye imara na asiye imara…kwakua unapo wekeza katika KUMJUA MUNGU, ndipo hapo uweza kuwa imara na kuona Mungu akikutunza zaidi ya kuona makucha ya shetani.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni