MAMBO
YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;
Tukiwa tunaendelea
katika uwanja wetu wa MAUSIANO kwakua ndani ya ulimwengu wa sasa kumekuwa na
tabaka mbili kati waliobebwa na mausiano ya kimapenzi na wasiobeba na mausiano
ya kimapenzi bali wanaojiongoza katika utashi wao, na leo tunaingia katika
sehemu ya sita (6) kwa hakika tunaelekea mwishoni wa som letu lakini huu mwisho
ndio unaokamilisha mwanzo………….kwakua kila lenye mwanzo lina mwisho na basi
pasipo mashaka basi lenye mwisho basi lilikuwa na mwanzo……..barikiwa na karibu
tena!
IV.KIBALI
KATIKA MOYO WAKO
Hii ni moja ya sababu
ya watu walio wengi katika kuingia na kutoka katika mausiano ya kimapenzi katika hili
utasikia kauli nyingi sana mathalani”SIJISIKII KUWA NAE”, “ YAANI MOYONI MWANGU
HAYUPO KABISA”, YAANI PALE…. HAKUNA CHA KUNISHAWISHI HANA PESA WALA MVUTO” na
mengine mengi ambayo naamini msomaji unayajua kama ujawai kusema moyoni mwako
basi umesikia na hata kuambiwa kama ujasikia kutoka katika mtu mwingine.
Na kubaliana kabisa
kuwa mausiano mazuri yanategemea sana kibali toka katika moyo wako, na
tunapozungumzia hali ya moyo kuwa na kibali na mtu huyo hapo tunazungumzia hali ya moyo wako kulizika
nae, lakini changamoto inakuja pale tu sababu za kuushawishi moyo wako
katika kuridhika nae zinamsingi wa kutosha katika kuimiri suluba za ndoa na kufanya uendelee kumpenda na kumuona bora
kuliko ulivyomuona jana………hapa ni swali ambalo moyo wako utaweza kujijibu pindi
utakaposema ndio au hapana!
Kwakua tumeona watu
wengi sana waliwapa kibali watu katika moyo wake na baadae akashindwa kuimiri
shuruba za ndoa na mwisho sijui ilikuaje ghafla tukaona amemtoa mtu katika moyo
wake na baada ya kumtoa katika moyo sijui lilibaki wazi au nafasi ilichukuliwa
na mtu mwingine!
Ndomana nasema kwamba
mtu kupata kibali katika moyo wako ni jambo la muhimu sana lakini inaweza isiwe
sababu ya kuchipua uhusiano wa kimapenzi kwakua hiyo pekee haijitoshelezi na
ukumbuke wewe unakuwa sio wa kwanza lakini mwisho wake unakua tofauti na vile
ulivyotegemea kwa maana unahitaji kuwa na kitu cha kukamilisha ikakuweke katika
mazingira salama yaliyo na matumaini katika maisha yako ya sasa na ya baadae.
Ni vizuri kuwa makini
sana kwa wakati ulionao sasa kwani hatua ikitokea umeikosea basi kinachofuata
ni majuto alama ambayo inaweza kuwa na nguvu ya kukurudisha nyuma kila mara
utakapotaka kupiga hatua ya kuleta maendeleo katika maisha yako.
Katika hatua hii
kunaweza kukupelekea kuwa tajiri au kuwa masikini uliokithiri na sijui
utamlaumu nani? Lakini katika mzuri unaweza kujipongeza katika maamuzi ulio ya
chukua lakini unahitaji wewe kuyabeba maisha yako na sio maisha ya kubebe wewe
kwakua yenyewe hayajui kule unatakiwa kwenda bali wewe katika hali stahili
unajua ulikotoka na unamalengo mema katika kukufikisha hatua moja iliyo na
hatima njema katika maisha yako
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson………………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni