SURA YANGU
Moja ya kitu kinacho dhihirisha huyu mtu anajipenda ni
muonekano wake!
Na kitu kimoja wapo kinachozingatiwa sana katika muonekano ni
sura hama kwa jina jingine uweza kuitwa RECEIPTION (Mapokezi), ni seme swala la
muonekano mzuri uwa alina jinsia wanaume au wanawake wote upenda kuwa na
muonekano mzuri na zaidi unao vutia.
Na ni rahisi mtu akasahau kusafisha miguu yake kuliko sura
yake, kwa maana sio rahisi kukuta mtu amewekeza sana kufanya miguu yake ing’ae
na kuacha sura yake ifubae na huku ana amani zote na pengine aseme “nafanya hivi kwasababu mimi naipenda sana
miguu yangu kuliko sura yangu” na huku ana uwezo wa kufanya vyote.
Ila kwa kiasi kikubwa unaweza kukuta mtu anapenda sura yake,
miguu yake pamoja na ngozi yake ili kukamilisha muonekano mzuri ulio kivutio
kwa wengi na kuwa faraja kwake! Na muonekano wa mtu utegemea uchumi wa mtu, na
aina ya ngozi aliyonayo ( maana kuna baadhi ya ngozi hata utumie mafuta,
matunda uongeze na mazoezi bado haibadiliki).
Mbali na hayo pia sura ya mtu utumika kutambua hisia za mtu,
kwaku mwangalia pana uwezekano wa kutambua hali ya mtu kama amekasirika hama
anafuraha au anacho ongea ana kimaanisha hama feki na wengine wana neema zaidi
pindi wanapo mwangalia mtu uweza kutambua kuwa huyu amekula hama ajala japo
anaweza asimsaidie hiyo hela ya kula,
Pia muonekano wa mtu ukihusishwa na sura uweza kutambua
chimbuko la mtu/ asili ya mtu husika aliko tokea na wengine kwaku mwangalia
sura yake uweza kukadilia miaka ya mtu husika………SURA YANGU!
Katika hali ya kawaida jambo baya linapo mpata mtu utoshangaa
maneno haya aki yasema…..nitaiweka wapi
sura yangu! Inawezekana amefanya yeye hama limetokea miongoni mwa familia
yake mathalani mwanae aliyekuwa anajivunia kwamba anapenda shule matokeo yake
ya mtihani kapata daraja ziro (0)
Kikawaida jambo lolote zuri unapolifanya utapenda watu walijue
na hapo utatembea kifua mbele alikadhalika jambo baya linapokutokea hutapenda
lijulikane na watu wengi, na muda mwingi hutapenda uonekane na watu. Japo
wakati mwingine unashindwa kutambua unaweza ukajifunza kupitia kukosea na sio kujilaumu na mwisho
kukata tamaa.
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………0764 018535