THAMANI
YAKE NDIO UTHAMANI WANGU;
hapa na zungumzia
UTHAMANI usio chuja au kupungua na hata kupotea kabisa bali na zungumzia
uthamani unaozidishwa kila siku na kung’aa siku baada ya siku…….huu ni uthamani
hautaji fedha au manukato yoyote bali wenyewe umebeba hivyo vyote na kwa maana
hiyo umejitosheleza kila idara hautaji usaidizi mwingine!
Huu uthamani uwa
haunaga badala yake( copy) kwa hiyo ukiupata umeupata na ukiukosa basi umeukosa
hakuna cha ongo wala rushwa yaani hakuna njia ya mkato wananchi wanaita
wakichina huu hauna feki wala mbadala wake huko wenyewe kama ulivyo na
unawezeshwa na kitu kisicho kijua ongo maana yake nini?
Hakuna mashaka endapo
ukiupata uthamani huu basi vyote vita (appreciate) kukubali kutokana uzito na
ukubwa pamoja na huo uthamani…..huu ni uthamani ambao mbingu inachilia ndani
yako na kukufanya kuwa tunu katika mbingu(macho pa Mungu) na kwa wanadamu wote
haijarishi mkubwa au mdogo………mathalani mfalme
suleimani alipewa hekima ambacho watu kutoka pande zote za dunia walikuja
kushuhudia hekima hiyo ya ajabu walioisikia kwa kua ilikuwa ya tofauti sana na
ilikuwa na majibu ya watu wengi ……….wafalme na wanachi wote waliitaji.
Hii ni thamani ambayo
inashikiliwa na mbingu na kamwe hakuna kitu ambacho kinaweza kuondoa hapo
kwako……biblia inasema Mungu akisema NDIO hakuna atayesema HAPANA.
Kibinadamu tumekuwa
tukitafuta thamani katika hali ya ufahari kuwa na magari ya kifahari na majumba
makubwa na mali zingine ambazo zinaonekana na kivutio kwa watu wengi sana na
kuamini kuwa hivi vitu vita leta heshima na hatimae uthamani… hivyo jamii
imejikuta kuingia katika udhulumati,ujamabazi,ujangiri na hata kuwa toa kafara
watoto wao na binadamu wengine
Nipende kusema kuwa huu
uthamani hauna ushawishi wowote ule wa kimwili bali unaushawishi mkubwa katika
kiroho tu, kwakua mafuruko ya rohoni ndio upelekea kumwagika katika nje! Kama
ningepewa nafasi ya kuwambia watu kuhusu UTHAMANI bali ninge uzungumzia sana
huu uthamani wa mbingu katika maisha ya mwanadamu kwakua hakuna majuto katika
uthamani wala mwisho wake sio ubatili.
Huu uthamani
unapatikana kwa njia rahisi sana……..ni kuruhusu nguvu ya Mungu itawale na
iendeshe maisha yako tu, najua unaweza kuwa na maswali lakini kubwa kuliko yote
niseme hakuna binadamu ambaye hakuna kitu kinachomwendesha inaweza kuwa hali
yake ya ubinafsi,elimu, maadili na hata nguvu za giza……..lakini mtu ambaye
Mungu kweli ndio dira yake na kiongozi katika maisha yake kwa asilimia zote.
Mtu aliyejaa uthamani
wa kimbingu ndani yake huwa na zungumzia ile thamani ya kimbingu iliyo ndani
yake inajilinda haiataji ulizi mwingine wala usingizi wake sio wa
mashakamashaka kwakua unatolewa katika kipimo cha kutosha na kukidhi viwango
stahiki huwa hauna vipimo bali unatolewa katoka hali na ujazo wa kumwagika
ambao unakuwa uliojaa na kuimalika katika ubora.
Hivyo niseme wazi bado
una nafasi kubwa sana ya kuupata huu uthamani kama ujaokoka ni vizuri umpokee
yesu katika maisha yako na kama umeokoka basi unayofursa kubwa na wakati ndio
sasa amua kuzidi katika Mungu katika maarifa sahihi ya Mungu, hauhitaji
ujifanyishe bali kipo ndani yako ni wewe kujiachia ili kijidhihirishe.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni