USIYESHINDWA;
Ningependa hili NENO likawe wimbo wako, unaotawala
akili yako na iliyopata nafasi katika moyo wako na udhihirisho mkuu katika
maisha yako. Ni kweli tunamshukuru Mungu kutokana na namna tulivyoishi mwaka
2014 haijarishi ulikuwa upande upi kwako kama ulikuwa mwepesi au mzito katika
yote bado tunamuona Mungu katika yote hasa yaliyo inje ya akili au uwezo wetu
binafsi.
Naamini wapo watu katika dunia tuliyonayo watu
hawaoni maana ya kumshukuru Mungu katika mwaka tunaomalizia kwa masuabu waliyo yapata
na pia kuna wengine wananafasi kubwa katika kumshukuru Mungu katika mazingira
ya wenye ufahamu na wasio na ufahamu unaomwezesha mtu katika kufanya jambo
stahiki.
Siko hapa katika kuwaambia mfanye tathmini katika
maisha yako zaidi sana ningependa uanze kuona katika muono mwingine wa
kumwezesha Mungu aweze kujidhihirisha vile alivyo katika maisha yako. Hili ni
neon ambalo mimi binafsi nalipenda sana kwani nimejifunza kumuona Mungu sana
pindi ninapoamini kuwa yeye Mungu ajawai shindwa kutokana na muonekano wake
ulivyo, japo kushindwa ni kibinadamu bali Mungu vile alivyo ajawai shindwa
katika kutekeleza mpango wake.
Hili ni neno kwa watu wengi uanza kulitumia lakini
kamwe hawawezi kumudu kulitumia kutokana na nguvu ya macho ya mwilini
yaliyomkuta petro.........(asomaye na hafahamu).
Kweli neno hili likatoe nafasi iliyokubwa katika
maisha yako na kuona fahari ya Mungu katika maisha pamoja nawe! Ni lazima
umuone kuwa ashindwi ili aweze kukuwezesha katika kushinda kwasababu ukweli ni
yeye anashinda kupitia wewe. Na hata kama umeshindwa mara nyingi sana lakini
jua kwamba yeye Mungu ajawai kushindwa kamwe kwakua yeye ni zaidi ya
chochote.........na macho yake hayawezi kuzuiliwa na chochote.
Ukweli kibinadamu kuna muda unachoka lakini tambua
kitu kimoja kwamba Mungu katika uumbaji wake alikutana na mambo mengi lakini
kamwe hakuona kile ambacho kinaweza kuwa ni changamoto kwake au kumzuilia yeye
asiendelee na mpango wake. Vile alivyokuwa akifanya yote ndivyo hivyo ataweza
kufanya yote kati ya yote yanayokukabili endapo tu ukimkubali katika maisha
yako ( kumwamini ).
Unahitaji kumwelewa Mungu kwa mapana yake kwakua
yeye jinsi alivyo anajitosheleza na hana kikwazo kwake ambacho kitamfanyaasiweze
kukutosheleza zaidi sawa na uwitaji wako katika haya yote jambo kubwa ni KUMJUA
MUNGU!
Lazima utofautishe kumjua Mungu na kujua habari za
Mungu kwani kumjua Mungu sio kujua habari za Mungu kwakua kujua habari za Mungu
hazitakusaidia zaidi sana ni kumjua Mungu mwenyewe, kwani katika yeye.
Kumjua Mungu ni namna unavyopata maongozi ya KImungu
katika shughuli za kila siku kwakua tunajua kileunachojua ndicho unkiweka
katika utendaji inaweza kuwa katika ujuzi mbalimbali mathalani upishi wa
kisasa, namna ya kutumia bidhaa kwa ufanisi au kuendesha biashara zako kwa
faida.
Kumjua Mungu akuishii kwenda kanisani tu bali
MPASUKO WA UFAHAM ULIOJAA MUNGU.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson................................................................0764 018535