Tarajio la wengi ni kupata kitu anachokita/kukipenda na wakati mwingine subira ya kitu inakuwa na maana pale unapokuwa na uhakika wa kukipata kile kitu unachokitaka.
Thamani ya kitu chochote inapanda au kushuka sio kwasababu umepata tu bali ni kwakua umepata kitu kilichobeba tazamio lako ambapo ukitazama hicho unakumbuka jitihada zako juu ya kitu na hapo tulizo la moyo utokea na furaha ya mbali toka moyo uanza ( tabasamu la moyo sio la sura).
Njia rahisi ya kupata kitu chochote ni muhimu kujua kinapatikanaje? Endapo utashindwa kujua kinapatikaje jitihada zako zitakuwa ni bure! Itakuwa sawa unamtafuta mamba katika bahari uku ukijipa matumaini utamuona akifurahia maji ya chumvi.
Najua sio jambo rahisi mtu akwambie yeye namna anavyopatika ( ratiba yake & mahali anapoishi) hata kama anakujua sana moja sababu yake ni kutoona umuhimu wa wewe kukwambia ubinafsi wake na sababu nyingine ni usalama wake, itakuwa rahisi kuongea yote yaliyo moyoni mwake kama tu utakuwa na nafasi ndani yake na moyo wake umeridhia…………………………..!
Karibu katika ujumbe wa leo………………………………………………………………..!
Kama kuna vitu bora katika maisha ya mwanadamu ni KUMTAKA MUNGUmaana yeye pekee anaweza kuirekebisha jana na kuiandaa kesho yako.
Uzuri wa kumpata Mungu hakuna siri ni wewe kudhamiria tu, hata kama umemuona mtu amejaa Mungu kwa kiasi cha kutisha ukimfuata na kumuuliza kama ni mkweli atakwambia vitu ambavyo ukimsiliza unaweza usiamini kwa urahisi.
Hata ikatokea usivutiwe na mtu yeyote ukionyesha kiu Mungu atakuja akujaze! Maana yeye ni furaha yake umpate yeye kamili, ni muhimu kutambua pindi utakapo amua kumtaka Mungu hauhitaji kwenda kwenye hatua za mtu au kundi la watu hama mtu/watu unao waamini.
Mnapokuwa sirini wewe na yeye atajifunua vizuri nawe utamwelewa vizuri utahitajika kuishi katika fahari yake ukizifuata hatua zake ( kutii neno lake).
Hauhitaji kupata msukumo wanje ukupelekee kumtaka maana huo ukiisha au kubadilika utakusumbua sana katika safari yako ya wokovu, bali ni muhimu umtake Mungu kwasababu maisha yako yanakamilishwa hama yanakuwa na maana pale utakapo mpata Mungu na kuruhusu akuongoze katika hatua zako.
Na ni muhimu kutambua furaha na raha ya kweli haipatikani kwasababu una nyumba, mke/mme, gari na thamani yoyote iliyo duniani maana kuna siku vitaondolewa hama utaviacha lakini Mungu utakuwa naye siku zote hadi umilele.
Kumtaka Mungu ni ishara kubwa ya kuyapenda maisha yako!
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………….. 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni