HITAJI
HITAJI LA MTU NI SIRI YA MTU
Naweza kusema ni
ugonjwa wa MOYO na ni mateso ya AKILI pindi unapolisikia neno hili HITAJI, hasa
panapokosekana na uwezekano wa kulikabili neno hili HITAJI, katika jambo hili
pamezaliwa vitu vingi sana mathalani ndoa, urafiki, uadui, mateso na hata
furaha ya kitambo.
Ni kweli unatambua
uhitaji ulionao kwa uhalisi au kunaushawishi mwingine ambao unakupa msukumo wa
wewe kuona uhitaji! Katika haya unaweza ukaambiwa au kujua hasa wewe unahitaji
nini? Hivyo lazima utambue msingi wa uhitaji wako umebebwa na nini?
Nipende kusema kwamba
kila rika katika ukuaji wa mwanadamu na katika hali stahiki kunauhitaji wake
ambao kiukweli unaweza kuwa tofauti mkubwa au sio mkubwa katika hatua nyingine.
Ni kuulize swali moja
tu unaelewaje neno hili HITAJI? Bila shaka unaweza kuwa na jibu zuri sana
ambalo moyo wako utaliamini na kulipenda sana kwakua ni jibu lako! Na hakuna
ataye kurekebisha au kukupinga kwakua ndicho kitu unachokiamini na kuona fahari
katika hilo.
Katika hatua za
mwanadamu;
i.mtoto aliye ndani ya
tumbo la mama
ii. mtoto aliyetoka
ndani ya tumbo la mama
iii.kijana
iv.mtu mzima
v.mzee
katika hatua zote hizo
kuna mahitaji maalum ambayo kila hatua inahitaji katika utashi wa nafsi yake ni
kubaliane na wazo hili kuwa kuna mahitaji ya msingi na mahitaji yasio ya
msingi, japo mahitaji ya msingi mtu anaweza kufanya yasiwe ya msingi na yasiyo
na msingi ya kawa na msingi kwa mtu husika.
Ni kubaliane kwa pamoja
kuwa wanaweza kuwa wanawake kumi wenye rika moja lakini kila mmoja anaweza kuwa
na hitaji tofauti tofauti kulingana na changamoto zinazo mkabili………wako watakao
hitaji nyumba bora, mtoto, mume, uponyaji(tiba), mali, amani, gari n.k na kila
mmoja hitaji atakalo kuwa nalo bila shaka wengine litakuwa linawatesa sana
kwakuto kuwa nalo na wengine watachukulia swala linalo hitaji muda zaidi kwa
kuwa na moyo wa uvumilivu.
Kwa wale ambao uhitaji
wao au wake utakuwa ukiwatoa machozi na ndani ya miyo wao wataamini kuwa kama
hitaji lake litafumbuliwa katika maisha yake bila shaka litachimbuka furaha na
kicheko kilicho jificha katika maisha yake.
Ukitaka mtu akuzarau na
kuona wewe sio kitu jaribu kuuzarau huo uwitaji wake ambayo kwa hilo yeye
anakosa usingizi, na kuzalisha mateso katika moyo wa mtu, lakini katika hili ni
kubaliane kuwa nguvu ya uhitaji utegemea akili yako na nani aliye karibu
yako……anaweza kuondoa mzigo uliondani yako.
Je! Ni kweli uhitaji
ulionao unaweza kukufanya uishi au kuishi ndiko kunaweza kukupa uhitaji
ulionao……uhai ni bora kuliko uhitaji!
Naamini kuwa uhitaji
wako ndio maumivu yako na inaweza kuwa furaha yako na naam inaweza kuwa huzuni
yako!!
Katika yote utambue
kwamba;
WEWE NI HITAJI LA MUNGU
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni