Unaweza kukuta mtu ameinamisha kichwa chini na machozi yakimtoka hama kumlengalenga nawe ulipo muona ukaingiwa na huruma na maneno kuanza kutoka kinywani mwako uku ukitafuta namna gani ya kumrudishia raha/furaha yake……… unaweza jikuta unaongea mpaka mate yanaanza kukauka lakini ya mtu haibadiliki na hali aliyonayo lakini ghafla likatoka neno kinywani mwako lililo unganika na jambo lililopelekea kukatika kwa maji machoni (machozi) hapo ndipo unaweza kukuta anaanza kuinua kichwa chake kukutazama kwa macho yake yaliyojaa maji ya mwili.
Na ni kawaida pindi unapotaka kuuangusha mti katika ukubwa wowote ni lazima uende kwenye kiunganishi kilichopo kati ya mti na ardhi kwa lugha rahisi ni mzizi, kinacho safirisha maji kutoka kwenye ardhi na kuelekea kwenye shina hatimaye kusambaza katika mti mzima na pindi unapofanikiwa kukata muunganiko huo huna haja tena ya kuwa na wasiwasi ujue tu mti utadondoka.
Huna haja kukesha usiku kucha kutafuta m baya wako ni nani? Ni muhimu kutambua kile ulichounganishwa ndicho kinachokutengeneza, hivyo huna haja ya kusumbuka na muonekano wan je bali angalia kilicho ung anika nawe na kukutengeneza vile ulivyo.
Wakati mwingine unaweza kushangaa kwanini huyu anafanya vizuri na huyu afanyi vizuri, unapoamua kutafuta sababu ipi ikapelekea utofauti wao ni muhimu uangalie muunganiko wa kila mtu hii inaweza kuwa ni hatua bora sana katika kupata jibu lililo sahihi kuliko kukaa na kuponda hama kukosoa tu.
Wazazi wengi wanapata tabu sana juu ya watoto wao na kuishia kutoa maneno makali pamoja na kuwapiga sana pasipo kutafuta nini watoto hawa wameungamanishwa nacho kinacho wafanya wawe hivyo, maana ni wazi usipojua nini kimeungamanisha mpaka kinapelekea mtu huyu kuwa hivi, unaweza ukashinda usiku mzima na hata miaka bila kupata suluhisho lolote ingawa unaweza kujipa matumaini kuwa labda kesho mambo yatakuwa sawa.
Kwa mtu aliyejiungamanisha na kitu sahihi ni ngumu kumuondoa hapo hata ufanyeje/ iweje atabaki kuwa salama tu maana ule muungamaniko utamnawilisha na kupingana nae ni sawa na kukata matawi katika mti ukitegemea huo ndio mwisho wa mti pasipo kujua shina na mizizi ikiwa salama basi ujue mti uko salama kwa wakati wake utachipuka tu.
Huna haja ya kulaumu/ kujilaumu maisha yako bali angalia sana ni nini ulichoungamanika nacho je! Kinaleta uzima au mauti katika maisha yako.
Unapokuwa makini na kile ulichoungamanika nacho basi hiyo ni ishara nzuri ya kujali ustawi wako kwa kuwa hauwezi kustawi inje ya kile ya kile ulichoungamanishwa nacho.
Swala sio kuungamanishwa tu bali unaungamanishwa na nini? Na hicho kitu kinaleta matokeo gani? Na je! Hayo matokeo yatadumu kwa muda gani? Na mwisho wa siku yatakuweka katika hali gani?
INAITWA SIKU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………… 0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni