Jumamosi, 6 Aprili 2019

LIACHE KUSUDI LIVUTE MAMBO YAKE:



Ni jambo la fahari kwa mtu pindi anapofanya jambo akatambua kwanini anafanya hivyo au jambo hilo! Na litakuwa ni jambo la kushangaza kwa mtu awe anatia bidii sana na uku asijue kwanini anafanya hivyo.

Ni ukweli usiopingika pindi utakapoamua kulitumikia kusudi basi haki inayoambatana na hilo kusudi udhihirika au uweza kulipata.

Na ni jambo linakuwa gumu pindi utakapoanza kulitumikia kusudi uku ukiwa na matarajio yako ambayo ayaletwi na kusudi mathalani mtu unaweza ukajikuta katika shughuli za uvuvi lakini itakuwa ngumu kama moja ya kusudi lako ni kuvua swala mkubwa badala ya samaki.

Unapolitumikia kusudi uku akili yako ina mtazamo wako mbali na kusudi lilivyo ni ngumu kudumu na hilo kusudi au kuendelea na kusudi mathalani utakuta mtu anajitoa sana katika shughuli fulani akitegemea labda atapata pesa lakini pindi inapokuwa kinyume na matarajio utoshangaa kesho katoa udhuru wa kutoendelea na shughuli hiyo.

Biblia inasema “ hakuna aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe “.
1 Wakorintho 9:7 Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?

Kusudi lenyewe linajua linahitaji nini ili liweze kudhihirika kwa hiyo ni muhimu ulitambue hilo na utoe nafasi lenyewe liite yaliyo yake sio swala la utendaji wa akili yako usio na uvuvio wake.
Ni muhimu kutambua kusudi lenyewe linaona kuliko macho ya nyama yanayoona, linajua chimbuko lake na hatima yake.

Uwezi kuchoka kama ukikubaliana na kusudi katika yale unayoyataka, kwa maana lenyewe kusudi linajua uhitaji wake.

Usipende kuishi katika maslahi yako pindi unapolitumikia kusudi bali ishi kwa matakwa ya kusudi bila shaka lenyewe litakutunza kukuimarisha maana ndilo matokeo au makusudi yake pindi utakapoamua kuishi katika hilo.

Kama unahitaji kuona fahari na ustawi wa familia na ukoo pamoja na watoto bila kusahau na wajukuu wako basi hunabudi kulitumikia kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.
Uzuri wa kusudi “ ukilitumikia nalo litakutumikia ila ukiliacha litakubwaga mazima “!

Nje ya kusudi uwezi kuona fahari ya wewe kuwepo duniani, kitu pekee ambacho kilicho mshawishi Mungu akuruhusu uje duniani ni kwa sababu ya hilo kusudi mbali na hilo hakuna kitu kingine.

Usiwe mjuaji sana katika kusudi maana utalitumia kwa namna yako ( kulitaka likutumikie baada ya wewe kulitumikia ) kwakuwa lenyewe lilivyoachiliwa linamaelekezo yote bali wewe kuwa mnyenyekevu na umakini wa kulisikiliza hapo utakua salama.

“ kuyapenda maisha yako ni kulipenda kusudi lililowekwa ndani yako “

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 8 Februari 2019

HUWEZI KUISEMEA KESHO KABLA UJAIONA LEO!



Ni jambo lisilo pingika kuwa “ fahari ya kesho inategemea maisha ya leo ” hivyo tunaifurahia jana kwakuwa tumeiona leo?

Karibu……….!!!

Japo zote tunahita kuwa ni siku lakini majina yao yanajitofautisha ndomana hii inaitwa KESHO na nyingine inaitwa LEO, na ujasiri wako wa kusema “ kesho tutaonana” ni kwasababu upo leo.
Mtu yeyote mwenye kiburi/ majivuno fulani, lazima pawepo na kitu kinachomfanya kuwa katika hali hiyo……hauwezi kuwa juu tu kama hakuna kitu kinacho kushikiria na kukufanya kuwa juu.

Unaweza kuipenda sana leo kwasababu ya kesho na pia unaweza kuichukia sana leo pindi utakapoifikiria kesho mathalani kijana anayejua kesho ndio siku yake ya harusi na yuko tayari uwa anaona kesho ni mbali kwa namna alivyopania na shauku iliyojaa moyoni mwake vilevile kwa mfungwa anayejua kesho ndio siku yake ya kunyongwa na anayapenda kuishi pindi atakapoifikiria kesho moyo wake utakuwa katika hali mbaya maana huzuni na simanzi vitakuwa vimeujaza moyo wake.

Ukiangalia maisha ya mkulima unaweza kujifunza kitu, unaweza kukuta mkulima anautesa mwili wake akiamka alfajiri na kwenda kulima, akihusisha na uchumi wake katika kununua vifaa bora, mbegu bora na hata mbolea lakini katika maumivu hayo bado akawa amejawa na furaha na matumaini pindi atakavyoifikiria kesho katika mavuno yake!

Kabla ujajitamba kwa ajili ya kesho ni muhimu uwe na leo imara inayoweza kukuweka katika hatua bora kesho, japo wakati mwingine ni ngumu sana kuitafsiri kesho kwasababu ya leo……….sio siku zote unapoona leo umeshiba basi ukajua kesho utashiba hivyo hivyo.

Maana wapo wanaoishi leo kanakwamba hakuna kesho na pindi leo ikianza kuyoyoma na kesho ikianza kuchomoza hapo uweza kumfanya mtu kuwa na maswali yaliyo kosa jibu kwakuwa hakujiandaa kwa ajili ya kesho.

Jifunze kuiona leo vizuri ili ije kesho iliyo nzuri, kwakuwa ukiichukia leo sio rahisi kuipenda kesho kwa maana kesho ni matokeo ya leo naam ni ngumu tu kuuchukia mwembe ukayapenda maembe kwakuwa mwembe unaotoa maembe mazuri huo utunzwa sana na wakati mwingine ata ulinzi uwekewa.

Na ni kawaida hauwezi kuyafanya makubwa kama ujaanza na madogo, kwahiyo usidharau moja ukapenda miamoja  pasipo kujua unaanza na moja ndiyo itakupeleka kwenye mia moja.
Unapoiona kesho usifikiri tu itakuwa  tu kesho ni muhimu utambue kuwa kabla ya kesho kulikuwa na juzi, jana na leo hatimaye itakupelekea kesho hivyo usione kesho kama kitu pekee kuwa unaweza kukipata pasipo kuitambua leo.

Japo usipoitambua leo ukaikulupukia kesho basi hapo utakapokuwa umeingia kesho utaanza kuona mapungufu yake na kuona kama umekosea kwakuwa ukuitendea vyema jana yake. Ni muhimu kutoitamani kesho maana kesho itakuja tu maadam leo ikisha malizika,

Ipende sana leo na uhakikishe imekaa vizuri maana ikiwa leo iko vizuri itakuwa sawa maana ni sawa na kutengeneza msingi wa ghorofa haraka haraka pasipo kuzingatia vigezo vyake ili msingi uwe imara na pindi baada ya kumaliza ujenzi muda si msingi ukalemewa na kuanza kuporomoka wewe unaweza kushangaa lakini uhalisia utazungumza.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson……………………………… 0764 018535

Ijumaa, 14 Septemba 2018

SWALI LINAKOSA MAANA!




Kama binadamu uliopata neema kuingia katika mifumo mbalimbali ya elimu na kufanya mitihani, utakuwa ulishakutana na maswali katika mitihani yaliyokosewa au yasiyo na majibu!

Wakati mwingine swali lililokosewa uweza kurekebishwa ili liwe na MAANA au kubadilishwa na pengine kutoa alama za bure (free masks) ikiwa hilo swali alikujulikana mapema wakati wa mtihani ila baada ya kusahihishwa mtihani likagundulika.

Karibu!!!

Maswali yamekuwa ni rafiki wa akili na hasa katika kupasha joto ubongo, na upelekea hali nzuri kwa akili kupanuka na kupata uelewa mwingine.

Na wakati mwingine mtu anapokosa jibu hali hiyo uweza kuingia ndani ya moyo na kuleta usumbufu, usumbufu wa mtu kuwa na maswali mengi kwa kile kinacho mkabili pasipo kujua niende kushoto au kulia, hali ya swali kuwa na jibu zaidi ya moja na hatimaye kushindwa kupata jibu linalojitosheleza na hata kujikuta uko njia panda.

Pindi inapotokea mtu anapokuwa na maswali mengi kichwani mwake kwa kiasi kikubwa inategemea hulka ya mtu husika wako watu wanapokuwa katika hali hii upenda kucheza mziki, au kupiga makelele,kuongea sana, kukaa kimya na mwingine upenda kulala hama kulewa na mambo mengine yafananayo na hayo lakini bado unaweza kukosa jibu sahihi au lililojitosheleza katika swali husika.

SWALI LINAKOSA MAANA PALE UNAPOPATA JIBU!

Kama samaki anapo poteza makeke yake au usumbufu wake ni pale utakapo fanikiwa kumtoa nje ya maji na kumweka nchi kavu………………………………………………..!

Ndivyo ilivyo pindi utakapopata majibu katika maswali yanayo kukabili hapo akili uweza kutulia na hali ya ushwari uweza kuingia ndani ya moyo wako.

Ndomana waswahili usema “ atafutae achoki na akichoka amepata” hivyo utashangaa pindi mtu atakapo choka wakati ajapata japo yote yanawezekana kutegemea na hali ya ndani ya mtu husika .

Na wakati mwingine unaweza pata majibu lakini sio utatuzi wa leo wala kesho bali utakuweka katika hali njema ya matarajio ya uhakika wa kweli katika majira yajayo.

Usiruhusu maswali yawe maisha yako maana yatautesa ufahamu wako! Bali tambua kwa kila jambo/swali linalokuja katika maisha yako uwa tatizo linaisha ni mpaka ujue majibu ya maswali hayo yanapatikana wapi? Maana ukikosa kujua sehemu husika hauwezi pata majibu ya uhakika.

“ hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea”

1 Wakorintho 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Endapo ikatokea ukakosa majibu ya maswali yako kwa wanadamu ( watu unao waamini) usihofu wewe fungua hazina ya mbingu hiyo uwa haikosi majibu maadam mbingu hipo basi mwenye mbingu yupo na majibu yapo.

Haya ni majibu yanayoleta amani ya kudumu, maana hicho ndicho chanzo sahihi cha majibu ya maswali yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………0764 018535

Ijumaa, 20 Julai 2018

CHA MUHIMU KWANGU!





“ ukristo wangu ndio maisha yangu”

Uzuri wa dunia na utamu wake ni kwamba kila mtu anakitu kwake anakiona kuwa ni muhimu kwake, lakini tatizo linakuja pale tu kitu kimoja kila mmoja akakiona ni muhimu kwake na kutaka kuwa nacho kwa muda mmoja hapo ugomvi na chuki uweza kuzaliwa.

Kama binadamu kuwa na kitu cha muhimu ni jambo la kawaida, kwa kuwa kila binadamu ana mwelekeo wake hivyo upelekea hali ya mtu kuwa na kipaumbele chake, japo anaweza asijue kuwa jambo hilo kipaumbele kwake ila hicho kitu kitachukua nafasi kubwa katika moyo wake na hata hisia zake.

Japo umuhimu wa kitu (kipaumbele) ubadilika kulingana na mazingira husika na hali iliyotokea mathalani baba anaweza kuweka kipaumbele kwa mwanae lakini inapotokea mwenendo wa huyo mtoto kutoufurahisha moyo wa baba, hivyo umuhimu wake unaweza kushuka na hatimaye kipaumbele kubadilishwa.

Cha Muhimu kwangu! Ni hali ya mtu kuwa na kitu kitakacho kukuwezesha kuwa katika hali yako ya ubora na ustawi na kwa umakini wa kufuata maelekezo kwa uangalifu wa rohoni na mwilini.
Ndomana unaweza usishangae kwa kipindi cha kwanza mtu anaweza fanya kitu kilicho bora au kizuri lakini pindi unapopoteza umakini katika kipaumbele chake ( jambo la msingi katika kufanikiwa kwake) basi hapo unawezafanya kitu kilekile na kwa namna ile ile lakini matokeo yakawa tofauti na alivyotegemea. 

Kuna wakati unaona kuna mambo mengi ya kufanya ukashindwa kuchukua hatua au kufanya maamuzi sahihi katika kutoa nafasi ya kwanza kwa kile kitu muhimu au kilicho kuwezesha kuwa pale.

Unaweza kukuta mtu alikuwa na huduma ilipoanza kutumika ikaleta matokeo mazuri na hatimaye kupelekea kufahamika na kuzidi kugusa maisha ya watu wengi na katika hali hiyo ukajikuta kupenda sifa na kutopenda kushuka ( kama ilivyo asili ya Mungu ndani ya mwanadamu) na hata kuanza kupelekwa na kila upepo kushoto au kulia na hatimaye kupoteza chanzo cha ubora/ ustawi wake.

Sio mara zote msingi wako ( chanzo cha ustawi) unapo poteza ukajikuta uko chini, unaweza kupoteza chanzo cha ustawi wako lakini ukakuta hakuna mabadiliko ya inje yanayoweza kukutisha hivyo ukaendelea na msimamo wako pasipo kujali mng’ao wa kesho yako.

Lakini dalili kuu ya kutambua kuwa chanzo chako kilichopelekea mng’ao wako kimepotea ni ongezeko la tabia za mwilini.( ubinafsi na kujiami zinakuwa na nguvu sana kwako ).

Kwa Yule ambaye ajapoteza chanzo japo upepo na dhoruba zinaweza kumsonga lakini hali ya uhakika wa kesho yake iliyojaa amani na tumaini la mbingu linakaa ndani yake.

Ni muhimu kuwa makini na utendaji wa mbingu katika maisha yako ( huduma/ shughuli unayoifanya).

Na mtu wa namna hii ( anayetambua chanzo na kukithamini ) uwa hana mashindano bali usimamia kwa ufasaha wajibu wake.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………0764 018535