UNAWEZA
Katika maneno ambayo watu wengi upenda kusikia wakiambiwa
mojawapo ni hili neno, na unaweza kuona tabasamu na changamko katika sura ya
mtu pindi anaposikia neno…UNAWEZA,
Unaweza kufanya misuli na mishipa iliyo kuwa katika hali ya
kusinyaa ikawa imara, unaweza kukatisha kisima cha machozi katika macho,
unaweza kufungua mlango wa moyo wa mtu uliofungwa kwa muda mwingi naam unaweza
kurejesha usingizi wa mtu uliotaka kupotea, unaweza fanya mtu aliyefunga mlango
kwa hofu kubwa ndani yake lakini ukakuta anafungua mlango na kutoka nje kwa
ujasiri pindi atakaposikia sauti ikimwambia……..UNAWEZA!
Hili neno UNAWEZA linaweza
kukosa umuhimu wake kwa wakati fulani ila kuna wakati utaona fahari yake
kuliko chochote, hii naweza fananisha na mtu anapokuwa mzima uwa haoni umuhimu
wa dawa hivyo anaweza pita katika duka la madawa na kuona kama aina fulani ya
duka linalo uza bidhaa fulani zisizo na tija kwake, lakini pindi ikatokea
unaumwa ukapewa orodha ya dawa kwa ajili ya afya yake hapo ndipo utakapoona duka la dawa kama lulu
unayo hitaji isivyo kawaida……….hivyo kila neno lina majira/wakati wake ili
kudhihirisha umaana wake!
Usijiwekee mipaka katika utendaji wako ila la msingi ujue
jambo limekuja kwako kwa namna yake jua hilo jambo limejipima na likaona
linatosha kuja kwako, likabili linaweza kukuvusha na kukupeleka katika hatua ya
kuweza zaidi.
Ukijiwekea mipaka katika kuweza itakujengea hofu na hatimaye
kushindwa kujifunza zaidi na mwishowe kujiona kutoweza ndio maisha yako.
UNAWEZA linapaswa kuwa
ni neno linalo tawala moyo wako ili kudhihirisha imani yako kwa Mungu ili naye
aone utayari wako na kuonyesha ukuu wake!
Katika biblia kuna mtu mmoja ninge penda tumwangalie anaitwa
DAUDI, karibu……………………….
1
Samweli 17: 45 Ndipo
Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na
mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi
ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na
kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi
mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu
katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa
upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi
mwetu.
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi,
ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule
Mfilisti.
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja,
akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo
likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga
Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa
upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao
Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.
Ni vizuri sana kuambiwa kuwa unaweza lakini ni vizuri zaidi
kujiona unaweza kama daudi alivyojiona anaweza japokuwa alikutana na vipingamizi vingi lakini
namna alivyojiona kuwa “ninaweza kuleta heshima katika Israeli” akuweza
kuruhusu ile namna anavyojiona ipotee kwasababu ya watu waliopinga mtazamo wake.
ANAITWA MUNGU!
BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………..0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni