MAMBO
YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;
Hakuna
USIKU pasipo kuwa GIZA na hakuna SABABU
pasipo kuwa na JAMBO!!
Tukiwa tuko mwanzoni
kabisa katika mfululizo mzima wa kuhusu MAUSIANO kwa ujumla wake….. na penda
kukukaribisha wewe mtumishi wa Mungu kwa maana mtu aliye okoka na asiye okoka
wote ni wamuhimu sana kwangu na hasa kwa Mungu aliye kuumba na kuniumba yaani
kutuumba sote wanadamu na vitu vyote vinavyoonekana na visivyo…………!
Furaha yangu nikuona
wewe rafiki yangu unasoma ujumbe huu inawezekana ni kwa mara ya kwanza au ni
zaidi ya mara ya kwanza katika kusikia UJUMBE HUU yote katika yote nasema
KARIBU SANA kwa maana ujumbe huu umeandikwa ili usomwe na mtu maalumu kama wewe
hivyo unavyotumia muda wako kwa wewe kuusomaUJUMBE huu….. moyo wangu
unafarijika sana kwani hili ndilo lengo langu …….unapochukua muda katika kusoma
ujumbe huu au mfululizo huu ni sawa na furaha ya mtu aliye pika chakula na
kuona watu wanakula chakula hicho tena kwa furaha sana hiyo inakuwa ni furaha!
Ni seme mada hii
itawafaidia wote na sio sehemu moja tu! Katika jamii kama haitakusaidia wewe
kwa wakati huu basi utakuwa msaada kwa wengine katika kusoma ujumbe huu hivyo
niseme karibu MAMA,BABA,KIJANA na MTOTO……Na amini mtabarikiwa sana!!!
Katika kuanza ni vizuri
niulize maswali yafuatayo! Kinachofanya mtu apende ni nini? Au kinachofanya mtu
ajiingize katika mausiano ni nini hasa? Inawezekana ni msukumo wake binafsi
(msukumo wa ndani) au msukumo wa ushawishi toka nje yaani marafiki,wazazi na
jamii inayomzunguka.
Ukweli kile kitu
kilichokusukuma kuingia katika mausiano ndicho kinabeba msingi mkubwa katika
mausiano yenu wote….kwakua hicho kitakuwa marejeo yenu katika utofauti wenu! Na
wazi kila mausiano yana sababu yake zinaweza kuwa ni sahihi au sio sahihi
lakini yote yanabebwa na muhusika au wahusika na mwisho wake ndio utaonyesha
maamuzi walifanya yalikuwa ni sahihi au yalikuwa hayana usahihi……..pamoja na
hayo yote wewe unaweza ukaona yalikuwa sahihi au hayakuwa sahihi lakini hayo
hayawi maamuzi yao, kwani wao wanaweza kuona kila walichokifanya wamekifananya
katika hali sahihi zaidi sana hivyo hawaitaji ushauri mwingine walioamua ndio
sahihi na ndio bora haijarishi machoni pako panaonekana vipi?
Katika dunia ya sasa
uwa hatupendi tu kwasababu tumeamua kupenda basi kuna msukumo ulioambata na
hisia kali katika maisha ya mwanadamu wakati mwingine usiojali nini
kitakachotokea?
Na je! Unaweza
kutofautisha katika ya kushawishiwa na kujishawishi wewe mwenyewe (kuchukua
maamuzi binafsi) ni swali jepesi katika moyo wa mwanadamu yeyote kwakua
linajibika kirahisi sana kwakua hakuna mtu atauficha moyo wake lakini jambo la
gumu sana kulianika hadharani. Ila unaweza kumwambia muhusika yule anaeutesa
moyo wako au aliye na nafasi katika moyo wako kwa lugha yako.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni