UPEPO UNANIPOTEZA
Upepo ni kitu chema sana na ni kitu kizuri kwani ndani yake hakuna ubaya uliobebwa ndani yake , tangu ulipoamliwa kuwepo haukubeba ubaya wowote….. wala muumbaji wa huo upepo hakuwa na kusudi baya ndani yake……..japo inategemea uko upande gani katika wepesi au uzito stahili kwani upepo umekuwa kero kwa wengine na wengine kuwa kiburudisho mathalani kwa wale walioanika nguo upepo una uzuri wake lakini kama ikitokea una nguvu unaweza kukuta nguo mahali zilipo hazipo tena ikawa huzuni badala ya kufurahia hewa safi inayopatika!!
Ninapozungumzia UPEPO
hapa na zungumzia hali ya wakati na kukubaliana na huo wakati ni kama vile nguo
zinaposhindwa kuimiri kishindo chake basi uondoka sawasawa na upepo unapotaka
kwenda pasipo kujali ulikuwa tayari au sio kwa utayari!!
Na ninapo zungumzia
UPEPO na zungumzia mambo mbalimbali
yanaendelea katika dunia yaliyojaa mapinduzi mengi na hata kufanya yaliyo
halali kufanya sio ya halali na hata kinyume chake ni kama vile upepo
umekusanya mambo mengi sana…… vitu vingi vinabebwa na upepo alafu vinaachwa
pasipo kurudi tena katika hali yake ya awali lakini pindi nguvu inayo kuja pale
wakati inakung’oa utafikiri haitakuacha lakini inakuacha pasipo kujali
utaendeleaje au utaponaje! Katikati pasipo muelekeo laiti ungeuona mwisho kabla
ya mwanzo usingekubaliana kwenda na nguvu zake.
Lakini sasa mambo yanayo
endelea katika dunia ni kama upepo yanakuchukua kwa nguvu na kukuacha mahali
ambapo uweza kwendelea na hata kujua kama utakuwa hapo ndomana katika mwisho
katika mambo ya kidunia mwisho wake tunaona vijana wakijingiza maisha yasiyo na
mfumo maalum na mwisho ujikuta wamepata magonjwa ambayo ni pigo katika maisha
yao na hatimae kufa na kukatisha ndoto zao, wako wengine kwakushindwa kuimiri
wanajikuta kupata shinikizo la damu, msongo wa mawazo(stress) na wengine kupata
mimba na kuiharibu na hata wengine kuitwa mama wakiwa wadogo na wengine hata
kuthubutu kutoa kujiua.
Katika dunia kumekuwa
na mitindo mingi(style) za namna ya kumtega mtu ili kumpata na hatimae awe
mpenzi wako (mwanamke au mwanaume wote wanaweza kufanya) na hivyo watu wamekuwa
na bidii katika kujifunza na bidii katika hilo……..ndoma mambo yote yahusiyo
mapenzi yanamvuto mkubwa katika jamii yetu iwe muziki au vitabu na hata
majarida mambo yote haya yanajaza katika akili ya watu na watu kuyafanya kuwa
ni maisha yao.
Mbaya zaidi
waliowateule wamechukua nafasi katika kujinza namna ya dunia inavyofanya na
hata kuwa waumini wakubwa wa mambo hayo kuliko hata wanagiza kusema na kuona
kwamba upepo wa dunia umekuwa na nguvu hata kuliko upepo wa Mungu…………..hapa na
zungumzia upepo kama mambo yahusiyo dunia yamekuwa na ushawishi mkubwa kuliko
mambo ya nuru.
Ni kisema usiyatazame
nitakuwa muhongo lakini kubwa ningependa kujua kwa ufasaha zaidi wa mambo
yaliyo bebwa na dunia kuwa hatima yake ni KUKUPOTEZA KATIKA KUHATAMIWA NA
MUNGU! Lazima ujue yaliyo ndani ya Mungu hayo mengine utayajua kwakua ndani ya
Mungu kuna hazina ya kutosha.
Ukienda kinyume na
dunia kunauwezo mkubwa kwenda sawa na Mungu lakini ukienda kinyume na Mungu ni
wazi utakuwa kinyume na Mungu ndoma dunia inakumeza kwakua uko nje ya utawala
wa Mungu.
Ni vizuri uweke maisha
yako SALAMA kwa Mungu ndio asili ya
USALAMA na penda ni kuhakikishie hakuna aliyeyaweka maisha yake katika mikono
salama ya Mungu na mwisho akashindwa KUSTAWI,
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535