KESHO
YANGU
Ni kweli KESHO ni kitu
cha ajabu sana……kwani ndio utofauti wa pekee kati ya JANA na LEO.
Kwakua atuijui kesho
ndomana tunaishangaa pindi inapokuja siku hiyo! Katika hali ya furaha au huzuni
itategemea jinsi ilivyo na jinsi ulivyo!
Ninaweza kusema kuwa ni
kitendawili ambacho sio rahisi kukitegua kitendawili hiki japo hauwezi
kukitegua kwa kuangalia mwenendo wa maisha ya mtu mwingine wala katika mfano wa
kitu kingine bali kila kitu kina bebwa na WEWE.
Na swali litakujia na
kusema mimi ni nani?
Tukiachana na swali
hili niseme hakuna mtu anahitaji kesho yenye maumivu bali wote wanahitaji kuwa
na kesho yenye ubora na ustawi uliotimilifu.
Hata mtoto uwa anapenda
kuwa na wazazi wake milele…… lakini majira yalipo duniani haya ruhusu hali hii
itokee lakini katika yote bado tunasema vile
ilivyo ndivyo itakavyokuwa na sio vile unavyopenda!
Japo maamuzi yanabakia
kwako lakini matokeo yanategemea sana na kile ulichokichagua na sio kitu
kingine!
Laiti
ni ngelijua kesho…….nisingelia leo, nisingelikubali….., nisingelicheka….,
nisingelitafakari……., nisingeliamini……,nisingeliacha……,nisingelihuzunika….,
nisingelichukia….., nisingelighairi….. na hata nisingetoa chozi!!!!
Haya ni maneno
yanayonenwa na mtu mwenye akili timamu na mara nyingi haya maneno ubeba uhalisia
mkubwa wa moyo wa mtu, na wakati mwingi haya maneno hayasikii katika masikio ya
kawaida bali uweza kusikia katika masikio ya moyo wa mtu husika. Na muda mwingi
maneno haya unenwa katika hali ya utulivu sana sio wa kimazingira tu bali hata
moyo, akili na mwili uwa na hali ya utulivu usioweza kuelezeka.
Haya ni maneno ambayo
yananenwa baada ya maamuzi fulani uliyo yaamini na kuyakubali na hatimae
yakakuweka katika nafasi ya kusema haya maneno haya………japo dhamira hasa ya
ujumbe huu ni kuonyesha mtu kuamua jambo ambalo moyo ulikupa tumaini jema na
kusindikizwa na msukumo wa moyo wako ukiambatana na utashi wa akili zako na
hatimae ukakuweka katika mazingira uliyonayo sasa inawezekana katika kucheka au
kuhuzunika!
Katika hali ya
kuhuzunika mtu anaweza asione kama kunakwendelea na safari mathalani mtu
aliyeingia katika ndoa na kuambikizwa UKIMWI na hata kupata ulemavu wa kudumu
na inawezekana ulikuwa na mtu ambaye ulimwamini sana ukafanya nae biashara
shirika lakini mwisho akakusaliti hali hii inaweza kuwa nzito sana na kuona
giza kana kwamba hakuna muongozo utakaotoa mwanga mwingine!
Niseme wazi kuwa haya
ni maneno ambayo hayasemwi kila wakati kwani sio maneno ya kuvutia sana kwakua
katika wengi haya maneno yamebeba maumivu makali sana yasioweza kuelezeka hivyo
hauwezi kukuta mtu anayaongea maneno haya katika furaha hasa Yule maamuzi yake
yaliyo mpelekea katika upande hasi!
Japo naweza kusema kila
jambo linaweza kuwa na hatua ambayo inawezakuwa ni vigumu tu katika kuanza upya
au msukumo mwingine katika hatua iliyo njema na mtu uweza kuamua na kufanya
jambo ambalo ukulitarajia wala kulitegemea!!
Niseme kwa Mungu
kunakuanza upya tena upya ulikushamiri na wenye mng’ao wa kimungu uliambata na
utiisho wa Mungu.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson………………………………………………..0764 018535
KESHO YAKO INAWEKWA NA MIKONO YAKO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni