Jumatatu, 27 Aprili 2015

MAUSIANO SALAMA-3



MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;

 Tukiwa katika nafasi ya tatu katika mfululizo wa somo letu linalo husuiana swala zima la MAUSIANO, bila kupoteza muda tutaenda kuangalia sehemu ya tatu  katika kupata mwanga katika fahamu zetu na kutupelekea maamuzi sahihi!

I.UTAYARI WA KIMWILI

Mabadiliko ya kimwili (biological change) hiki kitu cha kawaida sana na ni muhimu sana kwa mwadamu kitokee katika maisha yake…….na mabadiliko yanaanza tangu mtoto anapoanza kutungwa katika tumbo la mwanamke hivyo sio swala la kushangaa ila inabaki ni lazima na muhimu sana hayo mabadiliko ya tokee ili kukuweka tayari katika hatua inayofuata ili uweze kuimudu na kuifurahia. Zipo hatua kama tatu au nne katika ukuaji wa mwanadamu lakini mimi sitaziongelea hizo hatua kwa sasa bali nitatenga miaka ambayo mambo mengi yamekuwa yakitokea na mfumo wa mwanadamu umekuwa ukileta mapinduzi makubwa!

Miaka 14 hadi 35………..kwa wanawake na wanaume!!!
Hiki ni kipindi ninapenda ni kiongelee kwa sasa japo zaidi ya hapo sio kwamba wako salama sana…la asha! Wanaweza kuwa na hali mbaya kuliko hiyo miaka niliotoa hapo juu.
Miaka (14-35) hii ni miaka ambayo ni hatari sana kutokana na mabadiliko mengi uanzia hapo kwa wanawake mifumo ya uzazi inaanza kujiweka sawa mathalani maziwa uchomoza kwa mwanamke na mabadiliko mengine na hata kwa wanaume mabaliko uanza ya uzazi na hasa upande wa homoni uweza kujiweka sawa katika mfumo wa uzazi.

Hapa mtu uweza kujiona amekuwa zaidi ya hali halisi ilivyo uweza kujifananisha na mwanaume yeyote au mwanamke yeyote na kuona hakuna utofauti kutokana na mabadiliko ya mwili wake ya mefanana na mtu yeyote ukizingatia maneno anayopewa na watu wengine mathalani wewe sio mtoto ona kifua kimejaa, nyonga na vitu vingine hivyo mtu uweza kuona kweli amekuwa na kuwa na anauwezo wa kufanya mambo ya kikubwa yaani vile mkubwa anavyofanya nae anaweza kufanya pasipo kuanagalia na hiyo hatua watu wote wameipitia lakini uweza kujiona kuwa yeye ndio wa kwanza kupitia hatua hiyo hivyo uweza kuwa huru kufanya kile anachojisikia pasipo kuangalia uhalisia wake.

Hatua hii watu wengi upotea kutokana na kiburi, kujiusisha katika uvutaji wa sigara na hata ukahaba na mwisho kujikuta na matokeo tofauti na vile alivyofikiria……….majuto na kukata tama uanzia hapo.

Usijali fuatana nami katika hatua inayofuata……………………………………..!!!

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni