RAHA ISIYO
NA MIPAKA
Naomba
kuuliza hivi kunatofauti ya raha na furaha? Na furaha ndio inaleta raha hama
raha ndio inaleta furaha? Karibu sana tutafakari pamoja!
Furaha
na raha ni vitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwa ujumla wake na hasa katika upande wa afya
na hata kufanya ngozi yako kukunjuka na kunawiri a.k.a kuwa na mvuto,
Katika
ulimwengu wa kila mtu utafuta kufanya jambo litakalo mpa raha na wala sio mzigo
wala mateso katika mawazo yake, yanaweza kuwa kusoma, kufanya kazi hama kuoa au
kuolewa na mengine mengi lakini ukweli katika kutimiza lengo lako mwisho kunaweza kuwa raha hama
majuto pamoja na hayo lakini bado maisha yanaendelea.
Wako
watu wanajitahidi kulinda furaha zao, wako na wengine wanatafuta kuwa na furaha
na wengine wamechagua kuishi maisha yasiyo na furaha zaidi ya kuridhika tu, na
kuona ili mradi miaka inaenda basi hakuna cha maana zaidi ya pumzi anayoitumia.
Niseme
kuishi katika vita kali na bado ukawa raha ndani yako japo ina aminika mahali
penye vita hapo hapana raha kwa sababu hakuna utulivu….Niseme tu panapo kuwa na
vita sio wote wanakuwa hawana raha bali uko upande japokuwa unapambana unajua
utashinda tu kutokana na uwezo mkubwa walionao dhidi ya adui yao,
Tatizo
ya furaha hauwezi kununua japo kuna uwezekano kujifanya kuwa na furaha kana
kwamba umeajiriwa katika kitengo cha mapokezi hivyo wakati wote inabidi
uonyeshe tabasamu haijalishi unayo furaha hama hauna ili mradi mwisho wa mwezi paeleweke
na zaidi sana ili kibarua kisiote nyasi.
Upaswi
kuwa furaha kwakua uko kazini hama kwasababu ya kutunza afya yako bali
kwasababu ulikusudiwa kuwa furaha na raha tangu ujatoka tumboni mwa mama yako
na ulikusudiwa kuwa uishi maisha ya furaha kwa maana ni haki yako,
Mungu
anatazamia uwe na furaha wakati wote haijalishi uko katika hali gani na maana
Mungu ni zaidi ya baba kwa kuwa yeye anaijua kesho yako ambalo ni fumbo la
wanadamu wengi,
Ili
uwe na raha isiyo na mipaka kuna mambo ya kutambua;
i.uelewa sahihi kuhusu furaha
wako
watu wana amini wasipo kuwa na furaha katika jambo linalo watatiza wana amini
watakapo sikiliza muziki wa aina Fulani basi hapo furaha itarejea, wengine wana
amini wakienda disko watachangamka, wengine wana amini wakienda beach watapata
pumziko la akili na njia nyingine nyingi.
Ni
muhimu kutambua lolote unalopitia si kigezo cha kuondoa furaha yako na tambua
funguo ya kuruhusu huzuni ingie na raha iondoke iko katika himaya yako…
Ni
kweli unaweza sema ni gumu lakini wewe si wa kwanza, lazima utambue kuwa kila
jambo linakusudi lake lakini sio kuondoa furaha ndani yako.
ii.uwezesho Mungu katika kutunza
furaha ndani yako
wataalamu
(wanasaikolojia,washauri) wanapo shindwa kuona njia nyingine ya kukuwezesha
kuwa na furaha ndipo hapo Mungu ujidhihirisha kuwa yeye yuko juu ya vyote na
hakuna kinacho mshinda,
Ni
muhimu kutambua mambo mengi yanayo tukabili wakati mwingine uonekana ni mazito
lakini katika uwezesho wake furaha na raha itazidi kutawala mioyoni mwetu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni