Moja ya bidhaa inayopendwa na watu wote haijalishi ni tajiri au maskini ni MAJI kwani kiu hainaga mbadala kwakuwa hauwezi kula chispi badala ya maji wakati unakiu ya maji na pengine ukiulizwa kwanini unafanya hivyo useme ” mimi ni tajiri” unaweza fanya magazeti wapate habari ya kuandika.
Na unaweza kugundua kumbe sote maji ni muhimu kwetu pale maji yanapo kosekana kwa muda utakuta jamii yote wimbo ni moja “ natafuta maji”………. Unaweza kushangaa tajiri akimsalimia maskini kwa heshima zote “ ndugu habari yako” pindi anapo hisi kupitia huyu hitaji lake la maji litapatiwa ufumbuzi, na unaweza usishangie jamii yote ikakusanyika sehemu moja bila kujali hadhi zao na wote wakihitaji maji.
Na amini siku zote uhitaji ndio uzalisha kiu ya kutafuta, kwa maana nyepesi kama hakuna uhitaji basi hakuna maana ya kutafuta ( maana uwezi kutafuta kitu ambacho hauna uhitaji nacho).
Bidii au kujigharimu sana katika kutafuta kitu udhihirisha thamani ya hicho kitu / umuhimu wake, mathalani uwezi kumkuta mtu mzima anakesha usiku kucha na ukimwangalia unamuona hana raha kabisa na ukimuuliza kwanini uko hivyo akakujibu “ sh. 10 yangu nimeipoteza toka jana naitafuta bado sijaipata” unaweza kushikwa na bumbuwazi na kuzidi/ kuzalisha maswali kichwani mwako kuliko majibu! Lakini ikatokea akasema ” nimekesha usiku kucha kumtafuta mwanangu sijampata mpaka sasa” unaweza kujua kuwa hiyo ni kawaida ya wanadamu na hasa mzazi/mlezi mwenye mapenzi ya dhati kwa mwanae.
Japo maji ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, yakiwepo unaweza usione huo umuhimu wake lakini yatakapoanza kukosekana hapo ndipo utaanza kuona watu wakianza kuumiza kichwa jinsi gani wanaweza kupata maji ya kutosha ili kukidhi mahitaji yao.
Mng’ao wa kitu utegemea sana uhitaji wake! Kitu hata kikiwa na mng’ao gani kama akita tafutwa /hitajika basi jua huo mng’ao utafifia tu.
Pia inawezeka kuna kitu mwanzoni ukikipa thamani kwasababu yakutojua matumizi yake ukakipotezea, lakini pindi utakapojua jinsi kinavyoweza kukidhi uhitaji ulionao taratibu utaanza kukipa thamani ndani ya moyo wako.
Popote ulipo uhitaji wako utakapoanza kuongezeka utaanza kukumbatiwa na ikatokea uhitaji wako kuanza kupungua basi hapo utaanza kuona uhuru wako unaanza kuongezeka basi ni muhimu ujue hiyo ni ishara mbaya mathalani umechelewa kazini bosi akuulizi, umefanya kazi vibaya haulizwi wala hausemwi, uko nyumbani umezidisha chumvi kwenye mboga wanakuangalia, umeunguza chakula kila mtu ajali ni muhimu utafakari kwanini hivi?
Pindi utakapoamua kuwa hitaji la wengi ndipo hapo neema ya Mungu itazidi kukutawala na ongezeko lake ndani yako litakuwa kubwa na kukupa wepesi katika utendaji wako.
Kuwa sehemu yenye staha na viwango vya ajabu kama ukatambua ahutajiki mahali hapo inakuwa na sawa na nzi kuwa katika jagi la maziwa, na uzuri watu wanao uona wewe unaona giza tu, na pengine unaweza kujuta kwanini uko hapo? Ni bora usingeli kuwepo.
Uhitaji mzuri ni pale utakapo jitambua mwenyewe kuwa mimi ndio hitaji la mahali hapa na kuanza kuwajibika kuliko watu kutambua uhitaji wako alafu wewe usijitambue unaweza kuzaa maumivu kwa watu.
Mwendelezo wa uhitaji wako haupimwi na mtu yeyote bali unapimwa na yule aliyekufanya kuwa hitaji sehemu husika, maana pana uwezekano wa kujisikia upo chini pindi watu wakapoanza kupima uwajibikaji wako.
Unapotambua kuwa wewe ni hitaji la watu hawa hama mahali hapa basi ujue Mungu amekuheshimu na kukupa neema yake huna haja ya majivuno bali ni muhimu kuzingatia kuwa hao watu ni hitaji kwako pia ( mnahitajiana).
Ni jukumu lako kuhakikisha kuwa uhitaji wako unazidi na sio kupungua!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535