Jumanne, 6 Juni 2017

NITAIJUA BAADAE!

NITAIJUA BAADAE


Hakuna kitu kizuri kama kujua! Japo uzuri wa kujua unakamilika pale unapo jua na matokeo yake unapoyaona!

Kila mtu utamani kuwa na kesho nzuri lakini shida inakuja pale namna ya kuifikia hiyo kesho iliyo ndoto yako( iliyo beba kiu na shauku ya moyo wako)……… unaweza kukuta mwanafunzi alikuwa ana mipango yake labda baadae awe rubani, wakili, engineer, muhasibu, mwalimu na hata taaluma nyingine lakini mchakato  wake unaweza kubadilisha hiyo ndoto yake kutokana na matokeo ya kidato cha nne au cha sita kutokidhi vigezo vya kumwezesha kusoma masomo Fulani au taaluma aliyokusudia hama maamuzi binafsi, ukakuta muhasibu akawa mwalimu hama mwalimu akawa muhasibu,

Naam imekuwa ni rahisi kwa mtu kunung’unika, kughairi, kukasirika kwa jambo analolitegemea kushindwa kufanyika kwa muda alio upanga au namna alivyotaka mathalani unaweza kukuta mtu anaweza kujisikia vibaya kwa kuachwa na ndege na pindi akiwa kituoni analia na kusikitika pamoja na kumlaumu mtu anayedhani aliyesababisha hayo yatokee lakini ghafla akasikia ripoti kuwa ile ndege imelipuka…. Bila shaka ataondoka taratibu na kwenda sehemu ya mapumziko huku akimshukuru Mungu…..NITAIJUA BAADAE!

Wako watu wamegombana na kupelekea hata kuachana na wazazi wao, marafiki zao haya yote yanawezekana ni baada ya kutoa majibu binafsi katika kila tendo analofanyiwa hama analo hisi anafanyiwa na pindi ikatokea kuwa tofauti na uhalisia wa mawazo yake baadae ikapelekea majuto ya kudumu.

 Japo ni muhimu kutambua jambo kwanini hili limekuwa hivi au limekuwa vile lakini sio lazima kujisumbua sana ili mradi ujue tu! Unaweza kukuta mtu anasema kila jambo linalo nitokea uwa sili, silali mpaka nijue kinaga ubaga lakini yako mengi unahitaji ukubali tu kuwa UTAIJUA BAADAE SABABU YAKUTOKEA KWAKE.

Upaswi kukosa raha kwa jambo ambalo alina utatuzi uliobora au wenye tija katika ufalme wa Mungu maana huyo ndio ustawi katika maisha yako, 

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Kuwa na wasiwasi kama hatima yako imeshikwa na watu wengine lakini kama iko mikononi mwa Mungu huna  haja ya kujitetea zaidi wewe simama katika nafasi yako, japo kuwa yako mengine yataonekana ni magumu kunyamaza kimya tambua kuyaruhusu yachanganye akili yako kunaweza kupelekea kuharibu hatima yako.

Kuongea sana akupelekei usalama wako kuwa mkubwa bali ufumbuzi sahihi upelekea usalama wako wan je na hata wa ndani kuwa wakutosha na kufanya uzidi kuwa bora katika utatuzi wako katika yote yaliyopo na yatakayo kuja.

INAITWA SIKU!BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni