KITU KIGUMU.
Ni maneno ya kawaida
sana kusema NDIYO au HAPANA hama NAJUA au SIJUI! Lakini haya maneno yamekuwa
yakitumika kinyume chake yaani kile kinachozungumzwa ni tofauti na kile kinacho
maanishwa yaani ni tofauti na uhalisia wake………na hatima yake kumepelekea
urafiki kuvunjika,ndoa kuvunjika na hata jamii kusambalatika kutokana na maneno
haya………mathalani kunaweza kukawa na maji yenye sumu na inawezekana ukamuona mtu
anakunywa nawe ukakaa kimya na kumuacha apoteze uhai wake mbele ya macho yake.
Kusema NDIYO wakati
ulitakiwa useme HAPANA kunaweza kuwa mwisho wa safari… kwakua kunakuwa na
mashaka kusema huu mtindo utakuwa ukiendelea na unaweza ukanigharimu mbele ya
safari na baada ya kuona safari kuwa ni njema ikawa safari iliyo mbaya na
tofauti ulivyotegemea au hali ilivyo!
Wako watu wamejikita na
kusema kuwa ni hekima na kwasababu ni mtu mzima hivyo upaswi kuwa wazi kwa kila
mtu na kwa kila kitu, hivyo watu uweza kusema lazima utumie akili vizuri katika
kujiweka nafasi nzuri na wengine uweza kusema sehemu ile haikuwa sahihi kwa
mimi kusema HAPANA ili niliradhim nisema NDIYO na baadae ninge mwambia ukweli
tu!
Si katai na hekima za
namna hizi lakini niseme, sehemu kubwa tumetakiwa kuwa WAKWELI zaidi ya kutoa
tumaini mahali ambapo hapaitajiki tumaini hilo ambalo unaloliwaza na kufikiri
kuwa itakuwa ni hekima lakini katika ulimwengu wa sasa tumekuwa kinyume sehemu
kubwa imekuwa ni hekima kuliko uhalisia wenyewe……….LET CALL DARKNESS AS IT
IS! Na LIGHT AS IT IS! No approximation
acha yote yawe kama yalivyo.
Napenda kusema kuwa
UKWELI unakufanya kuishi maisha ya UHURU zaidi ya kusema nimetumia HEKIMA
lakini baadae ukaishi maisha ya UTUMWA na kuanza kukimbiana zaidi baada ya
kuboresha maisha yako ya kila siku….ni seme wazi hivi vitu havichangamani wala havifananishwi
kama vilivyotofauti na ndivyo vitakavyokuwa hakuna mbadala wake na bora uache
kuvichanganya hivi vitu kwani unaweza
kufanya kuwa na furaha badala ya huzuni au kuwa na huzuni badala ya furaha na
unaweza UA mtu kwa kuchanganya haya
maneno.
Sawa na dakatari
kumwambia mtu anaumwa mafua kumbe anaumwa kifua kikuu na kufanya mtu kuanza
kutumia dozi ya mafua badala ya kifua kikuu na hatimae kupoteza maisha…..hali
hii utokea sana pale mtu anapokuta na mtu anayemtamani sana na kuanza kumwagia
sifa ili mradi ampate na baada ya kumpata basi hapo uzaliwa uhalisia na huo
urafiki au ushirikiano uanza kupotea.
Kama wewe upendwi
kufurahishwa pasipo na manufaa kamili kwako hama kuambiwa kitu ambacho sivyo
kilivyo na hatimae nawe ukakubaliana na hali hiyo na kuchukulia kuwa hivi
ndivyo ilivyo kumbe ni tofauti kabisa hivyo ukupelekea baaada ya kufikiria
utatuzi ukaanza kufikiria namna ya kusherekea kitu ambacho hakipo!
Tumia muda wako kuongea
kile kilichopo KWELI ili Mungu akinyambulishe ndani ya mioyo ya watu na sio
wewe kutumia wakati huu kuonyesha una hekima kumbe unazidi kuharibu baada ya
kujenga..hata ukitumia maneno ya ushawishi wa kibinadamu bado hauwezi kugusa
moyo wamwanadamu vile unapaswa kuguswa na mbaya zaidi ya kuugusa ukaugusa
katika upande wa mbaya sana chuki ikaanza hapo! Au hata kuufurahisha sana moyo
wake lakini mara baada ya
kugundua ukweli utakuwa matatani sani kuliko vile
ilivyo.
Usitafute kumfurahisha
Mungu bali amua kuishi maisha yenye kibali kwa Mungu kwa ukamilifu yeye atakuwa kibali kwako na kukidhihirisha kwa
watu wengi na hata kama kibali akija tokea usalama wako na Mungu ni muhimu
kuliko chochote.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni