MASIKIO YA WENGI
Siku zote nguvu ya mtu ya kusema inakuwa pale utakapoona
mtu/watu wanakusikia na wakati mwingine umakini wao unaweza kukushawishi kusema
zaidi,
Uwa inakosa maana zaidi pale utakapo tumia nguvu kubwa
kuongea, wakati hakuna anaye kusikiliza kwa jina jepesi wanaweza kukuita chizi
kama hautakuwa unafanya mazoezi ya kuimba hama maigizo. (kwa maana rahisi raha
ya kusema ni kusikilizwa)
Maana ya kuwa na sikio ni kusikia, japo unapoona sikio sio
lazima huyo mtu awe anasikia kwani anaweza kuwa kiziwi lakini akakuangalia kana
kwamba anasikia lakini sivyo!
Katika dunia imekuwa ni fahari ya mtu kusema na watu wengi!
Imefika kipindi cha mtu kupata heshima kutokana na watu anaozungumza nao kama
ni watu wachache au wengi heshima yake itabebwa sawa na watu anao waongoza,
japo sina uhakika kama ni sawa!
Imekuwa ni changamoto kwa watu kutaka kuongea katika idadi
kubwa ya watu na sio kwa maana ya kuwasaidia bali kutaka heshima au umaarufu,
na amini ni mwalimu tu anapenda wanafunzi wachache ili aweze kuwa mudu vizuri
na sio wengi ikawa shida kuwa mudu.
Imefikia kipindi kujua mahali penye watu wengi basi hapo ndio
penye ubora, mathalani katika kikombe cha babu watu wengi walienda uko
wakijiamini kuwa ndio suruhu ya matatizo yao! Lakini ukweli anaujua mwenyewe
baada ya kunywa kikombe cha babu na kuona matokeo yake,
Hii imeenda mbali kidogo watu wengi upenda kuwa na mtu
anayejulikana sana hama kusikilizwa na watu wengi wakiwa wana amini kuwa ukikaa na waridi basi nawe
utanukia. Japo ni ukweli kila mtu upenda kusikilizwa.
Upaswi kushangaa pindi mtu anapotaka kuchukua maamuzi fulani
uwa ni lazima atafute maoni ya watu kuona hichi kitu ninachotaka kukifanya kuwa
ni sahihi au la! Niseme tu jambo hili linakuwa la maana sana kama maamuzi
yanayo husu kundi la watu lakini sio muhimu sana kutafuta ushahidi wa watu
wengi katika jambo linalohusu ubinafsi wako linaweza kukugharimu ukaanza
kutafuta nani wa kumlaumu.
MASIKIO YA WENGI! Imeathiri sana katika utendaji wa wengi;
Watu wamekuwa wakitumia nguvu kubwa ili mradi watu waendelee
kumsikiliza kuliko kuwapatia ufumbuzi sahihi na wenye tija katika maisha yao,
Siku zote utakosa mwelekeo ulio sahihi kwakua wako watu
watakuvutia huku na kule, wengine watapenda hiki na wengine watapenda kile kama
utakuwa pale ili waendelee kukusikiliza utakosa kujua nini nifanye ili wote
wafurahi maana utaki kuwapoteza.
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni