Jumatatu, 27 Aprili 2015

MAUSIANO SALAMA-3



MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;

 Tukiwa katika nafasi ya tatu katika mfululizo wa somo letu linalo husuiana swala zima la MAUSIANO, bila kupoteza muda tutaenda kuangalia sehemu ya tatu  katika kupata mwanga katika fahamu zetu na kutupelekea maamuzi sahihi!

I.UTAYARI WA KIMWILI

Mabadiliko ya kimwili (biological change) hiki kitu cha kawaida sana na ni muhimu sana kwa mwadamu kitokee katika maisha yake…….na mabadiliko yanaanza tangu mtoto anapoanza kutungwa katika tumbo la mwanamke hivyo sio swala la kushangaa ila inabaki ni lazima na muhimu sana hayo mabadiliko ya tokee ili kukuweka tayari katika hatua inayofuata ili uweze kuimudu na kuifurahia. Zipo hatua kama tatu au nne katika ukuaji wa mwanadamu lakini mimi sitaziongelea hizo hatua kwa sasa bali nitatenga miaka ambayo mambo mengi yamekuwa yakitokea na mfumo wa mwanadamu umekuwa ukileta mapinduzi makubwa!

Miaka 14 hadi 35………..kwa wanawake na wanaume!!!
Hiki ni kipindi ninapenda ni kiongelee kwa sasa japo zaidi ya hapo sio kwamba wako salama sana…la asha! Wanaweza kuwa na hali mbaya kuliko hiyo miaka niliotoa hapo juu.
Miaka (14-35) hii ni miaka ambayo ni hatari sana kutokana na mabadiliko mengi uanzia hapo kwa wanawake mifumo ya uzazi inaanza kujiweka sawa mathalani maziwa uchomoza kwa mwanamke na mabadiliko mengine na hata kwa wanaume mabaliko uanza ya uzazi na hasa upande wa homoni uweza kujiweka sawa katika mfumo wa uzazi.

Hapa mtu uweza kujiona amekuwa zaidi ya hali halisi ilivyo uweza kujifananisha na mwanaume yeyote au mwanamke yeyote na kuona hakuna utofauti kutokana na mabadiliko ya mwili wake ya mefanana na mtu yeyote ukizingatia maneno anayopewa na watu wengine mathalani wewe sio mtoto ona kifua kimejaa, nyonga na vitu vingine hivyo mtu uweza kuona kweli amekuwa na kuwa na anauwezo wa kufanya mambo ya kikubwa yaani vile mkubwa anavyofanya nae anaweza kufanya pasipo kuanagalia na hiyo hatua watu wote wameipitia lakini uweza kujiona kuwa yeye ndio wa kwanza kupitia hatua hiyo hivyo uweza kuwa huru kufanya kile anachojisikia pasipo kuangalia uhalisia wake.

Hatua hii watu wengi upotea kutokana na kiburi, kujiusisha katika uvutaji wa sigara na hata ukahaba na mwisho kujikuta na matokeo tofauti na vile alivyofikiria……….majuto na kukata tama uanzia hapo.

Usijali fuatana nami katika hatua inayofuata……………………………………..!!!

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………………………….0764 018535

Jumanne, 21 Aprili 2015

MAUSIANO SALAMA-1



MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;



     Hakuna USIKU pasipo kuwa GIZA na hakuna SABABU  pasipo kuwa na JAMBO!!

 Tukiwa tuko mwanzoni kabisa katika mfululizo mzima wa kuhusu MAUSIANO kwa ujumla wake….. na penda kukukaribisha wewe mtumishi wa Mungu kwa maana mtu aliye okoka na asiye okoka wote ni wamuhimu sana kwangu na hasa kwa Mungu aliye kuumba na kuniumba yaani kutuumba sote wanadamu na vitu vyote vinavyoonekana na visivyo…………!

Furaha yangu nikuona wewe rafiki yangu unasoma ujumbe huu inawezekana ni kwa mara ya kwanza au ni zaidi ya mara ya kwanza katika kusikia UJUMBE HUU yote katika yote nasema KARIBU SANA kwa maana ujumbe huu umeandikwa ili usomwe na mtu maalumu kama wewe hivyo unavyotumia muda wako kwa wewe kuusomaUJUMBE huu….. moyo wangu unafarijika sana kwani hili ndilo lengo langu …….unapochukua muda katika kusoma ujumbe huu au mfululizo huu ni sawa na furaha ya mtu aliye pika chakula na kuona watu wanakula chakula hicho tena kwa furaha sana hiyo inakuwa ni furaha!

Ni seme mada hii itawafaidia wote na sio sehemu moja tu! Katika jamii kama haitakusaidia wewe kwa wakati huu basi utakuwa msaada kwa wengine katika kusoma ujumbe huu hivyo niseme karibu MAMA,BABA,KIJANA na MTOTO……Na amini mtabarikiwa sana!!!

Katika kuanza ni vizuri niulize maswali yafuatayo! Kinachofanya mtu apende ni nini? Au kinachofanya mtu ajiingize katika mausiano ni nini hasa? Inawezekana ni msukumo wake binafsi (msukumo wa ndani) au msukumo wa ushawishi toka nje yaani marafiki,wazazi na jamii inayomzunguka.

Ukweli kile kitu kilichokusukuma kuingia katika mausiano ndicho kinabeba msingi mkubwa katika mausiano yenu wote….kwakua hicho kitakuwa marejeo yenu katika utofauti wenu! Na wazi kila mausiano yana sababu yake zinaweza kuwa ni sahihi au sio sahihi lakini yote yanabebwa na muhusika au wahusika na mwisho wake ndio utaonyesha maamuzi walifanya yalikuwa ni sahihi au yalikuwa hayana usahihi……..pamoja na hayo yote wewe unaweza ukaona yalikuwa sahihi au hayakuwa sahihi lakini hayo hayawi maamuzi yao, kwani wao wanaweza kuona kila walichokifanya wamekifananya katika hali sahihi zaidi sana hivyo hawaitaji ushauri mwingine walioamua ndio sahihi na ndio bora haijarishi machoni pako panaonekana vipi?

Katika dunia ya sasa uwa hatupendi tu kwasababu tumeamua kupenda basi kuna msukumo ulioambata na hisia kali katika maisha ya mwanadamu wakati mwingine usiojali nini kitakachotokea?
Na je! Unaweza kutofautisha katika ya kushawishiwa na kujishawishi wewe mwenyewe (kuchukua maamuzi binafsi) ni swali jepesi katika moyo wa mwanadamu yeyote kwakua linajibika kirahisi sana kwakua hakuna mtu atauficha moyo wake lakini jambo la gumu sana kulianika hadharani. Ila unaweza kumwambia muhusika yule anaeutesa moyo wako au aliye na nafasi katika moyo wako kwa lugha yako.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson……………………………………0764 018535

Jumanne, 14 Aprili 2015

KITU KIGUMU (hard thing)



KITU KIGUMU.


 Ni maneno ya kawaida sana kusema NDIYO au HAPANA hama NAJUA au SIJUI! Lakini haya maneno yamekuwa yakitumika kinyume chake yaani kile kinachozungumzwa ni tofauti na kile kinacho maanishwa yaani ni tofauti na uhalisia wake………na hatima yake kumepelekea urafiki kuvunjika,ndoa kuvunjika na hata jamii kusambalatika kutokana na maneno haya………mathalani kunaweza kukawa na maji yenye sumu na inawezekana ukamuona mtu anakunywa nawe ukakaa kimya na kumuacha apoteze uhai wake mbele ya macho yake.

Kusema NDIYO wakati ulitakiwa useme HAPANA kunaweza kuwa mwisho wa safari… kwakua kunakuwa na mashaka kusema huu mtindo utakuwa ukiendelea na unaweza ukanigharimu mbele ya safari na baada ya kuona safari kuwa ni njema ikawa safari iliyo mbaya na tofauti ulivyotegemea au hali ilivyo!

Wako watu wamejikita na kusema kuwa ni hekima na kwasababu ni mtu mzima hivyo upaswi kuwa wazi kwa kila mtu na kwa kila kitu, hivyo watu uweza kusema lazima utumie akili vizuri katika kujiweka nafasi nzuri na wengine uweza kusema sehemu ile haikuwa sahihi kwa mimi kusema HAPANA ili niliradhim nisema NDIYO na baadae ninge mwambia ukweli tu!

Si katai na hekima za namna hizi lakini niseme, sehemu kubwa tumetakiwa kuwa WAKWELI zaidi ya kutoa tumaini mahali ambapo hapaitajiki tumaini hilo ambalo unaloliwaza na kufikiri kuwa itakuwa ni hekima lakini katika ulimwengu wa sasa tumekuwa kinyume sehemu kubwa imekuwa ni hekima kuliko uhalisia wenyewe……….LET CALL DARKNESS AS IT IS!  Na LIGHT AS IT IS! No approximation acha yote yawe kama yalivyo.

Napenda kusema kuwa UKWELI unakufanya kuishi maisha ya UHURU zaidi ya kusema nimetumia HEKIMA lakini baadae ukaishi maisha ya UTUMWA na kuanza kukimbiana zaidi baada ya kuboresha maisha yako ya kila siku….ni seme wazi hivi vitu havichangamani wala havifananishwi kama vilivyotofauti na ndivyo vitakavyokuwa hakuna mbadala wake na bora uache kuvichanganya hivi vitu kwani  unaweza kufanya kuwa na furaha badala ya huzuni au kuwa na huzuni badala ya furaha na unaweza UA  mtu kwa kuchanganya haya maneno.

Sawa na dakatari kumwambia mtu anaumwa mafua kumbe anaumwa kifua kikuu na kufanya mtu kuanza kutumia dozi ya mafua badala ya kifua kikuu na hatimae kupoteza maisha…..hali hii utokea sana pale mtu anapokuta na mtu anayemtamani sana na kuanza kumwagia sifa ili mradi ampate na baada ya kumpata basi hapo uzaliwa uhalisia na huo urafiki au ushirikiano uanza kupotea.

Kama wewe upendwi kufurahishwa pasipo na manufaa kamili kwako hama kuambiwa kitu ambacho sivyo kilivyo na hatimae nawe ukakubaliana na hali hiyo na kuchukulia kuwa hivi ndivyo ilivyo kumbe ni tofauti kabisa hivyo ukupelekea baaada ya kufikiria utatuzi ukaanza kufikiria namna ya kusherekea kitu ambacho hakipo!

Tumia muda wako kuongea kile kilichopo KWELI ili Mungu akinyambulishe ndani ya mioyo ya watu na sio wewe kutumia wakati huu kuonyesha una hekima kumbe unazidi kuharibu baada ya kujenga..hata ukitumia maneno ya ushawishi wa kibinadamu bado hauwezi kugusa moyo wamwanadamu vile unapaswa kuguswa na mbaya zaidi ya kuugusa ukaugusa katika upande wa mbaya sana chuki ikaanza hapo! Au hata kuufurahisha sana moyo wake lakini mara baada ya 

kugundua ukweli utakuwa matatani sani kuliko vile ilivyo.
Usitafute kumfurahisha Mungu bali amua kuishi maisha yenye kibali kwa Mungu kwa ukamilifu yeye  atakuwa kibali kwako na kukidhihirisha kwa watu wengi na hata kama kibali akija tokea usalama wako na Mungu ni muhimu kuliko chochote.

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

Jumanne, 7 Aprili 2015

THAMANI YAKE NDIO UTHAMANI WANGU



THAMANI YAKE NDIO UTHAMANI WANGU;



 hapa na zungumzia UTHAMANI usio chuja au kupungua na hata kupotea kabisa bali na zungumzia uthamani unaozidishwa kila siku na kung’aa siku baada ya siku…….huu ni uthamani hautaji fedha au manukato yoyote bali wenyewe umebeba hivyo vyote na kwa maana hiyo umejitosheleza kila idara hautaji usaidizi mwingine!

Huu uthamani uwa haunaga badala yake( copy) kwa hiyo ukiupata umeupata na ukiukosa basi umeukosa hakuna cha ongo wala rushwa yaani hakuna njia ya mkato wananchi wanaita wakichina huu hauna feki wala mbadala wake huko wenyewe kama ulivyo na unawezeshwa na kitu kisicho kijua ongo maana yake nini?

Hakuna mashaka endapo ukiupata uthamani huu basi vyote vita (appreciate) kukubali kutokana uzito na ukubwa pamoja na huo uthamani…..huu ni uthamani ambao mbingu inachilia ndani yako na kukufanya kuwa tunu katika mbingu(macho pa Mungu) na kwa wanadamu wote haijarishi mkubwa au mdogo………mathalani mfalme suleimani alipewa hekima ambacho watu kutoka pande zote za dunia walikuja kushuhudia hekima hiyo ya ajabu walioisikia kwa kua ilikuwa ya tofauti sana na ilikuwa na majibu ya watu wengi ……….wafalme na wanachi wote waliitaji.

Hii ni thamani ambayo inashikiliwa na mbingu na kamwe hakuna kitu ambacho kinaweza kuondoa hapo kwako……biblia inasema Mungu akisema NDIO hakuna atayesema HAPANA.

Kibinadamu tumekuwa tukitafuta thamani katika hali ya ufahari kuwa na magari ya kifahari na majumba makubwa na mali zingine ambazo zinaonekana na kivutio kwa watu wengi sana na kuamini kuwa hivi vitu vita leta heshima na hatimae uthamani… hivyo jamii imejikuta kuingia katika udhulumati,ujamabazi,ujangiri na hata kuwa toa kafara watoto wao na binadamu wengine

Nipende kusema kuwa huu uthamani hauna ushawishi wowote ule wa kimwili bali unaushawishi mkubwa katika kiroho tu, kwakua mafuruko ya rohoni ndio upelekea kumwagika katika nje! Kama ningepewa nafasi ya kuwambia watu kuhusu UTHAMANI bali ninge uzungumzia sana huu uthamani wa mbingu katika maisha ya mwanadamu kwakua hakuna majuto katika uthamani wala mwisho wake sio ubatili.

Huu uthamani unapatikana kwa njia rahisi sana……..ni kuruhusu nguvu ya Mungu itawale na iendeshe maisha yako tu, najua unaweza kuwa na maswali lakini kubwa kuliko yote niseme hakuna binadamu ambaye hakuna kitu kinachomwendesha inaweza kuwa hali yake ya ubinafsi,elimu, maadili na hata nguvu za giza……..lakini mtu ambaye Mungu kweli ndio dira yake na kiongozi katika maisha yake kwa asilimia zote.

Mtu aliyejaa uthamani wa kimbingu ndani yake huwa na zungumzia ile thamani ya kimbingu iliyo ndani yake inajilinda haiataji ulizi mwingine wala usingizi wake sio wa mashakamashaka kwakua unatolewa katika kipimo cha kutosha na kukidhi viwango stahiki huwa hauna vipimo bali unatolewa katoka hali na ujazo wa kumwagika ambao unakuwa uliojaa na kuimalika katika ubora.

Hivyo niseme wazi bado una nafasi kubwa sana ya kuupata huu uthamani kama ujaokoka ni vizuri umpokee yesu katika maisha yako na kama umeokoka basi unayofursa kubwa na wakati ndio sasa amua kuzidi katika Mungu katika maarifa sahihi ya Mungu, hauhitaji ujifanyishe bali kipo ndani yako ni wewe kujiachia ili kijidhihirishe.

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535