Jumanne, 19 Mei 2015

UPEPO UNANIPOTEZA



UPEPO UNANIPOTEZA


Upepo ni kitu chema sana na ni kitu kizuri kwani ndani yake hakuna ubaya uliobebwa ndani yake , tangu ulipoamliwa kuwepo haukubeba ubaya wowote….. wala muumbaji wa huo upepo hakuwa na kusudi baya ndani yake……..japo inategemea uko upande gani katika wepesi au uzito stahili kwani upepo umekuwa kero kwa wengine na wengine kuwa kiburudisho mathalani kwa wale walioanika nguo upepo una uzuri wake lakini kama ikitokea una nguvu unaweza kukuta nguo mahali zilipo hazipo tena ikawa huzuni badala ya kufurahia hewa safi inayopatika!!

Ninapozungumzia UPEPO hapa na zungumzia hali ya wakati na kukubaliana na huo wakati ni kama vile nguo zinaposhindwa kuimiri kishindo chake basi uondoka sawasawa na upepo unapotaka kwenda pasipo kujali ulikuwa tayari au sio kwa utayari!!

Na ninapo zungumzia UPEPO na zungumzia mambo  mbalimbali yanaendelea katika dunia yaliyojaa mapinduzi mengi na hata kufanya yaliyo halali kufanya sio ya halali na hata kinyume chake ni kama vile upepo umekusanya mambo mengi sana…… vitu vingi vinabebwa na upepo alafu vinaachwa pasipo kurudi tena katika hali yake ya awali lakini pindi nguvu inayo kuja pale wakati inakung’oa utafikiri haitakuacha lakini inakuacha pasipo kujali utaendeleaje au utaponaje! Katikati pasipo muelekeo laiti ungeuona mwisho kabla ya mwanzo usingekubaliana kwenda na nguvu zake.

Lakini sasa mambo yanayo endelea katika dunia ni kama upepo yanakuchukua kwa nguvu na kukuacha mahali ambapo uweza kwendelea na hata kujua kama utakuwa hapo ndomana katika mwisho katika mambo ya kidunia mwisho wake tunaona vijana wakijingiza maisha yasiyo na mfumo maalum na mwisho ujikuta wamepata magonjwa ambayo ni pigo katika maisha yao na hatimae kufa na kukatisha ndoto zao, wako wengine kwakushindwa kuimiri wanajikuta kupata shinikizo la damu, msongo wa mawazo(stress) na wengine kupata mimba na kuiharibu na hata wengine kuitwa mama wakiwa wadogo na wengine hata kuthubutu kutoa kujiua.

Katika dunia kumekuwa na mitindo mingi(style) za namna ya kumtega mtu ili kumpata na hatimae awe mpenzi wako (mwanamke au mwanaume wote wanaweza kufanya) na hivyo watu wamekuwa na bidii katika kujifunza na bidii katika hilo……..ndoma mambo yote yahusiyo mapenzi yanamvuto mkubwa katika jamii yetu iwe muziki au vitabu na hata majarida mambo yote haya yanajaza katika akili ya watu na watu kuyafanya kuwa ni maisha yao.

Mbaya zaidi waliowateule wamechukua nafasi katika kujinza namna ya dunia inavyofanya na hata kuwa waumini wakubwa wa mambo hayo kuliko hata wanagiza kusema na kuona kwamba upepo wa dunia umekuwa na nguvu hata kuliko upepo wa Mungu…………..hapa na zungumzia upepo kama mambo yahusiyo dunia yamekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mambo ya nuru.

Ni kisema usiyatazame nitakuwa muhongo lakini kubwa ningependa kujua kwa ufasaha zaidi wa mambo yaliyo bebwa na dunia kuwa hatima yake ni KUKUPOTEZA KATIKA KUHATAMIWA NA MUNGU! Lazima ujue yaliyo ndani ya Mungu hayo mengine utayajua kwakua ndani ya Mungu kuna hazina ya kutosha.

Ukienda kinyume na dunia kunauwezo mkubwa kwenda sawa na Mungu lakini ukienda kinyume na Mungu ni wazi utakuwa kinyume na Mungu ndoma dunia inakumeza kwakua uko nje ya utawala wa Mungu.

Ni vizuri uweke maisha yako SALAMA  kwa Mungu ndio asili ya USALAMA na penda ni kuhakikishie hakuna aliyeyaweka maisha yake katika mikono salama ya Mungu na mwisho akashindwa KUSTAWI,

Imeandaliwa na;


Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni