Jumatano, 24 Juni 2015

NAOMBA JANA RUDI



NAIOMBA JANA

Unaweza kuzani kuwa ni kama ndoto au kitu ambacho akiwezekana kwani sio kawaida mtu kuomba jana irudi! Lakini ni jambo ambalo watu wanaomba ila wakati mwingine inakuwa ngumu sana kuirudisha jana ikawa leo au kesho ikawa jana kwakua imeshapita na mbaya zaidi inakuwa imepita na mambo yake ila inaacha alama ambayo kuonyesha kuwa ilishapita!

Mtu anaweza kuomba ombi hili endapo tu atakapo ona leo yake imekuwa ni tofauti na vile alivyotegemea yamkini aliona kutakuwa na manufaa zaidi lakini mwisho akaona hakuna unafuu wowote zaidi ya majanga na mateso tu wala hakuna unafuu wowote hivyo utamani kuona jana mrudie tena ili aweze kufanya tena maaamuzi yatakayo mmletea mwanga mzuri!

Sio jambo jema sana kwa mtu kukumbuka watu waliotangulia (kufariki) kuona kama wangekuwepo leo nisingekuwa hivi nilivyo japo uwezi kuzuia hisia za mtu kutokana na kukosa mahitaji fulani na hivyo kupelekea katika hali duni au isiyopendeza macho pake!

Katika swala hili wako watu ambao wanaiomba jana irudi kutokana walicheza/awakufanya vizuri pindi alipokuwa shule,au akumthamini mtu fulani na hatimae akawa bora kuliko yeye…pia wako watu wanalia juu ya viungo vyao baada ya kupoteza kwasababu mbalimbali mathalani ajari katika kazi au safari za kawaida wengine wamepoteza miguu,mikono na hata macho na wengi wao wanatamani sana kama siku zao zingejirudia tena wangefanya vizuri zaidi ya vile walivyofanya.

Katika jana kuomba irudi kuna wako watu walio wakimbia wenzi wao kwasababu mbalimbali zikiwemo umaskini, wakizamani, hana muonekano wa kuvutia au hajakizi vigezo vyake hivyo awezi kuendana nae na pindi baada ya kumwacha yule na kwenda kwa wengine hali huko ikawa mbaya sana na kutamani yule wa mwenzi wa mwanzo arudi tena kwake na wakati mwingine inakuwa ni ngumu tena kuirudia jana kwani mazingira yanaweza yasiruhusu tena katika kurudiana………….ikabaki kilio tu na kujilaumu tu na zaidi sana kuwa na maisha ya majuto siku zote.

Unaweza kuona kuwa ni kitu rahisi ukikaa na kutafakari kwa haraka pasipo kina basi bila shaka lakini ikifika kipindi jana yako ikawa mbaya na usione mwanga wa kutokea ndipo hapo utaanza kuyakumbuka yote ya jana pasipo kujali mapungufu yake na unaweza ukaishia kutamani tu lakini usiweze kuibadilisha jana ikawa leo au sasa!

Bila shaka kilio cha mtu au huzuni ya mtu uongezeka sana pindi anapoona ubora wa jana ulivyo tofauti na leo yake kwani ule utoshelevu wa jana haupo tena………lakini inakuwa ni furaha kwa mtu ambaye hakika jana yake ilivyokuwa ngumu sana na sasa leo yake imemjaa kicheko ambacho akina kikomo kamwe

Ni kweli walio wengi wanacheka leo inategemea sana maandalizi yao ya jana lakini sio wote wanalia leo jana yao hawakujiandaa inawezekana walijaandaa lakini hawakufikia lile lengo walilo kusudia au changamoto ikaibuka katikati akashindwa kutimiza ndoto yao.

Ni kweli maisha yako ya nyuma yana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya sasa kwani yanaweza yakaweka nuru au giza… hivyo kusema kila dakika unayo itumia ni mbegu matunda yake utayaona pindi muda wa kuchipua utakapofika!

Utakiwi kuishi maisha ya hofu sana ilikutaka kuwa na kesho isiyoihitaji leo irudi tena bali katika yote unachohitajika kuwa na maarifa sahihi katika kila jambo unalo lifanya acha kufuata mkumbo haijalishi nani yupo katika huo mkumbo bali heshimu maamuzi yako na kuyazingatia kwani huo ndio utambulisho wako…………kwakua kila kitu kitakachokutokea kitafanyika furaha kwako au hasara kwako kwanza kabla ya kutokea kwa mtu mwingine au katika jamii husika.

Unaweza kuwa wa maana kama ukisimamia kitu cha maana na unaweza usiwe wa maana kama hauta simamia kitu kisicho cha maana yote inakutegemea wewe na sio jirani yako! Tengeneza ajabu yako kuwa kweli na halisi sana.

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Jumanne, 16 Juni 2015

ISHI KWA SIKU



ISHI KWA SIKU

 Ni muhimu kwanza kwako wewe uipende siku na uhitazamie kuwa ni siku njema ambayo itakuwa na mchango mzuri katika maisha yako…… hakikisha unamtazamo sahihi sana katika hiyo siku, kwakua hiyo ni siku yako basi ifanye kuwa njema sana na ya maana sana katika maisha yako.

Niseme wazi kama siku unahitaji basi hauna budi uithamini na huone kuwa wewe ni mmoja kati ya waliopendelewa katika siku hiyo, hivyo lazima uone ni huruma za Mungu katika maisha yako na uone upendo wa Mungu katika hilo.

Usiruhusu kila kitu kiwe na mwendelezo katika maisha yako hasa kitu kilichoenda kinyume na matarajio yako……usikubali kuwa mtumwa wa makosa uliyo yafanya ili ya kuendeshe katika maisha yako.

Tamani kuona hata kama jambo alijawezekana leo lakini ipo siku itawezekana kwakua unatumia njia zilizo na maarifa mengine na katika uwezo mwingine!

Utakiwi kuchoka mahali ambapo siku inakuweka moyo wako kuwa chini na wala utakiwi kuwa juu maadam mambo yako yameenda vizuri bali katika yote jua hakuna kinachoweza kufanyika kinyume na kusudi lile ulilolibeba.

Ona siku haina maaana ila wewe ndio una maana uonyesha katika siku kuwa wewe ni wa maana kuliko yeye kwakua kuwepo kwake kunakutegemea wewe………ulimwengu uliumbwa kwa sababu ya wanadamu na sio wanadamu waliumbwa kwa ajili ya ulimwengu!

Siku haina mipango yake yoyote ila inamtegemea mwenye siku mwenyewe ambaye ni wewe hivyo siku ikiwa mbaya kwa mtazamo wako usijute na kuilaumu hiyo siku kama ni sababisho, kwakua  tumekuwa na hulka au mtazamo siku hizi hasa katika kuilaumu siku na kumuona Mungu kuwa hayuko pamoja nasi! Na pindi mambo yanapokuwa mazuri basi wote tuna sema kwakuwa siku hii imeanda vizuri na tunaamini kuwa Mungu ametuona hivyo mioyo yetu inakuwa imejaa shukrani sana kuliko kitu kingine na niseme wazi kuwa hiyo ni kawaida ya wana waulimwengu lakini nisingependa iwe ndio kawaida hata ya watu walio wake wa  imani yao katika Mungu wa kweli

Lazima utambue kuwa kila siku inakuja na upekee wake na matokeo yake, hakuna siku inakuja au unayopata kibali pasipo kuwa na kusudi lake ila inawezekana usilijue lakini kila siku inabeba kusudi lake…………!!

Unapoishi kwa siku ni uwanja mzuri wa kumuona Mungu katika moyo wa shukrani kwani utamuona Mungu sana maadam siku imekwisha haijarishi ni siku njema au siku mbaya lakini katika yote utaona bado Mungu ni mwema sana……kwakua ni kawaida ya wanadamu ya kutoridhika na hao ufurahia siku maadam imeisha katika mipango yake kutimia vizuri.

Katika siku moja tambua kuwa huo ni msingi mzuri wa kufikia au wakufanikisha siku inayofuata kwakua maandalizi mazuri ya leo ndio ubora wako wa kesho kwani vyote viko katika mawanda yako.

Siku inaratibiwa na mipango yako katika siku hiyo na hiyo ratiba ya siku inafuata na mtu ambaye amebeba hiyo siku kwakua uliyeipanga hiyo ratiba ya siku usipoiheshimu ni wazi hakuna mwendelezo mzuri wa ratiba na wala hakuna atayeiheshimu.

Napenda ujue kuwa sekunde utengeneza dakika na dakika utengeneza saa na saa utengeneza siku kwa vyote vinategemeana na endapo kimoja kikikosea basi kitasababisha kingine kiweze kutoa matokeo ambayo hayako sawa.

Itunze siku yako maana ndio fahari yako!

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson……………………………………….0764 018535

Jumanne, 9 Juni 2015

USALAMA WA NEEMA



USALAMA WA NEEMA


Unaposikia neno SALAMA bila shaka moyo wako na macho yako yanakuwa na matazamio yaliyo mema na ubora na hali ya kufaa na mahali kwa hakika ungependa ukae milele….na laiti pangekuwa na mtu ambaye anaitw SALAMA sio kwa jina tu bali hata katika matendo yake basi watu wengi wangetamani kuwa karibu yake na kama angekuwa ni binti basi vijana wengi wange tamani wawe  nae kwakua wanaamini watakuwa salama na angekuwa ni kijana wa kiume basi mabinti wengi wangetamani wawe nae kwakua hakuna mtu apendi kuwa mahali salama.

Kuna vitu viwili napenda kuviongelea kuna usalama wa kufikirika na usalama wa kuonekana hivi ni vitu muhimu sana katika kuangalia kwa namna ya kiupekee kwakua sio kinachoonekana ni salama basi ni salama kweli na sio kila kitu kinachofikirika si salama basi hakina usalama wa kweli…..wako watu walizani wako salama mahali Fulani lakini mwisho wakaona ni tofauti kabisa na walivyo tegemea!!!

Mathalani mtu anaweza kupata kazi ambayo moyo wake uliipenda sana na moyo wake ukaipenda ile kazi na hata mzingira ya ile kazi yakamvutia sana basi akaona hapo alipo ni mahali salama sana lakini mwisho akajikuta katika mazingira ambayo akuyategemea….mathalani kifungo gerezani, ukimwi, chuki na hata kupoteza sehemu ya viungo vyake na hata kufa.

Ni seme usalama wa kweli sio rahisi kugundua unaweza kuona mtu anakupenda sana kiasi kwamba ukaona umeshafika lakini ukweli ujajua ni kitu gani kimemshawishi yeye akupende na je! Hii ndio sababu ya msingi katika mapenzi ya kweli! Hiii ni zaidi ya hatari sana pindi unaposhindwa kutambua ukweli wa jambo gani hasa limemvutia kwako unaweza kuwa sehemu ukaona uko salama lakini sio salama kwa vile inavyo onekana kwa macho ni tofauti kabisa na itakavyo tokea!!! Ndomana katika moja ya ujumbe ninazo zipenda inaitwa ……laiti ningelijua kesho!!

Uwa tunaingia katika ushirika tukitumaini kuwa ni mahali salama sana mfano katika katika biashara, uchumba na hata urafiki wa kawaida….mwisho wake uwa tofauti kabisana na matarajio yako na ila ya naweza kuwa na matarajio ya mwingine aliyekaribu yako mathalani kukuambukiza ukimwi, kukuachanisha na mtu unaye mpenda na hata kukuachanisha na kazi na wengi hata katika kukupelekea katika kifo chako.

Ni seme wazi katika dunia ya sasa ni ngumu sana kuwa makini mahali ambapo utafikiri kuwa uko salama bali wengi wao ujifunza baada ya kuharibu na wakati mwingine inakuwa ni ngumu kurudi JANA yako hivyo inabaki kuwa ni historia inaweza ni machozi kila ukiyakumbuka!

Japo zipo changamoto katika ushirika wowote lakini namna mtakvyozitimiza zinategemea sana namna mnavyomaliza inategemea sana MSINGI WA USHIRIKA  WENU. Siwezi kukudanganya katika hili mwanzo wa ushirika ndio mwanga au giza katika ushirika wenu!

USALAMA WA NEEMA!!! Hapa na zungumzia usalama unaomabatana na Mungu mwenyewe huo ndio usalama ulijawa na muambatano ulio bora na salama sana ambao kila ushirika wowote usio sahihi hautaweza kuunganishwa kwako kama ujapata kibali kwa Mungu!

Hautaji kua mkali sana wala mpole sana bali wewe hakikisha kuwa usalama unajikita katika neema ya Mungu sio neema au huruma ya mtu yeyote kwakua katika yeye hakuna hatima iliyo njema sana,
Jifunze kuona maisha yako yana kuwa na kibali kwa Mungu zaidi ya kuwa na kibali kwa wanadamu, tamani kuona sana tabasam la Mungu wako kuliko tabasam la mtu yeyote! Tamani sana kuona furaha ya Mungu katika maisha yako!

Unahitaji kumpa Mungu fursa ya kutosha sana ili awe mwamuzi katika maisha yako na ndipo hapo usalama unaweza kutokea na kuwa matunda mema katika maisha yako!

Ukianza na usalama wa mbingu basi usalama mwingine utakuwa wa maana sana pasipo hata kuomba wala kutafakari sana kwakua katika yeye kuna kila kitu! Na kamwe hawezi kukupoteza kwa kua ukimwendea yeye utakuwa salama!

SALAMA NI ASILI YA MUNGU!!!

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson………………………………………………….0764 018535

Ijumaa, 5 Juni 2015

JE! UNALITAMBUA HITAJI LAKO?



HITAJI
HITAJI LA MTU NI SIRI YA MTU

 Naweza kusema ni ugonjwa wa MOYO na ni mateso ya AKILI pindi unapolisikia neno hili HITAJI, hasa panapokosekana na uwezekano wa kulikabili neno hili HITAJI, katika jambo hili pamezaliwa vitu vingi sana mathalani ndoa, urafiki, uadui, mateso na hata furaha ya kitambo.

Ni kweli unatambua uhitaji ulionao kwa uhalisi au kunaushawishi mwingine ambao unakupa msukumo wa wewe kuona uhitaji! Katika haya unaweza ukaambiwa au kujua hasa wewe unahitaji nini? Hivyo lazima utambue msingi wa uhitaji wako umebebwa na nini?

Nipende kusema kwamba kila rika katika ukuaji wa mwanadamu na katika hali stahiki kunauhitaji wake ambao kiukweli unaweza kuwa tofauti mkubwa au sio mkubwa katika hatua nyingine.

Ni kuulize swali moja tu unaelewaje neno hili HITAJI? Bila shaka unaweza kuwa na jibu zuri sana ambalo moyo wako utaliamini na kulipenda sana kwakua ni jibu lako! Na hakuna ataye kurekebisha au kukupinga kwakua ndicho kitu unachokiamini na kuona fahari katika hilo.

Katika hatua za mwanadamu;
i.mtoto aliye ndani ya tumbo la mama
ii. mtoto aliyetoka ndani ya tumbo la mama
iii.kijana
iv.mtu mzima
v.mzee

katika hatua zote hizo kuna mahitaji maalum ambayo kila hatua inahitaji katika utashi wa nafsi yake ni kubaliane na wazo hili kuwa kuna mahitaji ya msingi na mahitaji yasio ya msingi, japo mahitaji ya msingi mtu anaweza kufanya yasiwe ya msingi na yasiyo na msingi ya kawa na msingi kwa mtu husika.

Ni kubaliane kwa pamoja kuwa wanaweza kuwa wanawake kumi wenye rika moja lakini kila mmoja anaweza kuwa na hitaji tofauti tofauti kulingana na changamoto zinazo mkabili………wako watakao hitaji nyumba bora, mtoto, mume, uponyaji(tiba), mali, amani, gari n.k na kila mmoja hitaji atakalo kuwa nalo bila shaka wengine litakuwa linawatesa sana kwakuto kuwa nalo na wengine watachukulia swala linalo hitaji muda zaidi kwa kuwa na moyo wa uvumilivu.

Kwa wale ambao uhitaji wao au wake utakuwa ukiwatoa machozi na ndani ya miyo wao wataamini kuwa kama hitaji lake litafumbuliwa katika maisha yake bila shaka litachimbuka furaha na kicheko kilicho jificha katika maisha yake.

Ukitaka mtu akuzarau na kuona wewe sio kitu jaribu kuuzarau huo uwitaji wake ambayo kwa hilo yeye anakosa usingizi, na kuzalisha mateso katika moyo wa mtu, lakini katika hili ni kubaliane kuwa nguvu ya uhitaji utegemea akili yako na nani aliye karibu yako……anaweza kuondoa mzigo uliondani yako.

Je! Ni kweli uhitaji ulionao unaweza kukufanya uishi au kuishi ndiko kunaweza kukupa uhitaji ulionao……uhai ni bora kuliko uhitaji!

Naamini kuwa uhitaji wako ndio maumivu yako na inaweza kuwa furaha yako na naam inaweza kuwa huzuni yako!!
Katika yote utambue kwamba;


WEWE NI HITAJI LA MUNGU
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………0764 018535