Hakuna kitu muhimu kwa mtu kama maisha yake binafsi.
Kwa kuwa jukumu la maisha ni jukumu la mtu binafsi, hivyo kila mtu ushughulika sana kufanya maisha yake ya leo yawe bora kesho.
Hivyo sio jambo la kushangaza kuona mtu akipambana kuhakikisha maisha yake yanakuwa salama.
Japo kuna wakati tunajisahau kuwa hayo maisha unayoishi kuna MUNGU amekupa uyaishi na yeye akitaka usiendelee kuishi hakuna atakayezuia kusudi/ mpango wake labda atake mwenyewe katika mapenzi yake.
Ni kweli unayo nafasi ya kuwaza vizuri na mipango thabiti juu ya maisha yako lakini kukamilisha hayo vizuri, mbali na jitihada zako pia kuna hitaji neema ya Mungu ili kukupa kibali cha wewe kuyafikia yale uliyopaswa kuwa nayo.
Lakini Mungu anatambua unahitaji akupe maisha yake ili uishi maana katika maisha yako tu huwezi kujua mwelekeo unapaswa kuelekea.
Kuwa na mchakato wa kuyatengeneza maisha yako ukweli ni jukumu lako ili usiwe na lawama juu ya watu wengine wasio husika na maisha yako bali ni muhimu utambue kuna nafasi ya Mungu katika kukupatia mema ili uweze kuyakamilisha yale unayopaswa kuyafanya.
Karibu!
“ Yaache maisha yako akupe maisha yake”
Sio wakati wote yale unayoyawaza na kuyafikiria mchana na usiku juu ya maisha yako yanaweza kuwa na taswira sahihi ya wewe ulipaswa kuyaishi.
“ Maisha yake” ni yale maisha ambao ulitengenezwa kuwa ( original yake ) yeye anajua kwanini upo.
Unaporudi kwenye asili yako na Mungu anarudisha mema yake juu yako ili kukutambulisha katika nafasi yako katika utukufu wake wa ajabu.
Maisha hayabebwi na vitu vinavyoonekana kwa macho kuwa vinapendeza na vinavyovutia bali yamebeba vitu visivyoonekana vilivyowekwa ndani yako hivi vitu vikiwa hai na kukuta uhai wa mwili unakuwa katika hali yake njema yaani ndani ya asili yake.
Unaweza ukatengeneza gari na ukaweka kifaa au kubadilisha kifaa kibovu na kuweka kizima na kweli gari linaweza kwenda lakini mwendo wake unaweza usiwe sawa kama kukiweka kifaa halisi ambacho kilitakiwa kuwa hapo maana gari linarudi katika asili yake.
Unahitaji kumjua Mungu ili usiweze kupingana na Mungu pale anapotaka kukurudisha katika asili yako, kuwa mnyenyekevu na utaona matokeo yake.
Ni kweli mtu unaweza kuishi katika asili yake katika mazingira yasiyo sawa mathalani: mwandishi, mchungaji n.k ukafanya jambo nje ya neema ya Mungu ( tofauti na asili yako ) sawa na unachokiona kwa macho yako pasipo kuangalia mwenye asili yake aliyoyaweka ndani yako kama anakufurahia.
INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni