Jumanne, 10 Oktoba 2017

SAUTI YAKE NDIO NGUVU YANGU.






Tafsiri fupi ya neno nguvu ni uwezo wa kufanya jambo, na mafanikio ya jambo udhihirisha nguvu ulizo nazo…………………………………………………………………!

Sauti, kuna aina ya sauti zilizo ambatana na maneno fulani na pindi unapo yasikia uweza kubadili hali yako nzima ya mwili, unaweza kuta mtu anaacha kula, kuaghirisha safari zake, kuvunjika kwa baadhi ya ratiba zao na wengine uweza kuzalisha furaha hama maumivu kutokana na sauti iliyoambatana na maneno yaliyotoka katika kinywa cha mtu.

Naam kwa asilimia kubwa watu hisia zao (furaha/huzuni) utegemea maneno ya mtu mwingine. 

Unaweza kukuta mtu anasema siku yangu leo ilikua nzuri sana maana nimeyasikia maneno niliyokuwa na yatamani/ nayasubiri kwa muda mrefu nayo yamegusa hisia zangu na kuchangamsha moyo wangu na inaweza kuwa kinyume chake kwa mtu aliyesikia maneno magumu/ asiyo yapenda hama kuyatarajia.

Japo kuwa nguvu ya maneno unayoyasikia kwa kiasi kikubwa utegemea ufahamu wa wako, maneno ni yaleyale yanaweza kusemwa kwenye kundi lakini matokeo yake yakawa tofauti kwa kila mmoja kulingana na hali aliyonayo (hisia); inawezekana huyu akachukizwa sana na mwingine akajifunza kitu.

Na ikumbukwe kuwa unapokuwa binadamu hali ya kutawaliwa na hisia ni jambo la kawaida.

Karibu!

Sauti yake ndiyo nguvu yangu!!!

Unapokuwa duniani kusikia sauti nyingi ni swala lisiloweza kukwepeka lakini nguvu ya sauti utegemea ruhusa ya ufahamu wako/ udhaifu wa akili yako.

Ni muhimu uone/ utamani kuwa nguvu yako ya utendaji ibebwe katika kusikia sauti ya Mungu, kwani;

i.                    Ni sauti pekee yenye kumaanisha kile kinachosemwa

ii.                  Ni sauti iliyobeba dhamira njema na ya dhati

iii.                Ni sauti pekee isiyo na pande mbili (kigeugeu)

iv.                 Ni sauti pekee iliyo kukusudia kukufanya kuwa bora/ wa maana

v.                   Ni sauti yenye kukufikisha kwenye hatma yako iliyo njema.

vi.                 Ni sauti pekee ambayo ukiifuata hauta kaa ujute.

-          Maana unahitaji kufuata njia unayoelekezwa na sio unayoifahamu

Kama una nia ya dhati ya kupata usalama katika maisha yako basi ni muhimu ujenge urafiki na sauti hii, na unaielewa sauti hii kupitia neno la Mungu pekee hivyo ni lazima ulipende na kulipa nafasi katika maisha yako.

Matukio na simulizi za watu zenye kutia moyo na kuamasisha uwa sio msingi mzuri katika utendaji wako katika ufalme wa Mungu. Bali jenga sana ushirika mzuri na sauti hii maana wote walioifuata walijivunia maisha yao.

Japo wakati mwingi kuifuata sauti hii ni kwenda kinyume na mazingira yanayoonekana katika ulimwengu dhahiri, lakini hauna budi kuifuata maana ubora na ushindi uzaliwa hapo.

Unahitaji uwe halisi kwa Mungu na sio kutaka sifa kwa watu ambao wanakuwa na wewe kwa muda mchache na mwingi unakuwa peke yako.

Moja ya sauti ambayo haupaswi kuipotezea ni hii maana ukiipotezea itakugharimu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni