Ijumaa, 24 Julai 2026

KOSA LANGU

 



Hatia yoyote katika maisha ya mtu ni matokeo ya makosa aliyoyafanya kwa kujua au kutokujua.

Na kila kosa lina ishi na madhara yake haijalishi ni madogo au makubwa!

Na baada ya kufanya kosa kinachoendelea kukutesa sio kosa tena bali ni hile hatia ( madhara ) inayo tawala nafsi yako.

Na hatia inapokuwa ndani yako inapelekea kujihukumu na kujiweka mahali pa makosa.

Ni muhimu utambue kuwa maisha ya hatia yanakupa maisha yake na sio maisha yako utaanza kuishi sawa na hatia itakavyo kuongoza na sio kama unavyoona au unavyotaka.

Moja ya matokeo ya hatia ujasiri upotea kama sio kupungua, ukweli inawezekana hilo kosa hakuna aliyekuona lakini nafsi yako inapoaza kukuhukumu hapo uzito katika utendaji uanza kuchukua nafasi katika moyo wako.

Bila shaka katika dunia ya leo moja ya tatizo linalosumbua katika maisha ya watu ni hatia iliyo ndani ya maisha ya mtu inayomtawala na kuyaendesha maisha yake.

Hali hii isipofanyiwa utatuzi wa haraka unaweza kupelekea mtu kuwa na tatizo la akili. ( afya ya akili )

Zipo hatia zinazozalishwa na vitu mbalimbali mathalani, mikopo iliyoshindwa kulipwa na kupelekea kupoteza mali zake alizo chuma kwa tabu inawezekana ni mashamba,  nyumba au ofisi.

Maswali mengi yanakuwa hivi kwanini nilikopa na kwanini nimeshindwa kurudisha mkopo wa watu? Unaweza kuwaza siku nzima na bado ukakosa jibu sahihi.

Pia ziko hatia zinazozaliwa katika mahusiano hasa mahusiano ya ndoa , zipo ndoa zilizo dumu mwezi mmoja tu na baada ya hapo majuto na kujilaumu imekuwa ndio maisha ya kawaida na kusema kwanini nilikubali kuolewa na huyu na sio yule na mwingine anaweza juta kwa kusema sijui nini kilicho nifanya nimuoe huyu maana kama sio huyu nisingekuwa katika dimbwi hili lenye kina kisichokuwa na mwisho.

Mara nyingi maamuzi mengi yanayozaliwa na moyo uliojaa hatia na maumivu makali pamoja na majuto uweza kupelekea hata kifo.

Pia ziko hatia zinazotokana na watu wakaribu ( maraiki au ndugu ) pindi unapo msaidia katika jambo fulani kisha naye anakugeuka mathalani ulipambana kumtafutia nafasi hapo ofisini kwenu baada ya kupata kazi unakuta yeye ndiye anatengeneza mpango wa wewe kufukuzwa kazi, hali hiyo inaweza kuzalisha maumivu na uchungu usio isha.

Unapaswa kujua hatia haipo kwa ajili ya kukutesa bali ni kama alama unayokaa kwa kusudi maalum.

Hatia isikufanye kuona mambo sasa hayawezekani kana kwamba maji yame mwagika hivyo hauwezi kuyazoa tena.

Unapaswa kujua hatia ni msingi mzuri wa kufanya jambo ulilolifanya na kulitenda likutengenezee uwanja wa kuwa bora kesho kuliko leo.

Haupaswi kuruhusu hatia ikupelekee kuishi maisha ya hofu au ya mateso hali hiyo utakuwa umeruhusu mwenyewe lakini hilo sio lengo la kufanya ujisikie hatia.

Maisha mapya yapo tayari kuzaliwa katika hali hiyo ya hatia na sio kuharibu maisha yako uone kwamba umefika mwisho.

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

 

Imeandaliwa na:

 

Cothey  Nelson………………………………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni