Alhamisi, 14 Mei 2015

JANA INANISUMBUA



JANA INANISUMBUA,


 Ni rahisi kujikinga kwa jambo ambalo alijatokea kuliko jambo ambalo limeshatokea ndomana watu usema KINGA NI BORA KULIKO TIBA, wakati mwingine  mtu anawezafanya jambo ambalo hajui kwa uhakika hasa matokeo ya jambo hilo ndomana mwisho wa jambo unaweza kumkuta mtu anasema laiti NINGELIJUA! Ni singelifanya jambo kama hili hasa kwa jambo baya ambalo linamfanya mtu moyo wake kuwa chini.

Wako walikatika NDOA wanalia na kujuta kuolewa au kuoa na mtu wanaoishi nao wako watu wanaonabora wangekaa kama walivyo tu pasipo kujihusisha na jambo lolote hasa katika swala la mausiano…. mathalani katika NDOA mwenzi moja anapokosa kuwa mwaminifu na kumletea mwenzie magonjwa mfano UKIMWI(ushuhuda wa kweli) mwanamke aliambikizwa na ugonjwa huu na mume wake kutokana na kushindwa kuwa mwaminifu, na mwengine anaolewa na mtu mwenye uwezo mzuri ajui msingi wa fedha zake lakini mwisho wake anakuta mwanaume au mwanamke anakamatwa kwa tuhuma za madawa ya kulevya au jambazi.

Sio hao tu pia wapo wafanyakazi wengi wanajuta kwa kufanya kazi mahali wanapofanya kazi mathalani wasichana wanalazimishwa kufanya mambo ambayo kwa uhalisi wake anajua sio haki mathalani kuwa dhurumu watu kuandika taarifa feki na kusababisha mateso kwa mtu na familia yake na wako watu ambao waliomba kazi wakitegemea au kufikiri kazi hiyo ni halali na kile kinachotambulishwa na hiyo kampuni kumbe sicho anajikuta kujiingiza katika hali ya ubazilifu wa mali ya umma mbali na hayo wako mabinti na vijana wengi wakipoteza ndoa zao kwa sababu ya mabosi zao.

Ni seme wazi katika hili JANA INANISUMBUA ni kweli jana inaweza kukusumbua kunaweza kuwa katika katika UJINGA WA MTU au MSUKUMO USIOKUWA UTAYARI BINAFSI na hatimae kupelekea maisha yake kuwa kama jinsi yalivyo.

Mathalani ajari inamkuta  mtu na kupoteza baadhi ya viungo vyake mathalani macho,miguu na hata mikono na kusababisha yale aliyokuwa anayafanya kushindwa kuyafanya tena kutokana na utofauti aliokuwa nayo hili ni hali isiyohusishwa na utayari wa mtu…..niseme neema ya Mungu izidi kuwa juu yako!

Tundwe mbele na kurudi nyuma tuseme kila jambo ambalo limekufanya uwe hapo ulipo leo lazima na liweke kumbukumbu katika maisha yako inaweza kuwa ni njema ikazidi kukupa matumaini au mbaya ikazidi kukupa huzuni pindi unapoliikumbuka tu………na wakati mwingi katika jambo baya limesababisha msongo wa mawazo (stress), kubwa sana inatubidi tutafute suluhisho ili maisha yaendelee na sio kwendelea tu katika hali njema yenye ubora wake!

MWANGA WA MUNGU!

Ukweli tunamwihitaji Mungu wakati wote ili mradi maisha yanaendelea na hata yasipo ondolewa, unaweza ukajitaidi sana kumudu katika akili zako na hata kutumia taasisi katika kukushauri bado utakuwa na chembechembe katika ufahamu wako,

Na bado katika hali tumeona wako watu wamekuwa wakishindwa kumudu na hasa mambo mengine yanapoongezeka na wengine upelekea katika kujinyonga au kujiua katika namna nyingine yoyote………inasikitisha kwakua wengine walikuwa na potential katika kuisaidia jamii katika kuwatibia hama kuwaongoza katika kuwafanikisha katika hatima zao.

Mwanga ulijaa Mungu ndio suluhisho la kudumu mathalani akili iliyomjaa Mungu mathalani YUSUFU alimuona Mungu katika kila jambo alilokuwa akilipitia haijalishi ilikuwa inapicha hipi katika jamii inayomzunguka yeye alichokiangalia ni namna Mungu anavyhusika katika maisha yake!

Mungu ndiye aliyekuwa na spea zote za mwili wako na ndiye anaweza anaweza kurekebisha kila kitu au spea zilizo athirika na kuzifanya ziwe bora, amua kumfanya MUNGU kuwa na nafasi ya kipekee katika maisha yako kwa kumfuata kwa ukamilifu mbele zake!

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni