USALAMA WA NEEMA
Unaposikia
neno SALAMA bila shaka moyo wako na macho yako yanakuwa na matazamio yaliyo
mema na ubora na hali ya kufaa na mahali kwa hakika ungependa ukae milele….na
laiti pangekuwa na mtu ambaye anaitw SALAMA sio kwa jina tu bali hata katika
matendo yake basi watu wengi wangetamani kuwa karibu yake na kama angekuwa ni
binti basi vijana wengi wange tamani wawe
nae kwakua wanaamini watakuwa salama na angekuwa ni kijana wa kiume basi
mabinti wengi wangetamani wawe nae kwakua hakuna mtu apendi kuwa mahali salama.
Kuna
vitu viwili napenda kuviongelea kuna usalama wa kufikirika na usalama wa
kuonekana hivi ni vitu muhimu sana katika kuangalia kwa namna ya kiupekee
kwakua sio kinachoonekana ni salama basi ni salama kweli na sio kila kitu kinachofikirika
si salama basi hakina usalama wa kweli…..wako watu walizani wako salama mahali
Fulani lakini mwisho wakaona ni tofauti kabisa na walivyo tegemea!!!
Mathalani
mtu anaweza kupata kazi ambayo moyo wake uliipenda sana na moyo wake ukaipenda
ile kazi na hata mzingira ya ile kazi yakamvutia sana basi akaona hapo alipo ni
mahali salama sana lakini mwisho akajikuta katika mazingira ambayo
akuyategemea….mathalani kifungo gerezani, ukimwi, chuki na hata kupoteza sehemu
ya viungo vyake na hata kufa.
Ni
seme usalama wa kweli sio rahisi kugundua unaweza kuona mtu anakupenda sana
kiasi kwamba ukaona umeshafika lakini ukweli ujajua ni kitu gani kimemshawishi
yeye akupende na je! Hii ndio sababu ya msingi katika mapenzi ya kweli! Hiii ni
zaidi ya hatari sana pindi unaposhindwa kutambua ukweli wa jambo gani hasa
limemvutia kwako unaweza kuwa sehemu ukaona uko salama lakini sio salama kwa
vile inavyo onekana kwa macho ni tofauti kabisa na itakavyo tokea!!! Ndomana
katika moja ya ujumbe ninazo zipenda inaitwa ……laiti ningelijua kesho!!
Uwa
tunaingia katika ushirika tukitumaini kuwa ni mahali salama sana mfano katika
katika biashara, uchumba na hata urafiki wa kawaida….mwisho wake uwa tofauti kabisana
na matarajio yako na ila ya naweza kuwa na matarajio ya mwingine aliyekaribu
yako mathalani kukuambukiza ukimwi, kukuachanisha na mtu unaye mpenda na hata
kukuachanisha na kazi na wengi hata katika kukupelekea katika kifo chako.
Ni
seme wazi katika dunia ya sasa ni ngumu sana kuwa makini mahali ambapo
utafikiri kuwa uko salama bali wengi wao ujifunza baada ya kuharibu na wakati
mwingine inakuwa ni ngumu kurudi JANA yako hivyo inabaki kuwa ni historia
inaweza ni machozi kila ukiyakumbuka!
Japo
zipo changamoto katika ushirika wowote lakini namna mtakvyozitimiza zinategemea
sana namna mnavyomaliza inategemea sana MSINGI WA USHIRIKA WENU. Siwezi kukudanganya katika hili mwanzo
wa ushirika ndio mwanga au giza katika ushirika wenu!
USALAMA
WA NEEMA!!! Hapa na zungumzia usalama unaomabatana na Mungu mwenyewe huo ndio
usalama ulijawa na muambatano ulio bora na salama sana ambao kila ushirika
wowote usio sahihi hautaweza kuunganishwa kwako kama ujapata kibali kwa Mungu!
Hautaji
kua mkali sana wala mpole sana bali wewe hakikisha kuwa usalama unajikita
katika neema ya Mungu sio neema au huruma ya mtu yeyote kwakua katika yeye
hakuna hatima iliyo njema sana,
Jifunze
kuona maisha yako yana kuwa na kibali kwa Mungu zaidi ya kuwa na kibali kwa
wanadamu, tamani kuona sana tabasam la Mungu wako kuliko tabasam la mtu yeyote!
Tamani sana kuona furaha ya Mungu katika maisha yako!
Unahitaji
kumpa Mungu fursa ya kutosha sana ili awe mwamuzi katika maisha yako na ndipo
hapo usalama unaweza kutokea na kuwa matunda mema katika maisha yako!
Ukianza
na usalama wa mbingu basi usalama mwingine utakuwa wa maana sana pasipo hata
kuomba wala kutafakari sana kwakua katika yeye kuna kila kitu! Na kamwe hawezi
kukupoteza kwa kua ukimwendea yeye utakuwa salama!
SALAMA NI ASILI YA
MUNGU!!!
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni