ISHI KWA SIKU
Ni muhimu kwanza kwako
wewe uipende siku na uhitazamie kuwa ni siku njema ambayo itakuwa na mchango
mzuri katika maisha yako…… hakikisha unamtazamo sahihi sana katika hiyo siku,
kwakua hiyo ni siku yako basi ifanye kuwa njema sana na ya maana sana katika
maisha yako.
Niseme wazi kama siku
unahitaji basi hauna budi uithamini na huone kuwa wewe ni mmoja kati ya
waliopendelewa katika siku hiyo, hivyo lazima uone ni huruma za Mungu katika
maisha yako na uone upendo wa Mungu katika hilo.
Usiruhusu kila kitu
kiwe na mwendelezo katika maisha yako hasa kitu kilichoenda kinyume na
matarajio yako……usikubali kuwa mtumwa wa makosa uliyo yafanya ili ya kuendeshe
katika maisha yako.
Tamani kuona hata kama
jambo alijawezekana leo lakini ipo siku itawezekana kwakua unatumia njia zilizo
na maarifa mengine na katika uwezo mwingine!
Utakiwi kuchoka mahali
ambapo siku inakuweka moyo wako kuwa chini na wala utakiwi kuwa juu maadam
mambo yako yameenda vizuri bali katika yote jua hakuna kinachoweza kufanyika
kinyume na kusudi lile ulilolibeba.
Ona siku haina maaana
ila wewe ndio una maana uonyesha katika siku kuwa wewe ni wa maana kuliko yeye
kwakua kuwepo kwake kunakutegemea wewe………ulimwengu uliumbwa kwa sababu ya wanadamu
na sio wanadamu waliumbwa kwa ajili ya ulimwengu!
Siku haina mipango yake
yoyote ila inamtegemea mwenye siku mwenyewe ambaye ni wewe hivyo siku ikiwa
mbaya kwa mtazamo wako usijute na kuilaumu hiyo siku kama ni sababisho, kwakua tumekuwa na hulka au mtazamo siku hizi hasa
katika kuilaumu siku na kumuona Mungu kuwa hayuko pamoja nasi! Na pindi mambo
yanapokuwa mazuri basi wote tuna sema kwakuwa siku hii imeanda vizuri na
tunaamini kuwa Mungu ametuona hivyo mioyo yetu inakuwa imejaa shukrani sana
kuliko kitu kingine na niseme wazi kuwa hiyo ni kawaida ya wana waulimwengu
lakini nisingependa iwe ndio kawaida hata ya watu walio wake wa imani yao katika Mungu wa kweli
Lazima utambue kuwa
kila siku inakuja na upekee wake na matokeo yake, hakuna siku inakuja au
unayopata kibali pasipo kuwa na kusudi lake ila inawezekana usilijue lakini
kila siku inabeba kusudi lake…………!!
Unapoishi kwa siku ni
uwanja mzuri wa kumuona Mungu katika moyo wa shukrani kwani utamuona Mungu sana
maadam siku imekwisha haijarishi ni siku njema au siku mbaya lakini katika yote
utaona bado Mungu ni mwema sana……kwakua ni kawaida ya wanadamu ya kutoridhika
na hao ufurahia siku maadam imeisha katika mipango yake kutimia vizuri.
Katika siku moja tambua
kuwa huo ni msingi mzuri wa kufikia au wakufanikisha siku inayofuata kwakua
maandalizi mazuri ya leo ndio ubora wako wa kesho kwani vyote viko katika
mawanda yako.
Siku inaratibiwa na
mipango yako katika siku hiyo na hiyo ratiba ya siku inafuata na mtu ambaye
amebeba hiyo siku kwakua uliyeipanga hiyo ratiba ya siku usipoiheshimu ni wazi
hakuna mwendelezo mzuri wa ratiba na wala hakuna atayeiheshimu.
Napenda ujue kuwa
sekunde utengeneza dakika na dakika utengeneza saa na saa utengeneza siku kwa
vyote vinategemeana na endapo kimoja kikikosea basi kitasababisha kingine
kiweze kutoa matokeo ambayo hayako sawa.
Itunze siku yako maana
ndio fahari yako!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni