MAMBO
YA KUZINGATIA KATIKA MAUSIANO YA KIMAPENZI;
ASANTE….mpendwa msomaji
kwani tangu tulipoanza katika somo hili linahusu MAUSIANO ikumbukwe kuwa
sikuandika ujumbe ili kuchochea watu waingie katika mausiano katika hali ya
kukulupuka au kuharakisha mausiano…..bali kutokana na mateso na vifo na maisha
ya majuto yanayo wa kumba watu walio katika MAUSIANO kwa ujumla wao
BABA,MAMA,KIJANA na hata MTOTO…kubwa kuliko yote nikuhusishe WEWE BINAFSI
UJIWEKE KWA MUNGU.
Unaweza sema mbona
usiano wa watu wa nyuma ni tofauti kabisa na sasa kwani mwanzo mausiano
hayakuwa na matatizo kama hivi sasa….. bali ningependa kukutoa katika mawazo
hayo kukukwambia matatizo yalikuwepo japo yalikuwa ni tofauti na mateso yalipo
sasa hivyo si jambo la tofauti sana kwani kadili nyakati zinavyobadilika ndio
mambo mengine yanavyobadilika.
V.KIBALI CHA MUNGU
Hili ndio hitimo sahihi
kwa mtu ambaye anamwamini Mungu kwa dhati na kuruhusu maisha ya Mungu kuishi
ndani yake katika hali ya ujazo wa kimungu uliokamili. Ni seme tu hatua hii sio
lelemama kwani namna ya kuenda na jambo ni ngumu sana kwani wakati mwingine
inaweza kwenda kinyume kabisa na AKILI yako.
Kwa kifupi haya ni
mausiano ambayo uwa kwa asilimia zote 100% yana dumu sana kuliko yote lakini
jambo hili si rahisi na kwa kusema hivi haina maana kuwa hamtatofautiana wala
kupishana la asha yote yatatokea na hata kuzidi hayo lakini kubwa kuliko yote MIOYONI
hawezi kutoana kamwe.
Ni seme hapa ndio ndoa
inaanza na inakuwa ya maana sana kwani KIBALI kinaanza kutawala katika kila
mnachokifanya kina tawala na neema ya Mungu kwa asilimia zote na machozi yenu
yana kuwa machozi ya Mungu mwenyewe na hata furaha yenu inakuwa furaha yake na
hapo ndio fursa nzuri ya vipawa na huduma ambazo ameziweka ndani yenu kuanza
kufanya kazi katika ufanisi mkubwa.
Wakati mwingi katika
kibali cha Mungu kinaweza kisiwe kibali katika macho yako na endapo nguvu ya
macho ya nyama yakawa yananguvu kuliko macho ya rohoni ni wazi kupata na kudumu
katika kitu sahihi si kitu rahisi.
Mungu uwa anangalia
sana wakati wa mwisho kuliko mwanzo kwakua katika mwisho mzuri ndio ujenga
ushuhuda ulio bora na wenye maana sana kwa Mungu kwani katika yeye kuna kila
kitu ambacho wewe unakihataji.
Ni muhimu kutambua kuwa
MUNGU ANAKUPENDA KULIKO VILE UNAVYO ZANI kwakua yeye alikujua na hakika
aliyekutunza tangu awali na kamwe hawezi kukuacha uhaibike alipokuumba hakuwa
na JAMBO baya nawe kama ukiamua kumfuata na kumsikiliza kamwe hauta weza
kushindwa kufika SALAMA!
Yeremia 29:11
Najajua mawazo ninayo wawazia ninyi
sio mabaya bali kuwapa tumaini siku zenu za mwisho!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
********************MWISHO**********************
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni